Kaburi jingine la umati la Wahindi Wekundu lagunduliwa Canada, ni karibu na shule ya Wamishonari wa Ulaya

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,839
17,437
Kaburi jingine la umati la Wahindi Wekundu lagunduliwa Canada, ni karibu na shule ya Wamishonari wa Ulaya

Vyombo vya habari vimetangaza habari ya kugunduliwa kaburi jingine la umati lenye maiti za watoto zaidi ya 160 wa Wahindi Wekundi na wakazi asili wa Canada katika mkoa wa British Colombia.

Duru za habari zimeripoti kuwa, kaburi hilo la umati limegunduliwa karibu na shule ya zamani wa Wamishonari wa Kikatoliki katika mkoa wa British Colombia.

Habari ya kugunduliwa kaburi hilo lenye maiti za zaidi ya watoto 160 imetangazwa na watu wa kabila la wenyeji wa Canada la Penelakut.

Hadi sasa hakujatolewa habari zaidi kuhusu ugunduzi wa kaburi hilo. Habari kuhusu kashfa ya kutisha ya kugunduliwa makaburi ya maelfu ya wanafunzi wa shule za bweni zilizokuwa zikisimamiwa na Wamishonari wa Kikatoliki kutoka Ulaya huko Canada zimekuwa zikigonga vichwa vya habari katika vyombo vya kimataifa katika wiki za hivi karibuni. Habari hiyo imezusha malalamiko makubwa nchini Canada ambako kumeshuhudiwa vitendo vya kuchomwa moto makanisa katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.

Vilevile waandamanaji wenye hasira nchini Canada wameziangusha sanamu za wakoloni Malkia Victoria na Elizabeth wa II kwenye mji wa Winnipeg nchini huku hasira za umma zikiendelea kupanda baada ya kugunduliwa mabaki ya miili ya watoto wa wakazi asili wa nchi hiyo katika shule za bweni za makanisa.

Maelfu ya watoto wa Wahindi Wekundu waliuawa na kuzikwa katika makaburi ya umati

Tangu mwezi Mei mwaka huu hadi sasa, kumegunduliwa maeneo manne yenye makaburi ya miili ya watoto hao wa shule za bweni za huko British Colombia, Saskatchewan na Manitoba. Mabaki ya miili ya watoto wasiopungua 1148 imepatikana katika kaburi la umati na makaburi mengine kadhaa yasiyo na majina ya watoto waliozikwa ndani yake.

Ripoti ya Kamati ya Ukweli na Maridhiano ya mwaka 2015 imeonyesha kuwa, watoto wasiopungua 4,100 waliuliwa wakiwa katika shule za bweni za Wamishonari wa Kikatoliki au kutoweka.

Ripoti hiyo ilifichua unyanyasaji wa kutisha wa kimwili, ubakaji, utapiamlo na unyama mwingine uliowapata watoto wengi anokadiriwa kufikia 150,000 waliohudhuria shule hizo, ambazo zilikuwa zikiendeshwa na makanisa ya Kikristo kwa niaba ya serikali ya Ottawa.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amesema kuwa, ripoti iliyotolewa inatia uchungu lakini bado hajaomba radhi rasmi kwa niaba ya Kanisa Katoliki.
 
Wahindi wekundu wa Canada ambao ni wahangaso sad
4by154b45bf1981vq1j_800C450.jpg
View attachment 1852262
 
Nchi za Asia kama Japan ndo ziliwatia adabu wamishonari, sisi tuliwapokea na tukawapa kila kitu.
 
Hawa waindi wekundu kihistoria ndo wenye taifa hata la marekani naona saizi wapo sana Mexico
Mkuu kumbe bado wapo nilidhani kizazi chao kilifutika. Je kinachowafanya waitwe wahindi wekundu ni nini?
 
Kama Kanisa Catholic halikuhusika kwanini watoe $$$ in billions na kuomba samahani!?


'Where is their soul?': Inside the failed push to make Catholic Church pay for its residential school abuses


Church officials say they tried their best but could only raise fraction of $25M promised

Kanisa katoliki lilikia na visa gani na hao wahindi wekundu.

Kama waliweza kuwadahili kwenye shule zao kwa nn wafanye unyama huo?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom