Kada wa CCM anashikiliwa na polisi kwa kuwatishia wafuasi wa CHADEMA kwa bastola | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kada wa CCM anashikiliwa na polisi kwa kuwatishia wafuasi wa CHADEMA kwa bastola

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ruttashobolwa, Oct 14, 2012.

 1. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Kutoka Arusha jeshi la polisi lina mshikilia mfuasi wa CCM kwa kutaka kuwateka wafuasi wa CHADEMA walio kuwa kwenye harakati za maandalizi ya mikitano ya udiwani.

  Mtoa taarifa ameeleza ya kwamba wafuasi wa CHADEMA walikuwa kwenye harakati za kuandaa mikutano ya kugombea udiwani ghafla alitokea mfuasi wa ccm aliye kuwa amebeba bastola na kuwambia waache kuendelea na shughuli zao, baada ya purukushani kwa kuwa vijana wa cdm walikuwa wengi waliweza kumdhibiti na kumweka chini ya ulinzi na kuwaita polisi wamchukue!

  Kwa ufatiliaji ili onekana kuwa ulikuwa imepangwa kuharibu mikutano ya CHADEMA.

  Ninacho jiuliza ni kwamba kwa nini siasa zina tupeleka huku, leo kutishiana silaha imekuwa kawaida hasa wafuasi wa ccm na viongozi wao wame kuwa mstari wa mbele kutishia watu kwa silaha na wamekuwa wanaangaliwa yamkini wako juu ya sheria.

  Ni vyema CCM waka jua hii nchi siyo ya kwao ni yetu sote na safari yao wame iandaa wenyewe.

  Na kamwe CCM hamtozuia mabadiliko kwani ni wakati wake!

  Source: clouds fm (zilizo tufikia)
   
 2. M

  Magesi JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kwel mkuu
   
 3. g

  gagonza JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 309
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  kama ni kweli huo ni uchokozi wa dhahiri,lakini la pili ina onyesha wamesha zidiwa, na wamekata tamaa.
   
 4. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mfa maji daima haachi kutapatapa!!Huyo jamaa hakupewa kibano?
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  kama kakamatwa nampa pole sababu hata walio mtuma watamkana. vijana tuepuke kutumika kisiasa kwa manufaa ya wachache hasa wanamtandao.. mia
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Ndio hivyo wameamua kutumia silaha sasa!

   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Na inavyo onekana ilitumwa kabis.
  Sijui ule msemo wa sisiemu chama sikivu ndio maana yake!

  Hawa jamaa ni hatari na inaonesha wako tayari kumwaga damu ili mradi wasitoke madarakani.

   
 8. A

  Antar bin Shaddad JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  mtuhumiwa alipelekwa kituo cha polisi USA river but taarifa za sasa hivi ni kwamba ameshaachiwa huru baada ya viongozi wa juu wa CCM Arusha kuwapigia simu polisi
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Yan hii nchi sijui imefika wapi? Ndio maana wananchi wanashangilia wanapo sikia ma askari wame kufa.

   
 10. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Ni kata gani imetokea hii?? Daraja mbili au Bangata?? Na huyo kada wa ccm hajatajwa kwa jina?? Taarifa mbona haijitoshelezi
   
 11. C

  Chibolo JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 2,973
  Likes Received: 1,391
  Trophy Points: 280
  Wacha tuendelee kuchapana hivohivo make tuko kwenye kipindi cha mpito kwenye ukombozi kamili.
   
 12. MARCKO

  MARCKO JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 2,265
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Acha aachiwe kabisa! Kwanini nyie mkamwacha bila kumfinya?
   
 13. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  imetokea kata ya Bangata, kampeni meneja wa ccm anayefahamika kwa jina la Bosco akiwa na wenzake kutaka kuteka gari ya PA ya CHADEMA,akazidiwa nguvu na umma
   
 14. C

  Concrete JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Baada tu ya kumkamata kabla ya kuwakabidhi polisi, ilitakiwa kumpiga picha, kurecord video na sauti yake, kumbana ataje waliomtuma, kumchunguza vitambulisho vyake kumjua vizuri, kunakiri namba za bastola aliyokutwa nayo na mwisho kumpa kibano kizuri tu.
   
 15. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Na hivi viroba vilivyotapakaa mitaani,kuna haja ya busara kutumika kuliko wakati mwingine wowote!
   
 16. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  [h=3]CCM, Chadema watishia bastola Arumeru - Arusha Yetu[/h]


  Peter Saramba, Arusha


  POLISI wilayani Arumeru inamshikilia Kada wa CCM, Edward Simon maarufu kama Bosco kwa tuhuma za kumtishia kwa bastola mfuasi wa Chadema. Kada huyo wa CCM, anatuhumiwa kutishia kumuua kwa kumpiga risasi mfuasi wa Chadema, Boniface Kimario aliyekuwa akipita mitaani kutangaza mkutano wa hadhara wa chama chake uliotarajiwa kufanyika eneo la Sasi.


  Hatua ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ilikuja baada ya aliyetishiwa kufungua jalada la malalamiko Kituo cha Polisi cha USA-River na kupewa namba ya mashtaka USR/RB/4245/2012, kosa la kutishia kuua kwa silaha.


  Mtuhumiwa huyo aliyewekwa rumande baada ya kufikishwa kituoni hapo na polisi aliyekuwa akitumia usafri wa pikipiki.


  Mratibu wa Kampeni za Chadema katika kata hiyo, Henry Kileo alisema wakati akitishiwa kuuawa kwa kupigwa risasi, Kimario alikuwa akitekeleza jukumu la kutangaza mkutano wao wa hadhara na baadaye kwenda kumfuata mgombea wa Chadema, Peter Msere nyumbani kwake Kijiji cha Bangata.


  Kileo alisema wakati Kimario aliyekuwa kitumia gari aina ya Range Rover, ghafla mtuhumiwa alijitokeza na kuziba barabara kwa kutumia gari lake ndogo aina ya Rav 4 na kuchomoa bastola, kabla ya kutishia kumpasua kichwa kwa risasi.  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas alisema hajapa taarifa hizo, kwa sababu bado suala hilo linashughulikiwa na polisi wilayani Arumeru na kuahidi kufuatilia.  Mkoa wa Arusha unafanya chaguzi ndogo katika kata mbili za Bangata, Arumeru na Daraja II mjini Arusha ikiwa ni kati ya kata 28 zinazofanya chaguzi ndogo, baada ya nafasi hizo za udiwani kubaki wazi kutokana na sababu mbalimbali.

   
 17. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  CCM na risasi ni pua na kamasi.Leo ubabe wao umeanza kujulikana juzi wamemuua kada wa Barlow kule mwanza, na siku zote wanasema ccm na polisi ni kulwa na dotto.Mengi tutashuhudia mwaka huu.
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni aibu na fedheha kubwa kwa chama kikongwe kama CCM kuwakilishwa na wahuni wa barabarani kama huyu 'Aden Rage Al-Shaababu' wa huko Arusha.

  CCM ya miaka yetu hii hakichaguliki tena hata kwa bastola jamani mbona tu hamuelewi????
   
 19. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Atakuwa katumwa na kigwangala au bashe yule ambaye uraia wake unategemea matakwa ya riziwani na kikwete..
   
 20. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Wind of change has come to Tanzania! It is unstoppable by fire or flames!
   
Loading...