Kaburi la cuf | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaburi la cuf

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mwaipaja, Nov 17, 2010.

 1. m

  mwaipaja Member

  #1
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha Cuf kimekufa,kimezikwa,kaburi lake lipo zanzibar,yatima wamebaki bara wakifarijiwa na chama chama cha majambazi.Hiki ndicho kinachooneka dhahiri baada ya uchaguzi na kinachoendelea bungeni.
  Kwa cuf kuwa sehemu ya utawala zanzibar ni sawa na kujichimbia kaburi,hawapo tena katika orodha ya vyama vya upinzani.Viongozi wake waandamizi wamepewa vya juu serikalini kama ilivyotokea kwa sharif hamad na akina Juma Haji Duni,tutegemee yafuatayo ambayo yameshaanza kujitokeza waziwazi:
  1.Kwa cuf Kuikosoa ccm ni sawa na kujikosoa yenyewe kwa kuwa makamu wa rais wa zanzibar-sharif hamad anatoka cuf ambapo kwa nafasi yake kama makamu wa rais anatekeleza na kusimamia yote ambayo yanafanywa na serikali,kwa hiyo jaribio lolote la kuikosoa serikali haliwezi kufanywa na ccm wala cuf
  2.Mchango wa wabunge wa cuf bungeni utatolewa katika maudhui ya kuibeba ccm kwa kuwa tayari cuf na ccm wameshafunga ndoa
  3.Cuf hawatakubali wajiunge na kambi ya upinzani bungeni kwa kuwa wao si wapinzani,na hii ndiyo sababu iliyofanya cuf wajiunge na vyama vingine kuunda kambi ya upinzani isiyo rasmi ili kukwepa kuungana na wapinzani wa kweli na rasmi bungeni
  4.Cuf wataendelea kuwaandama wapinzani kwa kulinda maslahi yao na chama cha majambazi.Kwa mtindo huu,cuf wamejiua,wamezikwa
  Nawasilisha
   
 2. emmathy

  emmathy Senior Member

  #2
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Afdhali wewe umeliona mapema.....Mungu atuepushe ili safari ya mabadiliko isiishie njiani.
   
 3. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Niwazi kabisa upinzani kupitia CUF ndio basi tena! wale akina political analysit bado hili hawajaliona kabisa. CUF ambao ndio sisiem B wameungana na akina TLP, NCCR,UDP...tuwaitaje hawa nao? ni watoto wa kambo wa sisiem au? nivipi akina Rev kishoka wana lilia muungano na CDM? jamani akina mchungaji kishoka na akina political analist(PASCO) hamuoni haya hata mimi wa ifwenga kijijini ninaliona nyie vipi hapo mjini?
   
 4. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama CUF ni wafu.
  CUF wako hai tena wamenawili sana, ila tuwameolewa kwa ndoa ya mkeka,Dude ni CCM.
  Siku ya kupewa taraka pia watapewa hapo hapo mkekani.
  Hiii hiii! Nambari ONE Oyee! :first:
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Nov 17, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,068
  Trophy Points: 280
  ..CUF wamefaulu mitihani migumu sana.

  ..wanaweza kukosa umaarufu huku Tanganyika, lakini siyo Pemba.

  ..kumbukeni kwamba wamezoa viti vyote vya uwakilishi Pemba.
   
 6. kiraia

  kiraia JF Gold Member

  #6
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 1,614
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Hivi Ukubwa wa pemba unalingana na wilaya ya Kinondoni?
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Nov 17, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,068
  Trophy Points: 280
  Kiraia,

  ..nakubaliana na wewe kwamba Pemba ni eneo dogo sana inawezekana sawa na wilaya ya Kinondoni.

  ..lakini pamoja na udogo wa eneo la Pemba, hawa wenzetu wana msimamo usioterereka linapokuja suala la kuipinga CCM kule Zanzibar.

  ..binafsi inanisikitisha kwamba for some reasons wameshindwa kuleta ushawishi wa kisiasa huku Tanganyika kama walivyofanikiwa Pemba.

  ..ukifuatilia siasa za Zenj, unaweza kuona kwamba bado climate ya kisiasa ni ileile tangu enzi za ASP vs HIZBU. ndiyo maana nikasema si rahisi kwa kufa kufa kwasababu inawezekana hawa wakawa ni HIZBU.
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Nov 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huwa najiuliza hivi kampeni zikianza CUF au Seif atakuwa anasema tuchagueni sisi ili tuendelee kuwa madarakani au.
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakuna Kitu ila ni historia ndio inaifanya CUF iwe hivyo pemba ila huku bara wamebaki majungu sasa
   
Loading...