Kada wa CHADEMA akutwa amefariki Igunga!

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
TANZIA YA KIFO KWENYE UCHAGUZI IGUNGA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ubungo Mkoa wa Kichama wa Kinondoni Kanda Maalumu Dar es salaam kinasikitika kutangaza kifo cha mwanachama Mbwana Masoud kilichotokea wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.

Marehemu Mbwana Masoud alikuwa ni mmoja wa wanachama walijitolea kusafiri kwenda Igunga kwa ajili ya kuwa wakala kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 2 Oktoba 2011. Marehemu Mbwana Masoud alitoweka katika mazingira ya kutatanisha wilayani Igunga tarehe 2 Oktoba 2011.

Baada ya jitihada za viongozi wa chama kumtafuta marehemu kushindikana Mwenyekiti wa Chama Mkoa wa Kinondoni ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, John Mnyika (Mb) alitoa taarifa polisi tarehe 3 Oktoba 2011 na kufungua jalada RB/748/2011.

Tarehe 9 Oktoba 2011 wananchi wilayani Igunga walikuta mwili wa marehemu ukiwa porini katika eneo ambalo linajulikana zaidi kama msitu wa magereza.

Taarifa ilitolewa na wananchi kwa diwani wa kata ya Igunga Vicent Kamanga (CHADEMA) ambaye alifika katika eneo hilo na baadaye maafisa wa polisi walifika na kupeleka mwili huo katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Tarehe 9 Oktoba 2011 Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alitembelea nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Kwa Jongo Kata ya Makurumla kuifariji familia ya marehemu na kukubaliana na ndugu wa marehemu kutuma wawakilishi wa chama na familia kwenda Igunga kuhakiki mwili uliopatikana.

Tarehe 10 Oktoba 2011 wawakilishi wa familia wakiwa pamoja na Katibu Mwenezi wa Chama Wilaya ya Ubungo Ali Makwilo walishuhudia mwili husika na kuthibitisha kuwa ni wa marehemu Mbwana Masoud.

Leo Tarehe 11 Oktoba 2011 mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kidaktari (post mortem) kuweza kubaini chanzo cha kifo na ripoti wamepatiwa jeshi la polisi. Hata hivyo, mazingira ya kupatikana kwa mwili wa marehemu yanaashiria marehemu Mbwana Masoud aliuwawa.

Kutokana na hali ya mwili wa marehemu, maziko yatafanyika leo tarehe 11 Oktoba 2011 alasiri katika kata ya Igunga yakihusisha wawakilishi wa familia ya marehemu, viongozi wa chama, wanachama na wananchi wa maeneo husika kwa ujumla.

Viongozi waliopo kwenye maziko hayo ni pamoja na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Tabora, Halfan Athumani, Diwani wa Kata ya Igunga Vicent Kamanga na aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga kupitia CHADEMA, Joseph Kashindye.

Hitma ya Marehemu itafanyika hapa Dar es salaam nyumbani kwa marehemu Mtaa wa kwa Jongo Kata ya Makurumla tarehe 13 Oktoba 2011 saa 7 mchana baada ya swala ya adhuhuri na itahudhuriwa na viongozi waaandamizi wa chama ngazi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika.

Chama kitaendelea kuwa pamoja kwa hali na mali na wafiwa katika kipindi hiki kigumu na kinavitaka vyombo vya dola kuharakisha uchunguzi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wahusika. Marehemu amekufa akiwa katika safari ya kulinda haki na kutetea demokrasia na maendeleo; apumzike kwa amani.

Imetolewa tarehe 11 Oktoba 2011 na:

Nasor Balozi
Katibu-Wilaya ya Ubungo
0713/0767/0783-636676
[/QUOTE]

Ni simanzi kubwa; Wa-Tanzania sasa tutambue kwamba mauaji ya kisiasa yamefika katika nchi ya Mwalimu Nyerere ambako mambo kama haya yalikua ni ndoto kubwa.

Kamanda unaonekana kufa KWA MATESO MAKALI MNOO HUKU UKITETEA HAKI NA NCHI YETU, kifo chako motisha wa kuendeleza mapambano zaidi mpaka damu ya mwisho.

Pumzika kwa amani!!!!!!!!!!!


Burial has taken place, sensitive picture has been removed, please do not repost. Thanks !

11th October 2011 19:26


11th October 2011 19:23


11th October 2011 19:22



11th October 2011 19:21
 
Endelea kutujuza. Kuna wanachadema yoyote aliwekwa ktk gereza hilo? Kama wapo, vipi hali zao? Hiyo maiti ina majeraha yoyote?
 
Sijaelewa ngoja nisubirisubiri kidogo, maana sijasikia kuwa CHADEMA imeripori habari kwamba wakala wake amepotea. Nani kwa nini atambulike kwa hiyo title ya wakala badala ya raia wa Igunga pana kitu hapo.
 
mkuu jitahidi urudi haraka!
kwani kuna watu walikuwa gerezani? nahuyo mtu wamejuaje kama alikuwa wakala wa chadema mkuu?
dah mambo magumu sana!
 
Kama ni kweli itakuwa bad news kwa wana familia na wana Igunga lakini pia kwa Taifa zima maana tunako elekea hakutakiwa salama kabisa haya yakianza .
 
Alipotea usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura kny uchaguzi mdogo jimboni igunga. Alikuwa ni miongoni mwa makada wa cdm walioletwa kusimamia uchaguzi akitokea temeke (Dar) leo hii mwili wa marehemu umeokotwa nyuma ya gereza la igunga ukiwa umeharibika vibaya sana! Bwana alitoa na bwana ametwaa hakika damu ya mpigania haki haitamwagika bure, itakuwa mbegu ya mapambano dhidi ya udhalimu wa aina yoyote ile. Amen!
 
Endelea kutujuza. Kuna wanachadema yoyote aliwekwa ktk gereza hilo? Kama wapo, vipi hali zao? Hiyo maiti ina majeraha yoyote?
Kuna maakala zaidi ya wanne walipotea na ilikuwa vigumu kufatilia kwasababu ya mawasiliano duni huko ingunga kwani kuna baadhi ya kata hakuna kabisa mtandao...na polisi walikuwa waki wakamata wana wapeleka nzenga au sehemu nyingine mbali kiasi kwama kufatilia inakuwa vigumu kama huna taarifa kapelekwa wapi....
 
Maiti ya mtu anayesadikika kuwa alikuwa wakala wa Chadema imeokotwa nyuma ya Magereze.

Barabara zimefura raia.

Wana-Igunga wanasema hawana mbunge.

Dk. wa Manzese asikanyage Igunga.

Abari ndo iyo.

Live kutoka kwa Wajikoni Igunga.

Kama sababu za kifo chake ni siasa litakuwa jambo baya sana na vyombo vya dola vitapaswa kuwajibika katika hili.

Wa jikoni fuatilia kwa undani kujua chanzo na sababu za kifo cha huyo mtanzania mwenzetu.
 
Juzi nilianzisha thread yenye title : Polisi, ni wapi alipo Musa wakala wa CDM Igunga? nipo kwene cm ila ningeweza kuipost hapa au MOds waunganishe ili itupatie picha kamili, alitoka Dar na alikwenda kusimamia uchaguzi Igunga, kama kuna mtu anaweza kuiunganisha na kuweza kurudi nyuma kuona yaliyotokea! Pole kada damu yako tutaikumbuka daima na ikawe chemchemi ya chimbuko la mageuzi ya kweli na ya kudumu! amen
 
Wa Jikoni rudi haraka utupashe kinachoendelea, nataka kupasuka kwa hasira. Kama wamemuua wakala basi wamewasha moto wa vita ya wenyewe kwa wenyewe Tanzania. Kama CCM wanalitaka jimbo hadi kufikia kuua watu ina maana dhamira yao sio kuongoza nchi, kuna kitu wanalinda. To hell Mr M.kwere...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom