Kada wa CCM atangaza kumvaa Mh. Kikwete nafasi ya uenyekiti taifa...

Status
Not open for further replies.

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maliki Marupu kutoka wilayani Ulanga, mkoani Morogoro, ametangaza nia kuwania nafasi ya uenyekiti wa CCM taifa, inayoshikiliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Marupu ambaye amejitambulisha kuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa, alisema kuwa amefikia hatua hiyo ili kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho tawala.

Wiki iliyopita, gazeti hili liliripoti taarifa za kuwapo kundi linalompinga Rais Kikwete kutaka kutenganisha kofia ili asiendelee kuwa Mwenyekiti wa CCM taifa, na kumpa nafasi ya kubaki kwenye kiti cha urais.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Marupu alisema kama fomu za kuwania nafasi hiyo zitatolewa, ataandika historia mpya ndani ya chama hicho.

Hata hivyo, chini ya utaratibu wa sasa wa CCM, nafasi ya mwenyekiti taifa haigombewi, bali jina la mgombea ambaye kwa kawaida huwa ni Rais wa Muungano huteuliwa na Kamati Kuu (CC), kuthibitishwa na Halmashauri Kuu (NEC) na hatimaye kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu.

Huku akinukuu Katiba ya CCM, alisema ibara ya 14 kifungu kidogo cha 3, kinampa nafasi mwanachama yeyote ndani ya chama hicho kuwania nafasi katika ngazi yoyote.

"Unajua lazima tuwe wazi. Kinachoogopwa hapa ni kama ikitokea mwenyekiti akawa sio rais, iwapo patatokea kutoelewana kati yao, basi mwenyekiti wa chama ana uwezo wa kushawishi wanachama wakamvua madaraka rais," alisema.

Marupu alisema, utaratibu unaotumika wa kumpata mwenyekiti, umekuwa ukidumaza demokrasia ndani ya chama hicho.

Kada huyo alisema, wapo watakaomuona msaliti ndani ya chama, lakini amelazimika kuwania kiti hicho kuleta mabadiliko yanayoenda na wakati.

"Wajumbe wakinipitisha, mchuano wangu na Kikwete utakuwa kama ule uliowahi kutokea nchini Afrika Kusini kati ya aliyekuwa rais, Thabo Mbeki na rais wa sasa Jacob Zuma aliyeibuka mshindi," alisema.

Chanzo:
Tanzania Daima
 
mfumo utamkwamisha tuu huyu unless awe anatumiwa na kundi linalotaka kofia ya urais na mwenyekiti zitenganishwe....ila nae aangalie mambo mengine haya na mtazamo wa uhaini hasijetokea Mkenya aka Mlimboka bure...
Anyway Magamba kazi kwenu
 
Nafasi ya uenyekiti wa chama ilitangazwa lini?????? au iko wazi???????? kwani mwenyekiti ameenda wapi??????????
 
Mabwepande pana umbali gani kumbe tokea pale maguuguuni
 
Kada yeyote wa ccm akitangaza nia kama hiyo waungwana tunamtafsiri kama anatumiwa na anataka kuosha jina ili awekwe kwenye historia kuwa aligombe uenyekiti ili akumbukwe kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa inayolewa kwa kigezo cha shukrani tu.
 
Nadhani hili suala ni kubwa kuliko tunavyodhania; hawezi tu kada wa chama akakakurupuka kuwania nafasi hiyo bila ya kuandaliwa...; pia sidhani ni coincidence kwa suala hili kuhusisha kada kutokea mkoa wa morogoro, kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna shughuli nzito zinaendelea huko za maandalizi ya 2015 ambayo wengi hatuyajui; otherwise its a good idea but a bad move;
 
"kutokana na katiba ya ccm nafasi za mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa ccm hazigombewi mpaka muda wao uishe au vingenevyo sasa hizo form za hizo nafasi atapata kutoka wapi" haya ni maneno kutoka kinywani mwa VUVUZERA nape kupitia radio
 
Maliki Marupu ni mtu mwenye nia njema kabisa na CCM. Nadhani ni wakati sasa wana CCM kwa ujumla mumuunge mkono aweze kukisuka upya chama kuelekea 2015. Marupu for CCM Chairmanship!

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
nadhani huyo kaamua kutokuwa mnafiki kwa kumueleza wazi muu wa kaya kuwa ameche,ka mno katika kukiongoza chama na hata taifa.
 
Nadhan huyo jamaa ataibuka kidedea maana kwa sasa hata jiwe likigombea na jk litashind tu
 
Aiseee baba yangu haita kubadilisha wewe usiwe gamba utaendelea kuwa gamba milele
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom