Kada CCM akamatwa na shehena ya sukari mbovu

MADABIDA.jpg

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ramadhan Madabida.

Kada CCM akamatwa na shehena ya sukari mbovu



  • Ni tani 100 hutumika kutengeneza ARV
Manispaa ya Temeke, mkoani Dar es Salaam imekamata shehena ya sukari nyeupe (industrial white sugar) mbovu ambayo hutumika kutengeneza dawa za kupunguza makali ya ukimwi (ARV’s) ambayo inamilikiwa na kiwanda cha kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ramadhan Madabida.Shehena hiyo ambayo ni tani 100 za sukari zilikamatwa kwenye ghala maeneo ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam zikiwa zinatolewa kinyemela kupelekwa Arusha tayari kwa matumizi.
Vyanzo vya uhakika viliiambia NIPASHE jana kwamba sukari hiyo hutolewa kwa usiri mkubwa kwenye ghala hilo lililopo barabara ya Mbozi-Chang’ombe na kwamba huwa halifunguliwi mchana au mara kwa mara.

Taarifa hizo zilidai kwamba inakadiriwa juzi takribani tani 10 za sukari hiyo ambayo imekwisha muda wake wa matumizi zilikuwa zinatolewa. Kufuatia mwenendo wa utoaji wa bidhaa kwenye ghala hilo, raia wema walianza kufuatilia na kubaini kwamba ni sukari ambayo inamilikiwa na kada huyo.“Jana (juzi), tukaona malori yamekwenda pale kama kawaida kuchukua mzigo, sisi tukawasiliana na viongozi wa kata kuwaeleza waje wakague kama kweli bidhaa zinazotoka huku ni salama…alikuja bwana afya, polisi pamoja na viongozi wengine,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kilieleza kwamba wakati Bwana Afya akiwa kwenye ghala hilo, alipigiwa simu na baadhi ya viongozi wa CCM wakimtaka kutochukua hatua zozote kwa kuwa suala hilo litampotezea kazi.Mmoja wa viongozi hao ni Diwani wa Kata mojawapo ya Manispaa ya Temeke, ambaye alimweleza kwamba ghala hilo linamilikiwa na mmoja wa viongozi wa CCM wanaoheshimika hapa nchini.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Naibu Mkurugenzi wa kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI), kinachotengeneza ARV’s, Zarina Madabida, alisema: “Nipo safarini subiri nikifika nitakujulisha.”Hata hivyo, NIPASHE ilimwandikia ujumbe mfupi wa mkononi kumsisitiza kuhusu umuhimu wa kauli yake kwa suala hilo na ndipo alipopiga simu na kuhoji:
“Hivi unaona hiyo ni habari?”


NIPASHE ilipomwambia ni kwa ajili ya manufaa ya umma alisema: “Ni kweli kuna sukari ambayo imeharibika tangu mwaka jana, tulikuwa tunaipeleka kiwandani Arusha ikakae tu kule.”Zarina ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), alisema: “Najua aliyekupa hiyo taarifa ni mtu mmoja ambaye alitaka nimuuzie kwa magendo, hiyo sukari nikakataa…kama unataka kuiandika utakuwa umenisaidia sana na utaisadia pia serikali japokuwa sioni kama ni habari.”“Hayo ndiyo madhara ya serikali kufunga kiwanda, ni kweli haifai kutengeneza dawa, lakini inaweza kutumika kwa matumizi mengine,” alisema Zarina.Hata hivyo, alisema hajui kiasi cha sukari hiyo na wala mwezi ambao imemalizika muda wake wa matumizi.

Badala yake alisema: “Nipo njiani naenda Mbeya na Kamati ya Bunge, nitarudi Jumapili ukinitafuta Jumatatu nitaweza kukueleza kwa undani suala zima.”
NIPASHE ilipomtafuta Bwana Afya wa Kata ya Chang’ombe ambaye alifunga ghala hilo, Mohamed Mrindoko, alithibitisha kufunga ghala hilo na kueleza kwamba bado jambo hilo lipo kwenye uchunguzi.
 
Haya haya hawa ndio kila siku kutwa kucha wanatoka mapovu kuwa masisiem yatatawala milele kwa ajili ya kuficha
maovu haya,hawa si ndio wana kashfa ya kutengeneza arv's fake?enyi watanganyika mnayaona haya?nepi njoo mtete kada wako hapa....
 
Jana polisi na baadhi ya maofisa wa manispaa ya Temeke walikamata shehena ya sukari nyeupe (industrial white sugar), ambayo hutumika kutengeneza ARV. Sukari hiyo imekwisha muda wake wa matumizi tangu mwaka jana lakini ilikuwa inatoka kwenye warehouse inayomilikiwa na RAMADHANI/ZARINA MADABIDA maeneo ya Mbozi road ikiwa inasafirishwa kwenda kiwandani Arusha...HIYO NDIYO TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO. Ngoja tusubiri tuone picha maana wakati ule wa ARVs walisimamishwa mabosi wa MSD cjui sahizi itakuwaje? Usikose kutazama filamu hii murua.

"KADA wa CCM huwa hakosei"
 
hivi hawa watu akili zao wanazotumia kufikiri ni sawa na za binadamu wengine!!!!? au kuna lishe tuliyoikosa Watanzania ambayo ingesaidia kutodumaa akili?
Chanzo hicho kilieleza kwamba wakati Bwana Afya akiwa kwenye ghala hilo, alipigiwa simu na baadhi ya viongozi wa CCM wakimtaka kutochukua hatua zozote kwa kuwa suala hilo litampotezea kazi. Mmoja wa viongozi hao ni Diwani wa Kata mojawapo ya Manispaa ya Temeke, ambaye alimweleza kwamba ghala hilo linamilikiwa na mmoja wa viongozi wa CCM wanaoheshimika hapa nchini.
 
Ninani atakayeweza kuwakamata mafisadi na kuwaweka ndani wote ?
Ninani anayeweza kuwafunga wote wanauza vitu fake?
Ninani anaweza kuwasweka gerezani wote wanaoeneza udini?
Ninani anayeweza kuwavua madaraka watawala walio dhaifu ?
Ninani atawalinda tembo na wanyama wetu wasiuawe na kutoroshwa?
Ninani atakayewakamata wezi wa madini yetu na gesi?
Ninani atakayehuisha mioyo ya watu waache uchu wautajiri haramu?
Mungu aturehemu taifa letu linazidi kuzama kwa sababu ambazo kila mtu anazijua lakini Ninani sasa wakubadili hali hii??
 
Na Restuta James|Ni tani 100 hutumika kutengeneza ARV


Chanzo hicho kilieleza kwamba wakati Bwana Afya akiwa kwenye ghala hilo, alipigiwa simu na baadhi ya viongozi wa CCM wakimtaka kutochukua hatua zozote kwa kuwa suala hilo litampotezea kazi. Mmoja wa viongozi hao ni Diwani wa Kata mojawapo ya Manispaa ya Temeke, ambaye alimweleza kwamba ghala hilo linamilikiwa na mmoja wa viongozi wa CCM wanaoheshimika hapa nchini.

CHANZO: NIPASHE
Yaani hapa kwenye nyekundu, panaweza kukufanya utamani hata kuingia mitaani kuiondoa serikali ya CCM madarakani. Hizi hoja za uenzetu ndiyo zinalitafuta hili taifa. Hivi kwanini viongozi wa CCM hawana utu kiasi hiki kwa wananchi?
 
Haya haya hawa ndio kila siku kutwa kucha wanatoka mapovu kuwa masisiem yatatawala milele kwa ajili ya kuficha
maovu haya,hawa si ndio wana kashfa ya kutengeneza arv's fake?enyi watanganyika mnayaona haya?nepi njoo mtete kada wako hapa....

Na hapo utashangaa kuna genge la watu wanaojiita usalama wa taifa, wanakesha mchana kutwa kuitetea na kuilinda CCM ili ibaki madarakani milele? Ninajuta kuwa mtanzania!
 
hao waliomkamata wangeanza na Kinana a.k.a mzee wa tembo.!
 
harakati za uchaguzi jamani, lazima wazikusanye kwa kila namna mpaka sanduku la vita limejaa full. nahisi kitu hatari inakuja sikilizia
 
Na hapo utashangaa kuna genge la watu wanaojiita usalama wa taifa, wanakesha mchana kutwa kuitetea na kuilinda CCM ili ibaki madarakani milele? Ninajuta kuwa mtanzania!
Hapo kwenye red imeniuma sana kwa kweli,watu tunakata tamaa hata ya kuwa watanzania?Shame masisiem....
 
Mwanzo » Habari




Kada CCM akamatwa na shehena ya sukari mbovu




NA RESTUTA JAMES



14th February 2013


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa







headline_bullet.jpg
Ni tani 100 hutumika kutengeneza ARV



MADABIDA.jpg

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ramadhan Madabida.


Manispaa ya Temeke, mkoani Dar es Salaam imekamata shehena ya sukari nyeupe (industrial white sugar) mbovu ambayo hutumika kutengeneza dawa za kupunguza makali ya ukimwi (ARV's) ambayo inamilikiwa na kiwanda cha kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ramadhan Madabida.

Shehena hiyo ambayo ni tani 100 za sukari zilikamatwa kwenye ghala maeneo ya Chang'ombe jijini Dar es Salaam zikiwa zinatolewa kinyemela kupelekwa Arusha tayari kwa matumizi.
Vyanzo vya uhakika viliiambia NIPASHE jana kwamba sukari hiyo hutolewa kwa usiri mkubwa kwenye ghala hilo lililopo barabara ya Mbozi-Chang'ombe na kwamba huwa halifunguliwi mchana au mara kwa mara.

Taarifa hizo zilidai kwamba inakadiriwa juzi takribani tani 10 za sukari hiyo ambayo imekwisha muda wake wa matumizi zilikuwa zinatolewa. Kufuatia mwenendo wa utoaji wa bidhaa kwenye ghala hilo, raia wema walianza kufuatilia na kubaini kwamba ni sukari ambayo inamilikiwa na kada huyo.

"Jana (juzi), tukaona malori yamekwenda pale kama kawaida kuchukua mzigo, sisi tukawasiliana na viongozi wa kata kuwaeleza waje wakague kama kweli bidhaa zinazotoka huku ni salama…alikuja bwana afya, polisi pamoja na viongozi wengine," kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kilieleza kwamba wakati Bwana Afya akiwa kwenye ghala hilo, alipigiwa simu na baadhi ya viongozi wa CCM wakimtaka kutochukua hatua zozote kwa kuwa suala hilo litampotezea kazi.

Mmoja wa viongozi hao ni Diwani wa Kata mojawapo ya Manispaa ya Temeke, ambaye alimweleza kwamba ghala hilo linamilikiwa na mmoja wa viongozi wa CCM wanaoheshimika hapa nchini.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Naibu Mkurugenzi wa kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI), kinachotengeneza ARV's, Zarina Madabida, alisema: "Nipo safarini subiri nikifika nitakujulisha."

Hata hivyo, NIPASHE ilimwandikia ujumbe mfupi wa mkononi kumsisitiza kuhusu umuhimu wa kauli yake kwa suala hilo na ndipo alipopiga simu na kuhoji:
"Hivi unaona hiyo ni habari?"

NIPASHE ilipomwambia ni kwa ajili ya manufaa ya umma alisema: "Ni kweli kuna sukari ambayo imeharibika tangu mwaka jana, tulikuwa tunaipeleka kiwandani Arusha ikakae tu kule."

Zarina ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), alisema: "Najua aliyekupa hiyo taarifa ni mtu mmoja ambaye alitaka nimuuzie kwa magendo, hiyo sukari nikakataa…kama unataka kuiandika utakuwa umenisaidia sana na utaisadia pia serikali japokuwa sioni kama ni habari."

"Hayo ndiyo madhara ya serikali kufunga kiwanda, ni kweli haifai kutengeneza dawa, lakini inaweza kutumika kwa matumizi mengine," alisema Zarina.

Hata hivyo, alisema hajui kiasi cha sukari hiyo na wala mwezi ambao imemalizika muda wake wa matumizi.

Badala yake alisema: "Nipo njiani naenda Mbeya na Kamati ya Bunge, nitarudi Jumapili ukinitafuta Jumatatu nitaweza kukueleza kwa undani suala zima."
NIPASHE ilipomtafuta Bwana Afya wa Kata ya Chang'ombe ambaye alifunga ghala hilo, Mohamed Mrindoko, alithibitisha kufunga ghala hilo na kueleza kwamba bado jambo hilo lipo kwenye uchunguzi.




CHANZO: NIPASHE








 
Mzee Ramadhan Madabida; Wewe ni kiongozi wetu mwandamizi wa chama.Hakika kama hiki kinachoripotiwa ni kweli, utakuwa umefanya aibu ya mwaka isiyovumilika.Nakusihi sana mzee wangu, kokote uliko jitokeze hadharani waeleze watanzania ni nini unachofanya hasa!.Nawashauri na viongozi wetu wengine wenye kashfa kubwa kumbwa kama ile ya pembe za ndovu wajitokeze mapema na kujieleza ama kwa kujisafisha au hata kuomba radhi.Zaidi ya hapo;Ninyi viongozi wetu na sisi wanachama wenu karibuni tutadhalilika; tena udhalilifu uliomkubwa kabisa! Itakabokaribia hali hiyo, wanachama wenu wazalendo ambao bado wako wengi watawakimbieni.Mnaweza mkajikuta mkiwa mmebaki ninyi wenyewe huku mkiwa hamna mfuasi hata mmoja.Najua hii inauma.Hata mimi betlehem inaniuma pia.Ila hata mtoto anaposhikwa na homa kali dawa ni sindano,JAPO inauma lakini ukimwacha atakufa.Ifahamike kwamba utu wa mtu ni zaidi ya chama na ushabiki wa kisiasa.Madabida na wenzako kazi kwenu.

 
ccm pango la majambazi,wanaofanya biashara haramu na mafisadi,si chama cha wakulima na wafanyakazi,ushauri wangu kwao; Waondoe ile alama ya jembe na nyundo
 
Back
Top Bottom