Kada wa CCM: Mandamano ni upuuzi, yaishe... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kada wa CCM: Mandamano ni upuuzi, yaishe...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RMA, Dec 24, 2010.

 1. R

  RMA JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchangiaji mmoja amehoji hapa kwamba maadamano ya upuuzi yatakwisha lini? Amewataka wananchi watulie kwa vile uchaguzi umekwisha na CHADEMA wasilete chokochoko. Waiache ccm iendelee kutekeleza sera zake. Ni swali zuri. Nampongeza. Naomba ndugu yangu nikupe "lecture". Chukua kalamu na karatasi unakili points zifuatazo na uzitafakari. Ni kweli maandamano yanayofanyika sehemu mbalimbali nchini ni ya kipuuzi lakini yana mwisho wake, yatakwisha iwapo:

  1. Nchi itakuwa na utawala bora na utawala wa sheria.
  2. Ufisadi utatokomezwa na watuhumiwa wote kufikishwa mahakamani.
  3. katiba mpya itaundwa na kuridhiwa na wananchi wote.
  4. CCM ambayo ndio chanzo cha maandamano ya kipuuzi itang'oewa madarakani.
  5. Maliasili itatumika kwa faida ya wote
  6. Jeshi la polisi litatenda haki kwa vyama vyote na si kuwa jeshi la ccm au chama kingine.
  7. Sheria ya nchi itakuwa na usawa kwa wote na sio wengine kuwa juu ya sheria.
  8. Maadili ya uongozi yatarejeshwa na uzalendo wa nchi utazingatiwa.
  9. Kazi za kitaalamu zitapewa vipaumbele na motisha mzuri kuliko siasa kama ilivyo hivi sasa ambapo nchi imedumaa kwa vile wataalamu wote wameparamia siasa kwenye masilahi mazuri. Wengine wanakimbilia masilahi nchi nyingine.
  10. Maisha vijijini yataboreshwa ili watu wasisongamane mijini.
  11. Maadili na moyo wa kufanya kazi kuzingatiwa.

  Mlolongo ni mrefu unaweza kuongeza. Zitunze points hizo uwe unajisomea kila siku. Lakini iwapo kweli mang'amuzi ya kiakili ni mapana, hata kama wewe ni miongoni mwa mafisadi, bado unaweza kugundua kuwa CCM ndio chanzo cha migomo ya kipuuzi kama unavyoiita. Uamke basi kutoka usingizini na utambue kuwa mtu asiyedai haki yake ndiye mpuuzi! Mtu anayejali masilahi binafsi na kuikumbatia dhuruma, ndiye mpuuzi. Lakini hao wanaoandamana kudai haki kwa ajili yao na ndugu zao, sio wapuuzi hata kidogo!
   
Loading...