Kada wa CUF auawa Kwimba; Ushabiki wa kisiasa wahusishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kada wa CUF auawa Kwimba; Ushabiki wa kisiasa wahusishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ntamaholo, Oct 29, 2011.

 1. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Habari JF,
  CCM wilayani kwimba, mkoani Mwanza, wameua kwa kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake mtu aitwaye NDULLU MABEJA 50YRS, aliyekuwa ni kampeni manager wa mgombea wa udiwani CUF wakati wa uchaguzi uliofanyika hivi karibuni ulipelekea mgombea wa CCM ambaye mpaka sasa nimenasa jina lake moja la MAJALIWA kushindwa vibaya katika uchaguzi huo.

  Tukio hili la kinyama, limetokea katika kijiji cha Mhulya, kata ya Ngula, tarafa ya Ngula wilaya ya Kwimba,, mkoa wa Mwanza.

  Majaliwa ametajwa na wakata mapanga waliofika nyumbani kwa marehemu usiku wa manane, wakamkuta NDULLU MABEJA akiwa amelala na mke wake VALENTINA NGAIGE 45YRS na kuanza kumkata mapanga huku wakisema, wao WASILAUMIWE bali alaumiwe Majaliwa aliyekuwa mgombea wa CCM kwa kuwa ndiye aliyewalipa pesa na kuwatuma kuua ili kummaliza kwa kosa la kufanikisha ushindi wa mgombea wa CUF.

  CCM wamemwachia mke wa Ndullu ujane na mzigo wa kutunza watoto just kwa uroho wa madaraka.

  Chanzo. Mdau aliyesindikiza mke wa marehemu kituoni kutoa taarifa.

  Nawasilisha
   
 2. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hatafanywa lolote huyo maana walioua Igunga hadi sasa ni kimya maadamu tu ccm imehusishwa ingekuwa ni cdm ungeshasikia.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,367
  Likes Received: 22,228
  Trophy Points: 280
  Chama cha Machinjachinja hamta tawala milele.
  Mungu ailaze pema roho ya marehemu
   
 4. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Too painfull...mpaka lini?
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,250
  Trophy Points: 280
  Hivi wauaji wanaotumwa wanasemaga kabisa nani kawatuma? Tena wakati wa tukio? Curious!
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mafia mkubwa wewe unalala ukiamka unaota mauaji tu, si ungeenda LIBYA ili hasira zako zipungue
   
 7. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We ni gamba nini?
   
 8. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,277
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Inaezekana,
  1. kama alekutuma humpendi lakini inakubidi kufanya hiyo kazi upate pesa?
  2. Labda ni technic ya alekutuma ili kutilia shaka habari za mauaji hayo.
  3. Au wauaji kama binadam wengine waliingiwa na huruma ikabidi kumtaja alewatuma.

  Ni theory tu.
   
 9. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Duu hiii kali
   
 10. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  bujibuji tuna kazi ya kufanya, kulalamika haitatusaidia. ueona na sheria ya katiba wanayotaka kuirudisha tena bungeni? kwa mtindo huu tusitegemee uhuru wetu mkuu
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  ndo nature ya watawala unaowataka Mzee wa Rubisi
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  umaskini unakufanya uwe mwehu. kile usichokipenda utakifanya na kile unachokipenda hutopata nafasi ya kukifanya, kwani magamba lazima wakunyime nafasi. Kwa mwenye link na polisi W kwimba, atapata maelezo kamili huko
   
 13. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Umafia wangu uko wapi? kutoa taarifa ya mauaji yaliyotokea na wala siyo tetesi, ni ishu ya kweli? Nahisi wewe umehusika kupanga mauaji hayo. malipo ni hapahapa tu
   
 14. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  inatokea sana tu, kwani mara nyingi wanaotumwa nao huwa hawapendi ila kwa kuwa na ugumu wa maisha they opt to do. Hata hivyo, hizo ni tuhuma zilizoripotiwa kituo cha polisi, mahakama italifanyia kazi na haki itatendeka. Ingawa pia huwa sina na mahakama kwani zote ni mali ya CCM kwa kiasi kikubwa.
   
 15. O

  Omr JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe uliwaona CCM wanaua? Au ndio propaganda zenu nyie CDM, mnaua nyie halafu mnasingizia CCM.
   
 16. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,957
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Pole mjane! Mpe ushauri awaloge hao Magamba tu wahamishiwe Gamboshi.
   
 17. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  maelezo yako yanaonyesha ulikuwepo wakati wa tukio, tuambie kati ya wewe na ccm hasa nani kaua!!
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mm binafsi sina chama,lakini km great thinker,hii tarifa imeandikwa hisia,chuki na haiko neutral!no objectivity..sijawai kuskia muuaji anajitaja zaidi ya yule alshabab aliyehukumiwa kenya..mleta mada ametudanganya.ni mchochezi.
   
 19. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  hivi hawa waathirika wa vitisho na mauwaji wakiamua kulipiza Tanzania patakalika kweli?
   
 20. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hii ni mbaya sana...........................
   
Loading...