Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
Inaripotiwa kuwa jijini Arusha kada maarufu wa Chadema John Mushi almaarufu "kadogoo" usiku wa kuamkia jumatatu tarehe 21 June, 2021 nusura ajiue kwa sumu baada ya waliokuwa wabunge wa Chadema Joshua Nassari na Lijuakali kuteuliwa U-DC.
Baada ya kuzinduka akihojiwa na Mwenyekiti serikali ya mtaa Ndg. Motika, kijana huyo anayeishi maeneo ya Suye ameeleza kukerwa kuona akina Nassari na Lijuakali wakiteuliwa kuwa wakuu wa wilaya na Rais wa JMT Mh. Samia Suluhu Hassan. Kadogoo akiongea kwa unyonge amesema kuwa "siamini kama Nassari na Lijuakali leo ni ma-DC, kwa sasa baada ya kunusurika kifo nitajikita na kutafuta maisha,nimepoteza mali zangu kwa ushabiki wa siasa"
My take;
Kuna fundisho kwa vijana wa Chadema, wengi wanaingia kushabikia siasa jumla jumla. Kuna mwingine mwaka 2015 alijikata kidole baada ya EL kukosa urais. Wengi leo wapo hohehahe kwa ushabiki wa kijinga.