Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,576
- 729,449
Mao tse tung rais aliyeitoa China kwenye umaskini na ufukara wa hali ya juu ambaye hata hapa kwetu ni maarufu sana alipata mazishi ya aina yake.
Maiti yake ikiwekwa kwenye jeneza la mawe ya quartz(mawe kioo) ambayo yanapatikana hapa nchini....quartz inaaminika ni mawemadini yenye nguvu ya ajabu hasa kwenye kumpa mtu umaarufu heshima madaraka utajiri na nguvu za kisiasa na kijeshi.
Lakini vile vile ukiwekwa kwenye jeneza la quartz stones mwili wako hauozi milele, mwili wa Mao mpaka leo uko kwenye jeneza la mawemadini ya quartz pale Beijing kwenye makumbusho ya Taifa na inasemekana mawe kioo yale yalipatikana Taiwan na kusafirishwa mpaka Beijing na gharama yake kwa wakati huo inasemekana ilikuwa usd million 2...!
Pale Kilindi Songwe Morogoro na ukanda wote huo mpaka Arusha Tanga na kwingineko tuna haya mawe ya quartz yanang'aa kama kioo na watu wa Asia hasa wachina wanayatafuta mno.
Wengi wetu hatujui thamani yake lakini kwa wenzetu hao hilo jiwe ni kitu cha thamani mno! Ikitokea ukawa nayo jihesabie utajiri