Kaburi la kiyeyeu lililopo Iringa ni kweli linamaajabu yanayozungumzwa ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaburi la kiyeyeu lililopo Iringa ni kweli linamaajabu yanayozungumzwa ?

Discussion in 'Jamii Photos' started by kituro, Dec 26, 2010.

 1. k

  kituro Senior Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [​IMG]
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mwenye data atujuze zaidi jmni maana huwa nasikia tu hizi story!


   
 3. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145  Maria Roza.............
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Sema paka karibu thamakiiiii:hungry:
   
 5. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Nasikia Ukiyadiscuss sana haya makaburi, cha mtemakuni utakiona.
   
 6. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #6
  Dec 26, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kaka wafate wazee wa Kinyalu,usitutafutie matatizo.
   
 7. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #7
  Dec 26, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ecclesiastes 9
  5
  For the living know that they shall die: but the dead know not any thing, neither have they any more a reward; for the memory of them is forgotten.
   
 8. k

  kituro Senior Member

  #8
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  makaburi yapo iringa je wewe upo wapi mpaka unayaogopa? na hicho unacho kiogopa ndicho tukitakacho
   
 9. anjnr

  anjnr JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 483
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tanesco walipopitisha line ya umeme juu ya lile kaburi haukupita mpaka walipohamishia nguzo upande wa pili wa barabara
   
 10. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kiyeyeu ndo nani huyo?
   
 11. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,898
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145


  Nafuu, wacha nije nile samaki mie naona hapa watu wanaanza kuogopa makaburi.
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  KABURI la Marehemu, Martine Kiyeyeu linalokadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 50 limeendelea kuwa mtihani mgumu kwa Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads), mkoani Iringa baada ya kuendelea kusuasua kuling'oa ili kuruhusu ujenzi wa barabara kuu ya Tanzania-Zambia.

  Familia ya Marehemu huyo imeshajaribu kuling'oa kaburi hilo bila ya mafanikio na kwamba sasa mtihani huo umeutupa kwa Tanroads mkoani humo.

  Kaburi hilo linalodaiwa kuwa na maajabu lipo kandokando ya barabara kuu ya Tanzania-Zambia, katika kitongoji cha Isimila, Kijiji cha Ugwachanya, wilayani Iringa.

  Habari za uhakika zinasema kuwa, Tanroads nayo ilijaribu kuliondoa Novemba, lakini ilishindikana na baadaye ikasema kuwa italiondoa Disemba mwaka huu, ambapo hadi sasa halijaondolewa.

  Habari kutoka ndani ya Tanroad mkoani humo, zinasema kwamba kila kitu katika maandalizi ya kuliondoa kaburi hilo kimekamilika ikiwa ni pamoja na fedha, lakini kilichokosekana ni jasiri wa kufanya kazi hiyo, baada ya kuwapo kwa imani kwamba wote waliojaribu kuliondoa walifariki dunia.

  Jambo hilo linaonyesha kuwa kuna mpango wa kurushiana mpira kati ya wanakijiji na maofisa wa Tanroads kuhusu nani atasimamia kuondolewa kwa kaburi hilo.

  Wakizungumza na Mwananchi Jumapili, baadhi ya ndugu wa Kiyeyeu walisema tangu Tanroads ianze mchakato wa kuliondoa kaburi hilo kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara, ni zaidi ya miezi miwili na hawajajua lini hasa litaondolewa.

  Mkwe wa Kiyeyeu, Yoseph Msakwa (70) alisema wamekubali kwa shingo upande kuliondoa kaburi la ndugu yao, kutokana na ukweli kwamba, serikali ndiyo yenye mamlaka.

  "Tanroads walisema watakuja Novemba, baadaye wakasema Desemba mwaka huu, lakini ndio hiyo inaisha, sijui watakuja lini kuliondoa, tumekubali kwa sababu wanasema hiyo ni serikali, ingekua amri yetu tusingependa kuliondoa," alisema Msakwa.

  Msakwa aliongeza, "Wakati wanajenga barabara hii kwa mara ya kwanza, walikuja na tingatinga lao, ili kubomoa kaburi la Kiyeyeu lakini walishindwa na kuamua kuondoka. Mkandarasi wa barabara ambaye alikuwa mzungu alipoambiwa juu ya kushindikana kwa kazi hiyo, alikana na kuamua kuja mwenyewe, lakini naye akashindwa ndio maana waliamua kupindisha barabar."

  Miongoni mwa maajabu ya kaburi la Kiyeyeu, ni jinsi nguzo za Umeme ambazo zimehama toka upande mmoja na kwenda wa upande wa pili ili kupisha eneo la makaburi, na baadaye kurejea tena kwenye njia yake.

  Barabara kuu ya Tanzam nayo katika eneo hilo imepindishwa kupisha kaburi hilo, ambalo pia lipo na makaburi mengine 19, yote yakiwa ya familia moja.

  Msakwa alisema mara kadhaa walishajaribu kuhamisha kaburi hilo, lakini haikuwezekana:"Tulishachimba kaburi lingine ili kuhamisha mabaki ya maiti amayo yapo mita chache kutoka barabarani lakini haikuwezekana, kwani matingatinga yote yaliyokuja yalishindwa kufanya kazi na madereva wake kupata madhara," anasema Msakwa.

  Mjukuu wa Kiyeyeu, Anatalia Msakwa alisema mbali na wajenzi hao wa barabara kutaka kuliondoa, ilishatokea ajali kubwa ambapo gari la mafuta liliangukia kaburi hilo na kusababisha dereva wake kufa.

  "Siku moja wakati nikiwa karibu, nilishuhudia ajali iliyotokea hapa, ilisababisha maafa makubwa, lakini kaburi la babu halikudhurika zaidi ya kukatika kipade kidogo cha msalaba ambacho kilitengenezwa," anasema na kuongeza:

  "Mila za kabila la kihehe zinaheshimu sana makaburi ndio maana ukija Iringa kila kaburi limejengewa na kupakwa chokaa. Hatupendi kuwanyanyasa waliozikwa ndio maana tumekubali kwa shingo upande kuhamisha makaburi haya."

  Akizungumzia kaburi hilo, Fundi Mkuu wa Mradi wa Umeme miaka hiyo, ambaye alijenga kutoka Tagamenda hadi Ifunda kupitia kwenye eneo la makaburi, Said Abdalah Said alisema walichimba mashimo na kuweka alama kwa ajili ya kuweka nguzo, lakini vioja vya kaburi hilo viliwafanya wahamishe haraka laini ya umeme.

  Alisema wazee wa eneo hilo waliwafuata na kuwaeleza; ‘hapa paacheni kama mlivyopakuta, mnaona hii barabara ilivyopinda, mnafikiri kwa nini hawakuondoa hili kaburi.

  Kauli za wazee, vituko na ajali zilizokuwa zikitokea eneo hilo, ziliwafanya mafundi hao waogope kupitisha nyaya z umeme kwenye eneo hilo.

  "Sio kama historia, dereva wa tingatinga la kwanza lililotaka kuondoa kaburi alikufa, akaja wa pili akang'atwa na nyuki na kufa pale pale, nasi tukaogopa ndio maana umeme haujakatisha juu ya makaburi hayo," anasema Said.

  Meneja wa Tanroads Iringa, Paul Lyakurwa alisema kuwa wanatarajia kuhamisha makaburi hayo kwa ajili ya mradi mkubwa wa barabara, ambayo ni muendelezo wa barabara ya Tanzam toka Iyovi mpaka Mafinga.

  "Huu ni muendelezo wa barabara ya Tanzam, mara ya kwanza tuliishia Iringa mjini kutokana na ufinyu wa bajeti, Serikali ya Denmark imekubali kutoa fedha ndio maana tunafanya usanifu, ili barabara ianze kujengwa," alisema Lyakurwa.

  Alisema wamefanya usanifu na moja kati ya maeneo ambayo yanahitaji kuandaliwa ni eneo la Isimila ambako kuna makaburi 20, likiwemo lile la Kiyeyeu na kwamba ujenzi wa barabara hiyo utagharimu zaidi ya Shl68.5 bilioni.

  Alisema kuwa familia hiyo imetaka kulipwa kiasi cha Sh3 milioni kwa ajili ya kuhamisha makaburi yote 20, zoezi ambalo linatarajiwa kufanywa mwezi huu.

  Mwenyekiti wa Kijiji cha Ugwachanya, Nicholous Kindole alisema katika mkutano kati ya Tanroads na wanakijiji, kati ya wananchi 30 waliojitokeza, wananchi wanne tu ndio walikubali kushiriki katika kuhamisha kaburi hilo, huku waliobaki wakihofia maisha yao.

  "Wanakijiji hawataki kushiriki kwa sababu tumeambiwa kuwa lazima watu ndio wabomoe na sio gari, wananchi wamegoma ila tutawatumia wale wa vijiji vya karibu vya Wenda na Njiapanda kwani tunachotaka ni maendeleo," alisema Kindole.

  Hata hivyo, inadaiwa kuwa Kiyeyeu alikuwa mkulima mkubwa ambaye hakuwahi kuwa na cheo chochote cha kichifu au kimila kama ambavyo wengi wanadhani.

  Bado kila mmoja ana shauku kubwa ya kushuhudia kaburi hilo likiondolewa japo siku maalum ya zoezi hilo haijawekwa hadharani.
   
 13. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  je, uliwahi kusikia maajabu ya Kaburi hili la mtu maarufu katika fani ya waganga wa jadi Almaarufu Kiyeyeu? Eti Kakobe naye alitaka kujifananisha na mtu huyu kipindi Shirika la Umeme Tanesco likiwa katika harakati za kupitisha nguzo kubwa za umeme mbele ya Kanisa lake, ambapo aliibuka na kusema kuwa hata nguzo hizo zikipita mbele ya Kanisa hilo basi umeme hautawaka kamwe kwa miujiza na nguvu zake, kumbe haya yanawenyewe hebu pata kisa cha Kaburi hili japo kwa ufupi.....
  Kaburi la Kiyeyeu, lipo Njiapanda ya Mlolo pembezoni kabisa mwa barabara iendayo Mkoani Mbeya ukitokea Iringa lipo upande wako wa kulia, katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
  Hili ni kaburi alilozikwa mtu mmoja aliyekuwa Mganga maarufu wa jadi katika ukanda mzima wa maeneo ya mkoa huo, ambaye alifariki dunia miaka ya nyuma kidogo lakini hadi leo hii kaburi hilo ukiliona ni kama limejengwa jana.
  Baada ya kufariki dunia mganga huyu, alizikwa kwa kufuata taratibu na mira za Machifu ambapo alizikwa kwa kusindikizwa na mtu aliye hai, aliyejitolea kwa ajili ya kuzikwa naye akiwa hai ili kumsindikiza, ambapo inadaiwa mtu huyo aliketi na kumpakata mganga huyo aliyezikwa huku akiwa amekaa.
  Kaburi hilo limekuwa liwashangaza watu waliowengi na hata ndugu wa marehemu huyo kutokana na kuwa na maajabu na miujiza isiyoisha kana kwamba mtu huyo amezikwa mahala hapo jana.
  Moja kati ya maajabu makubwa yaliyowahi kutokea mahala lilipo kaburi hilo ni wakati Shirika la umeme lilipokuwa katika zoezi la kuweka Nguzo za umeme pembezoni mwa barabara hiyo na kutokana na kaburi hilo kuwa karibu kabisa na barabara kubwa, Imedaiwa kuwa Tanesco walifanya mazungumzo na ndugu wa marehemu huyo ili wakubali kusogeza ama kuhamisha kaburi hilo ili kupisha zoezi la kuweka nguzo za umeme ili kupitisha umeme mahala hapo.
  Imeelezwa baadhi ya ndugu hao walikubali baada ya mazungumzo hayo na kuwaruhusu Tanesco kuhamisha kaburi hilo, lakini zoezi la kuhamisha lilishindikana na walipojaribu kulibomoa hata nyundo haikuweza kufua dafu kubomoa hata sehemu ya tofali lililojenga kaburi hilo.
  Ndipo ilipoamuliwa kuweka nguzo hizo na kupitisha nyaya za umeme kiubishi.
  Lakini baada ya kumaliza zoezi hilo walishangazwa kwa kuona kuwa eneo la juu ya kaburi hilo hapakuwa ukipita umeme hali ya kuwa ulipoanzia hadi kabla na baada ya kaburi hilo umeme umejaa tele, ila eneo la juu ya kaburi hilo tu hakuna umeme.
  Jambo hilo liliwafanya Tanesco kukubali matokeo na kuamua kuchukua uamuzi wa busara kwa kuhamishia baadhi ya nguzo hizo upande wa pili wa barabara ili kukwepa eneo hilo, hivyo nyaya hizo zikavuka barabara kabla ya kufikia kaburi hilo na baada ya kulivuka kaburi hili, na baada ya kufanya hivyo ummeme huo uliwaka na hadi hii leo unaendelea kuwaka, hivyo Serikali japo haiamini uchawi lakini hapa iliamini uchawi upo. Angalia picha hiyo katika alama nyekundu ndizo nyaya zilizovushwa kutoka upande wa pili kukwepa kaburi hilo.
   
 14. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Thamakiiiii ganiiiii huyo jamaniiiii......


  [​IMG]
   
 15. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Makubwa haya ila njoo na kwetu GAMBOSHI mkuu ushuhudie..............
   
 16. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #16
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani mi naogopa mwenzenu??????????? :shock::shock::A S 109::A S 109:
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Na wakilazimisha watakiona kila kiongozi akipita hapo lazima ale mzinga wa nguvu
   
 18. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #18
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Kwa John Pombe Magufuli hilo kaburi halitafua dafu ataliondoa nyie subirini!:whoo:
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Sijui kwa nini aliitwa MARTIN na si vinginevyo.....jina hilo na haya mabo tafauti kabisa
   
Loading...