Kada wa CCM: Watanzania wanahitaji maendeleo zaidi kuliko wingi wa wabunge wa CCM

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
TUKIENDELEA KUWABEMBELEZA WANAOHAMA CHAMA NCHI ITAKUWA KWENYE UCHAGUZI KILA SIKU.

Na Thadei Ole Mushi.

[HASHTAG]#Kuna[/HASHTAG] tofauti kati ya adhabu na na motisha. Hizi ni dhana mbili zenye lengo la kuimarisha tabia au kuikomesha tabia.

*Adhabu* Ni kichocheo kinacho tolewa ili kufuta tendo au mwitiko ambao hakubaliwi au si mzuri kwa mtazamo wa jamii. Ni hali ya kumfanya mtu asirudie kosa au jambo ambalo amelifanya au amekuwa akilifanya mara kwa mara.

*Adhabu* ni tofauti na motisha wakati adhabu ikiwa na lengo la kukomesha jambo flan kujirudia motisha kwa upande wake hutolewa kwa lengo la jambo flan kujirudia.

*Katika* scenario ya Shule sisi waalimu tunajua ni wakati gani wakutumia mambo haya mawili, adhabu huwa tunazitoa pindi mwanafunzi anapokuwa amefanya jambo ambalo haliendani na maadili yetu na motisha huwa tunautoa pindi mwanafunzi anapofanya jambo zuri. Mfano kama mwanafunzi ana tabia ya kuchelewa shule sana au ni mtoro huyu tunampatia adhabu na si Motisha. Na kama mwanafunzi anafanya vizuri Darasani sana huyu tutampa motisha ili jambo hilo liendelee kujirudia.

WANAOHAMA TUNAWAPA MOTISHA BADALA YA ADHABU.

*Kuna* utaratibu umeibuka usiokuwa Rasmi wa mtu kujiuzulu uanachama wa chama chake na kuachia nafasi zote za kiuongozi halafu akihamia upande wa pili anapewa fursa ya kugombea tena.

*Kwangu* hii ni Motisha na kwa sababu hiyo tabia hii itadumu milele. Kwa motisha hii wengi watashawishika kuhama na taifa litaendelea kupoteza mamilioni ya fedha kwa ajili ya Uchaguzi.

*Watu* wengi wanalia sio kwa sababu wamepoteza mwanachama wao bali wanalilia gharama za uchaguzi. Fedha zinazopotea tungeliweza kuzitumia kufanya mambo mengine mengi tu. Ni jukumu letu kuzuia hali hii isiendelee kuliko kuiwekea Mbolea tabia hii. Hili ninalolizungumza litaeleweka kwa kila mtu mwenye utashi na mapenzi mema na nchi hii.

*Nakumbuka* kuna fedha ziliwahi kurudishwa na tume ya uchaguzi tukazielekeza kwenye madawati. Tunataka tuimarishe tabia kama hiyo na si kuchochea wao kuondoka.

IMPACT YA KINA MTULIA NA WINGI WA WABUNGE WA CCM.

*Watu* aina ya kina Maulid Mtulia na Dr Moleli tukiangalia historia zao hatuoni chochote alichokifanya kwa wananchi wake kabla ya kuhama chama. Sisemi hivi ili anyimwe ubunge lah hasha nasema hivi ili tubadili fikra na dira zetu katika kuharakisha maendeleo ya taifa hili.

*Hawa* kina Mtulia na baadhi ya wananchi wanaamini kuwa walishindwa kutekeleza yale walioahidi kipindi wakiwa upinzani kwa kuwa walikuwa upinzani ila wakienda CCM chama tawala watafanikiwa kuyatekeleza.

*Sijui* kwa nn wanaamini hivyo ila mimi naona ni kukosa ubunifu binafsi. Niliwahi kusema jukumu la mbunge na viongozi wetu si kuomba misaada serikalini tukifanya hivyo tutachelewa sana kwenye swala la maendeleo.

*Jukumu* lao kubwa ni kuunganisha nguvu za wale anaowaongoza ili wajiletee maendeleo. Kama wananachi wataambiwa ukweli na wakahimizwa kuchangia na Serikali ikaweka mkono wake basi kila mbunge atafanya vizuri.

*Watanzania* wanahitaji maendeleo zaidi kuliko wingi wa wabunge wa CCM au CHADEMA. Tuchukulie mfano kwa wingi wa wabunge wa CCM kwenye mabunge yaliyopita walifanya nn? Si haya madudu yanayorekebishwa leo na Mh Rais? Kumbe basi wingi wao sio hoja bali hoja je wanaweza kusimamia serikali yao ili wananchi wapate maendeleo?

*Kwa* siku za Karibuni ninaona baadhi ya viongozi wakijitahidi kweli kutoa misaada kwa watu maskini. Kwa upande wangu naona kama viongozi hawa wanatoa tu panado kwa malaria inayopanda kichwani.

Badala ya kujikita kwenda kuomba misaada wajikite kwenye kutengeneza sera. Sera ambayo itakuwa ni solution ya tatizo husika kwa muda mrefu badala ya kutoa misaada.

*Naamini* kiongozi huwa muda wake unaweza kuisha lakini atatuachia sera na dira itakayokuwa inatusidia pindi yeye akiwa hayupo.....

Ole Mushi.
0712702602
 
Hakika kada wa chama tawala amesema ukweli mtupu.
Bado tutaona madiwani na wabunge wengi wakihama vyama vyao hasa vya upinzani kwa sababu kuu mbili :
1) Kushawishiwa kwa ama fedha au vyeo.
2) Kuona kuwa CCM ndio sehemu ya kupata ushindi wa bwerere age kocha au Kipa ushindi ni lazima.
Sababu hii ya pili ni mbaya sana mana itafikia mahali watu wataanza hata kutoana roho ili nafasi ziwe wazi waende kuchukua ubunge tu kirahisi mana hakuna tena uchaguzi mana ushindi ni suala la Msimamizi wa uchaguzi kumtangaza mgombea wa CCM kuwa ameshinda iwe kwa kupata kura nyingi au chache ,ushindi ni lazima.

Kwa haki hii kila MTU atakimbilia kule panapompa nafasi ya kushinda bila kupingwa na hata akipingwa nguvu inatumika kumpa ushindi.

Watu wanamuunga mkono mkuu wa nchi kwa kulisababishia hasara Taifa.
Hili kwa sasa halipendezi.
Uchaguzi ni hasara kubwa sana. Kuna madiwani kule Mbeya wanakimbilia misaada ya mifuko 20 ya sementi na kulisababishia hasara ya mabiliani Taifa letu kurudia uchaguzi. Yote hiyo ni jeuri ya Kuona kuwa hata uchaguzi ukirudiwa wao waliosababisha hasara watapewa nafasi ya kugombea tena na watatangazwa kwa nguvu au watapita bila kupingwa.

Pakiwa na Demokrasia ya kweli kila MTU ataheshimu kura . Kila MTU ataogopa kuwachezea wananchi kwenye kuomba kura Mara mbili mbili bila kuwajibika kama wewe badala ya kutembelea nyota ya MTU kama ilivyoleo. MTU huko jukwaani kwa kutumia jina la MTU kuwa namuunga mkono hivyo munipe kura bila kusema kuwa we we umefanya na utafanya nini zaidi ulichoshindwa kufanya.
 
Wewe jamaa sijui umekunywa dawa gani hadi ukapona, wape na CCM wenzio nao wapone. Maana mkipona kuanzia wanachama hadi Mwenyekiti, naamini nchi pia itapona. Nakuombea ule ugonjwa usikurudie tena.
 
Nadhani hili wanapaswa kulijua fika wa chama tawala kuwa hamahama haina tija yoyote juu ya ustawi wa nchi zaidi ya kuturudisha nyuma maana hizi chaguzi zinatumia gharama kubwa achilia mbali baadhi ya sehemu tumeshuhudia vurugu na watu wakiumizwa wengine wakipatwa na vilema pia. Hivyo basi hatuna budi kutoshabikia huu mwendo wa kuhama hama unaoendelea kutoka upinzani kuelekea chama tawala nadhani si busara kwanza kumchagua kiongozi ambaye anayumbishwa na upepo wa kisiasa leo kijani kesho bluu, kiongozi wa namna hiyo hatufai hata kidogo kwanza anapaswa kupuuzwa.
 
Back
Top Bottom