Kaburi la albino lafukuliwa kutwaa mifupa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaburi la albino lafukuliwa kutwaa mifupa

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jul 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Hofu ya kusakwa kwa viungo vya walemavu wa ngozi imeibuka upya baada ya watu wasiojulikana kudaiwa kufukua kaburi la mlemavu wa ngozi katika kitongoji cha Izengwabasumba katika kijiji cha Nyamalulu wilayani Geita na kutoweka na baadhi ya mifupa.
  Tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na imani za kishirikina za kusaka utajiri unaotokana na dhahabu. inadaiwa kuwa jeshi la polisi halijakamata mtuhumiwa yeyote lakini linaendelea na uchunguzi na tayari orodha ya watu kadhaa wakiwemo mganga wa jadi yanafanyiwa kazi kwa siri katika hatua za awali.
  Tukio hilo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia Julai mosi na kisha kuripotiwa makao makuu ya polisi wilaya.
  Inadaiwa kuwa wakazi wa kitongoji hicho waligundua kaburi hilo la Zawadi Mangidu (22), majira ya saa kumi na nusu jioni likiwa limefukuliwa huku kipande cha mfupa mmoja kikiwa kimedondoshwa juu ya kaburi.
  Habari kutoka eneo la tukio zimedai kuwa watuhumiwa walifukua kaburi hilo pembeni mwa eneo liliojengewa kwa saruji..kwa kuchimba eneo lisilo na saruji nabaada ya kufukua na kutoa mifupa walifukia tena na kutoweka.
  Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Julai mosi na kuwa tayari timu ya jeshi la polisi ikiongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita walifika eneo la tukio.
  Alisema kuwa polisi walikwenda eneo la tukio baada ya kupata taarifa kupitia mwenyekiti wa kitongoji hicho na kuanza kufanya uchunguzi ambapo imebainika kuwa baada ya kufukua kaburi baadaye walilifukia.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  Jamani hili Tatizo la hawa ndugu zetu Maalbino Serikali ya Mzee J.Kikwete halishughulikii ipasavyo?Mbona bado halijamalizika?
   
Loading...