- Tumeona mara kadhaa Jeshi la Polisi likikimbilia mbio kuwashika watu wanaotumia mitandao ya kijamii wanaotukana viongozi wa kisiasa wanaotoka kwenye chama tawala, lakini wanapotukanwa viongozi wa Upinzani huwa wanasema hawana Intelenjesia hiyo. Hivi sasa ni wiki tokea mtu mmoja anayeitwa Abdalla Saleh aliporekodiwa anaMtukana kiongozi wa Upinzani Zanzibar, amemtukana matusi ambayo ni kikomo cha matusi na chuki isiyomithilika. Amesema kuwa kiongozi huyo analawitiwa. Bw Abdalla pia amefika kiwango cha kudhalilisha dini na waislamu kwa Ujumla na kusema kuwa Mtume Muhammad Saw alikuwa analawitiwa.
Kuna watu wameshitakiwa kwa kmuita kiongozi wa Chama tawala BWEGE, wapo wenye kesi kwa kutamka kuwa tupambane na DIKTETE UCHWARA, lakini pia wapo waliofikishwa mahakamani na kuyimwa dhamana kwa kuhadithia ndoto zao, na zaidi ya yote wapo waliohijiwa kwa kumuita kiongozi wa chama tawala MTUKUFU.
Bw Abdalla pamoja na kukiri makosa hayo katika video mbili bado bado anatembea kifua mbele.