mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
BERNARD Membe, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesema, mazingira magumu ya Siasa kwa sasa, yamesababisha marafiki na wafanyabiashara kushindwa kuwasaidia. Na kwamba, kusuasua kwa kampeni hasa vyama vya upinzani nchini, kunatokana na ukweli kwamba, wagombea wengi wana ukata kwani hawana msaada tofauti na chaguzi zilizopita.
“Mnapokuwa katika mbio za urais, unatakiwa ukae ujipange kifedha na uwe na timu za kampemi, vyama vyote vyenye wagombea, wana ukata wa fedha sababu vyanzo vyetu vinavyokubalika kisheria, wafanyabiasha wanaotoa msaada wote wamekimbia, hatuna fedha,”
“Sababu nyingine, tunazuiliwa muingiza fedha, ukitaka kuingiza ama kutoa fedha, unakataliwa. Nikiwa rais, nitaboresha mfumo wa fedha kuiondoa changamoto hiyo,”
Akielezea sababu za kushindwa kuendelea na kampeni za urais kwa mujibu wa ratiba yake, amesema waliamua kusitisha kwa kuwa baadhi ya wagombea wa ubunge na udiwani kwenye chama chake waliwekewa pingamizi.
“Kilichotokea, baada ya kuteuliwa mgombea wa urais, sisi wabunge wetu zaidi ya 40 waliwekewa pingamizi.
Sasa akili inakutaka utafute changamoto ya tatizo kwanza. Huwezi kukurupuka peke yako, unawaacha wabunge na madiwani wamewekea pingamizi,” amesema Membe.
Akizungumzia safari yake ya Dubai Membe amesema, alikwenda kwa kuwa, ni ratiba yake ya kawaida kwa maana ndani ya mwaka mmoja anapaswa kwenda mara nne kutokana na shughuli zake binafsi.
“Kuna malalamiko kwanini ameenda Dubai kipindi hiki, huwa naenda Dubai mara nne kwa mwaka, kuna kampuni mimi ni mwanachama, sasa sikwenda mara mbili sasa nimeenda, lakini pia nimekwenda kucheki afya yangu,”
Mwanahalisi