Kaburi katikati ya jiji, je, ni la nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaburi katikati ya jiji, je, ni la nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kashaija, Nov 18, 2008.

 1. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuna bustani moja katikati ya jiji la Dar es salaam (katikati ya barabara ya Samora, India na Mosque) maeneo ya clock tower. Ukifika katika bustani hiyo, kitu cha kwanza utakachokiona pale ni kaburi lililojengewa na marumaru nyeupe na ambalo kwa mujibu wa watu waliozoea kukaa pale mara kwa mara ni kwamba kuna mtu maalumu ambaye hulifanyia usafi kila siku kwa kuliosha na kusafisha mazingira yaliyozunguka kaburi hilo (siyo bustani yote!) na hulipwa mshahara wake kwa kazi hiyo (sijui hulipwa na nani). Vile vile nimesikia kwamba baadhi ya watu huenda kuabudu pale nyakati za usiku.

  Swali, je kaburi hili ni la nani ambaye ni muhimu sana kiasi hicho katika historia ya nchi yetu hadi akazikwa katikati ya jiji? Je, kaburi hili likihamishwa pale kama mengine yavyohamishwaga kutakuwa na athari gani?

  Nilidhani mtu wa muhimu sana katika historia ya nchi yetu ni Marehemu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere ambaye kama angelizikwa pale au sehemu inayofanana na hiyo ingetoa mwanya hata vizazi vyetu vijavyo kuona na kushuhudia alipolazwa mhasisi wa Taifa letu, vile vile kwa vitendo vya hawa MAFISADI tungeweza kuamua wana JF tukaenda kuwaombea dua baya.
   
 2. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  its true hilo kaburi lilikuwepo pale...m not sure if bado lipo cz i am nt in bongo,na kuna kipindi flani cha nyuma lilianza kubomolewa ikatokea ugomvi mkubwa kweli na mwishowe ndo likaachwa na kuwekewa hizo maru maru...
  any one with clear maelezo please??????
   
 3. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mtaalam, hili kaburi bado lipo, hata leo asubuhi nilipita hapo nimeliona limeoshwa limetakata kweli. Si unajua tena marumaru?

  Kwa wanaojua, tafadhali tupe habari zaidi. Ni la mtu gani?
   
 4. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2008
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Angeulizwa mtoto wa mjini DITO, labda sykes atueleze.
   
 5. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2015
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Mkuu utotoni tumecheza sana pale kwenye Bustani hadi pale ilipovamiwa na wale watoto watundu kipindi kile walikuwa wanaitwa Changudoa na sio kama sasa hivi Changudoa ni muuza Uchi... Bustani ilivamiwa na hao watoto kisha wakaja Omba omba haswa na familia zao wagogo na sisi tukakosa kabisa sehemu za kuchezea michezo ya kitoto kama Bembea kuteleza n.k kwa akili yangu sikufahamu kama kuna kitu kama hicho kaburi maana siku si nyingi kuna mtu alikuwa anamuelekeza mtu Dukani kwake na huyo mtu akawa hamuelewi akaniuliza Kaburi moja ni wapi nami nikaduwaa wakati mimi ni Master wa City Centre Mitaa na Vichochoro nilikuja kumuelewa aliposema bustani na pia lipo kaburi pale Nikaduwaa na nilipoenda kweli nikalikuta... eno hilo kitambo kulikuwa na Bembea ya chain kubwa... ni Madereva taxi wamaduwaa tu...

  Kama ni kaburi la kitambo basi sikulifahamu utotoni na kama lilikuja baadae sikufahamu hii kitu... Nchokumbuka pale kulikuwa na mitambo maalum ya kilipia parking pembezoni unalipa mwenyewe kwa lisaa ilikuwa ni 1 shillings ukitumbukiza dala chenge inatoka...
   
 6. Mkazuzu

  Mkazuzu JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2015
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 208
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  hilo no kaburi la shekhe mkuu wa msikiti wa kwanza kabisa wa mzizima ambao hapo awali ulikuwa maeneo ya magogoni karibu na ikulu,ukaja kuhamishiwa maeneo hayo ya clock tower nadhani bado upo had Ieo,ni msikiti wa miaka ya 1800,zama za usultani
   
 7. C

  COPPER JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2015
  Joined: Dec 28, 2012
  Messages: 1,667
  Likes Received: 344
  Trophy Points: 180

  Hata pale Utumisbi kuna makaburi ya zamani nadhami.ni ya waarab wa miaka hiyo
   
 8. k

  keki tamu Member

  #8
  May 1, 2015
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 19
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  weka picha tuone
   
 9. SOGHOO

  SOGHOO JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2015
  Joined: Mar 25, 2015
  Messages: 1,274
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 0
  CCM ikishinda uchaguzi mwaka huu kile kiwanja kitauzwa kwa wawekezaji feki a,k.a mafisadi na hili kaburi litahamishwa.

  MARK MY WORDS
   
 10. o

  oldonyosambu Senior Member

  #10
  May 1, 2015
  Joined: Apr 28, 2015
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Msikiti wa kwanza kujengwa ulikuwa mahala palipo kanisa la Kilutheri sasa hivi Hapo Luther House
   
 11. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2015
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mlaleo, haya maelezo yako ndio yanaweza kutoa mwanga zaidi. Hii sehemu nafikiri ilikuwa wazi tu lakini wakati wa 'chokochoko' za siasa za udini miaka ya mwanzo mwa tisini ndipo watu (from nowhere) wakaja na kuweka alama za kaburi. Baada ya wengine kubisha ndipo baadhi (pia from nowhere) wakadai kuwa alizikwa Ustaadhi fulani pale hivyo kutokana na mazingira ya wakati huo hoja ikapata nguvu na mpaka wakalijengea na hizo marumaru nyeupe.
  Labda tumuulize Mohamed Said mtaalamu wa histori tata za aina hii kama kweli anamjua aliyezikwa pale lakini kama naye hajui basi Archeologists itabidi waje wafanye kazi yao ili kuweka kumbukumbu sawa.

   
 12. ras jeff kapita

  ras jeff kapita JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2015
  Joined: Jan 4, 2015
  Messages: 5,672
  Likes Received: 3,728
  Trophy Points: 280
  Kwani ni nani alizikwa humo?
   
 13. zambez

  zambez JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2015
  Joined: Dec 28, 2013
  Messages: 2,048
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mzee kapita....
   
Loading...