Kaburi la maiti iliyoibwa hospitalini kufukuliwa . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaburi la maiti iliyoibwa hospitalini kufukuliwa .

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ndiyomkuusana, Sep 24, 2012.

 1. ndiyomkuusana

  ndiyomkuusana JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Maiti itasafirishwa kutoka Tanga hadi Mwananyamala Dar
  *Mahakama kutoa kibali maalum, Jeshi la Polisi kusimamia
  HATIMAYE mwili wa marehemu Ntimaruki Khenzidyo (23) uliodaiwa kuibwa katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam na kusafirishwa kwenda Handeni, Tanga kwa mazishi, imeamriwa ufukuliwe na kurudishwa Dar es Salaam.

  Uamuzi wa kufukuliwa mwili huo, ulifikiwa Dar es Salaama jana baada ya kikao kilichofanyika katika Kituo cha Polisi Oysterbay ofisini kwa Mkuu wa Upelelezi, Moses Fundi ambaye ndiye aliyeongoza kikao hicho.

  Kikao hicho kilijumuisha askari polisi, ndugu wa marehemu Khenzidyo, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwanyamala, Sofinius Ngonyani na watu waliodaiwa kuutorosha mwili wa marehemu Khenzidyo na kuusafirisha kwenda Tanga ulikozikwa.

  Kikao hicho kilichokuwa na mvutano mkali, kilichukua zaidi ya masaa manne na kilianza saa tano asubuhi na kumalizika saa nane mchana.

  Wakati wa mjadala, hatimaye ilibainika kuwa, mwili wa marehemu Khenzidyo, ulisafirishwa kimakosa na familia nyingine, ambayo ilikosea kuchukua mwili wa marehemu ndugu yao, Ramadhan Mhina, uliokuwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mwananyamala.

  Kabla ya mvutano huo, awali ndugu wa marehemu Khenzidyo, walimtaka Mganga Mkuu Hospitali ya Mwananyamala, Sofinius Ngonyani, aeleze uamuzi uliofikiwa na utawala wa hospitali hiyo, juu ya tukio hilo ambalo waliliita ni la uzembe.

  Akijieleza katika kikao hicho, Ngonyani alisema, kutokana na ufinyu wa bajeti ya hospitali yake, suala la kugharamia usafiri wa mwili wa marehemu Khenzidyo kuutoa Tanga hadi Dar es Salaam, halitawezekana kwa kuwa hospitali hiyo haina fedha.

  Pia alisema, hospitali hiyo haina uwezo wa kuusafirisha mwili wa marehemu Mhina na kuupeleka Tanga, kwa kuwa hakuna fedha za kufanya hivyo.

  “Ni kweli tukio hili limetokea katika hospitali yangu, lakini kama mnavyojua, hospitali haipo Serikali Kuu, hii ipo chini ya Halmashauri. Kwa mazingira haya, hakuna fungu lolote lililotengwa kwa ajili ya dharura.

  “Binafsi sina uamuzi wowote juu ya jambo hili, lazima nipate kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na itachukua muda kuonana naye, ili kuafikiana na ombi la kutoa gari au fedha kwa ajili ya kusafirisha maiti zote mbili,” alisema Ngonyani.

  Ngonyani alipotoa kauli hiyo, Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Oysrebay (Fundi) na ndugu wa Marehemu Khenzidyo, walihamaki na kumshambulia Mganga Mkuu huyo wa Hospitali ya Mwananyamala na kusema kuwa, anafanya mzaha na suala lisilohitaji kuchezewa.

  Katika mazungumzo ya watu hao, walimtaka Ngonyani afanye kila atakaloweza, ili fedha zipatikane za kurudisha mwili kutoka Tanga kuja Dar es Salaam na kutoka Dar es Salaam kwenda Tanga.

  Wakati mvutano huo ukiendelea, hatimaye pande hizo mbili zilipendekeza kwenda kupiga kambi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni leo asubuhi, ili kushinikiza miili hiyo miwili isafirishwe kwa gharama za manispaa hiyo.

  Wakati wa mjadala huo, upande wa marehemu Mhina ulikuwa ukiongozwa na Husein Sempombe, ambaye alisema wao watagharamia kusafirisha miili yote miwili na kuifikisha inakotakiwa kufikishwa.

  “Kwa kuwa kuna makosa yamefanyika, yaani badala ya kuusafirisha mwili wa ndugu yetu Mhina ili tuupeleke Tanga, sisi tukachukua mwili wa Khenzidyo na kuupeleka Tanga, basi tutagharamia gharama zote za kuutoa mwili huo Tanga na kuuleta hapa Dar es Salaam.

  “Nayasema haya kwa sababu utawala wa Mwananyamala umekataa kutoa msaada, sasa naomba tufupishe kikao, sisi tutawajibika kuurudisha mwili wa Khenzidyo pale tulipouchukua.

  “Pamoja na hayo, tunaomba tupewe maiti yetu leo (jana) ili tuanze safari pia tunaomba ndugu wa marehemu Khenzidyo twende nao Tanga, ili tukawakabidhi maiti yao,” alisema Sempombe.

  Licha ya ndugu wa marehemu Mhina kujitolea kutoa gharama, bado ilizuka hofu kwa upande wa ndugu wa marehemu Khenzidyo na kudai watatelekezwa baada ya kufika huko Handeni mkoani Tanga, kitendo ambacho Fundi alilazimika kukitoMAAMUZI
  Akitoa ufafanuzi juu ya tukio hilo, Fundi atasimamia ili kipatikane kibali cha mahakama cha kufukua kaburi la marehemu Khenzidyo, ambaye ameshazikwa Tanga. Pamoja na hatua hiyo, alisema atasimamia zipatikane tiketi tatu za basi za ndugu wa marehemu, watakaokwenda kufuata mwili wa marehemu huko Tanga.

  Pia aliahidi kuwasiliana na Jeshi la Polisi, Mkoa wa Tanga kikiwamo kituo cha Polisi, Wilaya ya Handeni ili waweze kusimamia usalama wakati kaburi la Marehemu Khenzidyo likifukuliwa.

  Kwa upande wa Hospitali ya Mwananyamala, ilipewa jukumu la kutoa dawa kwa ajili ya maiti pamoja na mtumishi mmoja wa chumba cha kuhifadhia maiti atakayesimamia shughuli ya kuziwekea dawa maiti kama zitakuwa zimeharibika.

  Kwa upande wa ndugu wa marehemu Mhina, watawajibika kusafirisha mwili wao hadi Tanga na kuzika pia kushiriki katika kufukua maiti ya Khenzidyo na kuirudisha kwa gharama yao hadi Hospitali ya Mwananyamala walikoitoa.

  Vile vile upande huo wa marehemu Mhina, utawajibika kukodi jeneza litakalokuwa na mwili wa marehemu Khenzidyo wakati wa kuurudisha Dar es Salaam, ambalo ndilo litakalokuwa limesafirisha mwili wa Mhina kutoka Dar es Salaam kwenda Tanga.

  Hata hivyo ndugu zake Khenzidyo walipinga kitendo cha maiti yao kuwekwa katika jeneza litakalohusika kusafirisha maiti ya Mhina, lakini Fundi aliingilia kati na kusema uamuzi huo hauna tatizo kwa kuwa utapunguza gharama.

  Baada ya mjadala, hatimaye baba mzazi wa marehemu Khenzidyo, Marko Khenzidyo, alikubali mwili wa mtoto wake uwekwe katika jeneza litakalokuwa limesafirisha mwili wa marehemu Mhina kutoka Dar es Salaam kwenda Handeni Tanga.

  Mjadala huo ulipokaribia mwisho, Fundi aliwataka walioteuliwa kufuata maiti Tanga, kufika kituoni Oysterbay leo saa mbili asubihi, ili waende mahakamani kwa ajili ya kushughulikia kibali cha kufukua kaburi la Marehemu Khenzidyo.

  Septemba 21, mwaka huu, Hospitali ya Mwananyamala ilikumbwa na kashfa ya kupoteza mwili wa marehemu Khenzidyo, aliyekuwa amehifadhiwa hospitalini hapo baada ya kufariki dunia kwa ajali ya gari, Septemba 17 mwaka huu.

  Marehemu Khenzidyo alikuwa Mfanyakazi wa Kampuni ya Ulinzi ya Group 7 na alifariki baada ya kugongwa na gari katika Barabara ya Kawe, Dar es Salaam.

  Hata hivyo, wakati ndugu zake walipofika na jeneza hospitalini hapo kwa ajili ya kuuchukua mwili wa ndugu yao huyo, mwili huo haukuwapo, jambo lililozusha hofu hadi polisi walipoingilia katilea ufafanuzi.
   
 2. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Huu ni uzembe uliovuka kiwango!

  Hivi ina maana maiti ilitolewa Dar mpaka Tanga bila ndugu yeyote kuhakiki?Au ndio yale mambo ukishakufa,wengine wanaogopa kukuangalia?
  Hofu yangu ni hali ya hiyo maiti iliyoamriwa kufukuliwa itakuwa katika hali mbaya!!!
   
 3. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Jamani kweli duniani kuna mambo mengi sana ya kusikitisha na kukatisha tamaa kabisa.Hivi inaingia akilini wanasafirisha maiti ya mtu ambae sio ndugu yao wakamfanyia sara mpaka wakamzika bila kumkagua.Kwa upande wangu sasa its high time for Islamic to allow waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho kama wakristo wanavofanya.Hii ya mazishi kwa waislam kuwa ni siri iishe otherwise watakuja kuzika upepo kuwaridhisha waombolezaji so long as wale key participants wakubali kutunza siri.

  Mbali na hilo kama Ntimaruki Khenzidyo (23) atakuwa mkristo na Ramadhan Mhina ni muuislam maanayake ni kwamba tayari atakuwa ameshazikwa kwa taratibu za kiislam ambazo waislam wenyewe wanazijua. So the whole saga is really confusing.Lakini wa kulaumiwa ni ndugu wa marehemu Ramadhan Mhina waliokwenda Mwananyamala hospitali.Kweli nduguzanguni hata kama kwenye msiba unachanganyikiwa utashindwa kweli kutambua maiti inayokuhusu, unless huyo mtu awe amepata ajali mbaya sana au ameungua na moto lakini kama sio hivo kweli kuna uzembe mkubwa uliotokea kwanza kwa wahudumu wa Mwananyamala mortuary na then wanandugu wa Ramadhan Mhina. Anyway ya Mungu ni mengi tumwachie yeye maana ndo alietuumba na ndie anaejua mwisho wetu utakueje hapa dunia
   
 4. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hesabu janga la kitaifa
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Naona umewajumuisha wahudumu wa motuary katika lawama kuwa nao ni wazembe, mimi sikuungi mkono, harafu ati wanataka hospitali igharamie gharama za kusafirisha maiti!, silly !
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Mi nafikiri ndugu wa mhina nao ni wehu walipofika kuaga awakuona sio wao mpaka waweke kaburini mwili wa mtu mwingine kweli ...inaingia akilini kweli??
   
 7. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kwani Waislamu si huwa wanamkamua marehemu tumbo ili asizikwe na uchafu?,inamaana huyu marehemu hawakumkamua?,maana najiuliza ni vipi wasione hata sura yake nakosa majibu.
   
Loading...