‘ Kada ‘ zinazochochea Rushwa / Ufisadi nchini Kenya ni hizi Tatu je kwa Tanzania yetu ni zipi ili tuwe nazo makini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,054
107,538
Hatimaye Bosi Mkuu wa TAKUKURU ya nchini Kenya amevunja ‘ ukimya ‘ na kusema kwamba kama kuna ‘ Kada ‘ ambazo ndiyo Vyanzo na Vichocheo vikubwa na matendo ya Rushwa / Ufisadi nchini Kenya basi ni za Wanasheria ( Lawyers ), Wahandisi ( Engineers ) na Wahasibu ( Accountants )

Ameziomba hizi ‘ Kada ‘ Tatu Kujitathmini haraka na ikibidi wabadilike kwani ni wao ambao ndiyo wanaichafua nchi ya Kenya kwa tabia zao za ‘ Kuchochea ‘ na ‘ Kusababisha ‘ Vitendo hivi vya aibu na vinavyowanyima haki Wakenya wengine vinginevyo sasa ataanza kuwaweka hadharani kwa ‘ Kuwaumbua ‘ mmoja mmoja ili Wananchi wa Kenya wawajue.

Namsubiri sasa na Bosi wa TAKUKURU yetu hii hii ya Tanzania nae bila Kupepesa macho, Kutikisa masikio wala Kumung’unya maneno na Yeye atuwekee hadharani ‘ Kada ‘ zake kama ni Tatu au Tano ambazo ana uhakika nazo kuwa na zenyewe ndizi ‘ vinara ‘ wa Rushwa / Ufisadi. Binafsi nina ‘ Kada ‘ moja ambayo naijua na naamini hata Watanzania 99.9% nao wanaijua sasa ole wake isiwepo katika hiyo ‘ line-up ‘ yake.

Nawasilisha.

Chanzo: African News.com
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom