Kada wa CCM afa kwa kunywa gongo akishangilia ushindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kada wa CCM afa kwa kunywa gongo akishangilia ushindi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtoto wa Mkulima, Oct 31, 2007.

 1. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu hii nayo kali

  Kada wa CCM afa kwa kunywa gongo akishangilia ushindi
  Na Abdallah Nsabi, Maswa

  FURAHA ya ushindi wa Chama cha Mapinduzi CCM kupata ushindi wa Udiwani imemtokea puani mkazi wa kata ya Nguliguli Wilayani Maswa, Lonjini Petro (54) ambaye alikunywa lita tatu za pombe aina ya gongo na kufariki dunia.


  Tukio hilo lilitokea juzi katika kata hiyo baada ya kutangazwa matokeo ya ushindi wa chama hicho ndipo Petro alipokwenda nyumbani kwa Gumba Mboje na kuangiza lita tatu za gongo ili anywe afurahie ushindi huo ambao alikuwa anausubiri kwa hamu.


  Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa kifo cha marehemu Petro kilitokana na ulevi wa pombe haramu aina ya gongo wakati akisherehekea ushindi wa mgombea udiwani wa CCM.


  Chanzo cha habari kutoka katika eneo hilo kilisema kuwa Petro aliwekeana ahadi na mtu mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana kuwa iwapo chama cha CCM kingeshinda wangenunuliana pombe aina ya gongo na kunywa mpaka asubuhi.


  Inadaiwa kuwa mara baada ya ushindi wa chama cha Mapinduzi CCM, marehemu aliamua kujikita katika moja ya nyumba ambayo wanafanya biashara hiyo na kisha kuanza kunywa pombe hiyo haramu hadi kukutwa na umauti papo papo.


  Marehemu huyo ambaye enzi za uhai wake alikuwa kada wa chama hicho, siku hiyo alifurahi kupindukia baada ya chama chake kushinda ndipo alikwenda kunywa kinywaji hicho kufurahi ushindi wa mgombea wao.


  Baada ya kumwona mwenzao amezidiwa na kinywaji hicho kutokana na kuanguka chini na kuzimia walianza kumwagia maji ya baridi huku wakimpepea lakini baada ya muda mfupi aliaga dunia.


  Inadaiwa kuwa Petro alikuwa na kawaida ya kunywa pombe, lakini akuwahi kulewa kama ilivyotokea siku hiyo .


  Mbunge wa Maswa, John Shibuda, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mwanachama wa CCM na kuongeza kuwa hali hiyo ilimtokea wakati akishangilia ushindi wa mgombea wa CCM.


  Alisema marehemu aliaga dunia mara baada ya Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kumtangaza mgombea wa chama kwa ushindi ndipo alipoamua kupiga mayowe na kisha kuelekea katika moja ya nyumba iliyokuwa inafanya biashara hiyo na kuagiza lita tatu za gongo na kuzinywa

  http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=2625
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Duuh! Nimekimbilia kusoma haraka haraka nikifikiria KadaMpinzani nd'o ka... samahani sana Kada, simaanishi utani, it's true nimekimbilia hii thread...

  SteveD.
   
 3. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  Mambo ya kinywaji kikongwe hayo........kumbe sisiemu nao hawana adabu yaani wanakunywa gongo!!??. Pole nyingi kwa familia ya Petro. Jina la bwana lihidimiwe!!.
   
 4. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2007
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Duuh, ngosha mwanawane kafakamia Komoni. RIP.
   
 5. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  heheheeeee, duh hiyo kali steve-d ! umeniacha mbavu wazi, mie mzima bana !
   
Loading...