Ijue historia ya kaburi la Sharif Abdushakur Salim Al Attas lililopo Samora, Posta Jijini Dar es Salaam

Kashaija

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
255
58
Kuna bustani moja katikati ya jiji la Dar es salaam (katikati ya barabara ya Samora, India na Mosque) maeneo ya clock tower. Ukifika katika bustani hiyo, kitu cha kwanza utakachokiona pale ni kaburi lililojengewa na marumaru nyeupe na ambalo kwa mujibu wa watu waliozoea kukaa pale mara kwa mara ni kwamba kuna mtu maalumu ambaye hulifanyia usafi kila siku kwa kuliosha na kusafisha mazingira yaliyozunguka kaburi hilo (siyo bustani yote!) na hulipwa mshahara wake kwa kazi hiyo (sijui hulipwa na nani). Vile vile nimesikia kwamba baadhi ya watu huenda kuabudu pale nyakati za usiku.

Je, kaburi hili ni la nani katika historia ya nchi yetu hadi akazikwa katikati ya jiji?​
Je, kaburi hili likihamishwa pale kama mengine yavyohamishwaga kutakuwa na athari gani?​

Nilidhani mtu wa muhimu sana katika historia ya nchi yetu ni Marehemu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere ambaye kama angelizikwa pale au sehemu inayofanana na hiyo ingetoa mwanya hata vizazi vyetu vijavyo kuona na kushuhudia alipolazwa mhasisi wa Taifa letu, vile vile kwa vitendo vya hawa MAFISADI tungeweza kuamua wana JF tukaenda kuwaombea dua baya.

1624860268771.png


************************
Maoni kutoka kwa wadau​

Hilo ni kaburi la Sharif na Imam mkuu wa msikiti mkubwa ulokuwepo hapo kabla ya kuingia wajerumani.
Msikiti huo ndio wa kwanza kabla ya kanisa la St Joseph pale Sokoine Drive.

Germans waliposhika hatamu za Tanganyika waliamua kujenga ofisi na nyumba zao barabara hii ya samora na sokoine.ndio mjii wa kisasa ulipoanza kujengwa.

Hivyo huu msikiti ulokuwapo hapo clock tower nao ukawa lazima uvunjwe katika master plan yao.

Wajerumani walipata upinzani mkuu kutoka jumuia ya waislam na wenyeji kuhusu kuvunjwa msikiti huo. Baadae Governor wa German Tanganyika walikubaliana kuuhamisha msikiti huo na kujengwa pale Kitumbini na kukubaliana kaburi la Sharif libaki hapo hapo kama ukumbusho kwa waloleta uislam Dar Es Salaam.

Hapa jambo moja ni kuwa hawa wajerumani walitawala Tanganyika lakini wakiheshimu mila na taratibu za wenyeji kama uchifu na Customary laws.

Pia waliheshimu tarehe za sherehe za kiislam na sheria za mahakama ya kadhi walozikuta.

Waingereza nao waliookuja waliheshemu pia waliheshimu hizi taratibu na hakuna mahali inapo onesha kuwa lilikua tatizo kuruhusu mahakama ya kadhi.

Kinachoshangaza sasa baada ya uhuru wafrika kujitawala na wakristo wafrica ambao hawakuwepo hapa dar es salam leo wamepiga marufuku Mahakama ya kadhi kwa chuki za kidini. Wale walowaletea ukristo hawakuona kuwa ni tatizo ila wao wamejenga chuki dhidi ya Waislam.

Anyway huu msikiti wa Kitumbini ulijengwa na Wajerumani kulipa ule ilokuwapo clock tower na tembelea huu msikiti uone archtect yake ilivo nzuri na kuta imara utadhani umejengwa juzi.

Chuki za kidini zimeletwa na wakuja waloingia Dar juzi kwa azimio la Arusha
************
Yapata meta 300 hivi Kusini mwa mnara wa saa jijini Dar es Salaam ipo bustani ya muda sana kama miaka 220 iliyopita upande wa Magharibi kuna Barabara ya Samora na India street huku upande wa Kaskazini na Kusini kuna barabara ya Aggrey na Mosque street lakini upande wa Kusini mwa mwa bustani hiyo ya kale kuna kaburi kongwe sana lisilokuwa na jina wala mwaka wala alama yoyote ile limekuwa mahali hapo yapata miaka karibu 200 hivi.

Je, ni nani huyu asiyekua hana jina ?
Kwanini alizikwa mahali pale tena peke yake!!

Twende sasa taratibu...
Ni wachache sana wanajua siri ya kaburi hili la mtu asijulikana wala jina lake halipo hata mamlaka zimekaa kimya juu ya kaburi hili lililopotea hasa Halmashauri ya Jiji.

Sharrif Abdul Shakur Sali'm L'attasi alifariki dunia mwaka 1862 kabla Seyyid Majjid wa Oman na wakoloni wa kijerumani kutua hapa nchini ndie alizikwa hapo.

Kwenye miaka hiyo wakati jiji la Dar es salaam paliitwa Mzizima eneo hilo kuanzia clock tower mpaka kule. Magomeni likitawaliwa na Diwani Sharif Abdul L'aatasi ambaye ndio amelazwa hapo peke yake

Kwanini alizikwa mahali pale?
Ni maswali ya kujiuliza kaburi katikati ya mji lisilo na jina limekujaje hapo

Jibu hili hapa....
Mnamo mwaka 1820 ulikuwapo msikiti ambao ulijengwa na Huyu bwana Sharif Abdul L'aatasi kwa kusaidiana na Wandugu wengine wa Mzizima wakati huo.

Msikiti huo wa udongo wa kuchoma na miti uliendelea kuwako hadi mwaka 1865 wakati Sayyed Majjid akiishi jumba alilojenga ambalo sasa ni ikulu ya Magogoni

Wakoloni walipokuja wa kujerumani mnano 1885 baada ya kifo cha Sayyed Majid walifanya kazi na Laatasi kama Kadhi mkuu mpaka alipofariki dunia

Diwani Laataasi Sharif ni mzaliwa wa Mzizima lakini anaasili ya damu ya Uajemi au Persian alikuwa maarufu sana pia aliaminika sana na Wajerumani alifariki mwaka 1860 hivi na kuzikwa nje karibu na msikiti wake
Mwanae Omary Salem L'aatasi alirithi kiti kama Kadhi mkuu.

Wakati ule ulitokea mgongano mkubwa kati ya watu na imani zao hasa baada ya wajerumani kujenga maeneo. Hayo na shughuli za kijamii eneo LA msikiti wa L'aatasi hivyo ilibidi msikiti ule uhamishwe na watachangia kujenga msikiti mpya

Basi wajerumani walitoa rupee 50 kama fidia ya jengo jipya lakini ilitoka udhuru kaburi la Diwani Sharif Abdul Shakur L'aatasi na kutunza kumbukumbu

Eneo jipya lililojengwa msikiti likawa ndio hapo Msikiti wa Ijumaa wa Kitumbini ulipo kwa sasa
Kwa kawaida Wakoloni hasa wajerumani wanaheshimu Sana makaburi hasa ya watu ambao walisaidiana na wenzao kipindi cha ukoloni.

Hivyo kaburi lake likabakia pale pale hadi Leo ambalo halikuandikwa jina(Kaburi la Asienajina) mjini kabisa
Watu siku hizi wamegeuza kiti cha kupunga upepo kaburi hilo
 
its true hilo kaburi lilikuwepo pale...m not sure if bado lipo cz i am nt in bongo,na kuna kipindi flani cha nyuma lilianza kubomolewa ikatokea ugomvi mkubwa kweli na mwishowe ndo likaachwa na kuwekewa hizo maru maru...
any one with clear maelezo please??????

Mtaalam, hili kaburi bado lipo, hata leo asubuhi nilipita hapo nimeliona limeoshwa limetakata kweli. Si unajua tena marumaru?

Kwa wanaojua, tafadhali tupe habari zaidi. Ni la mtu gani?
 
Waungwana kwa yeyote anaejua vizuri jiji la Dar maeneo ya Posta kuna kaburi moja tu la kipekee makutano ya Samora Street na India street karibu na clock tower, pembeni kidogo kuna bank ya NMB, Jmoo au maarufu kama Harbor view. Pana kontena la Voda hivi!

Hili kaburi nimejaribu kwa mda mrefu kuwauliza wale wanaoshinda eneo hilo hasa madereva tax wamesema hawajui ni la nani!Sasa ndugu wana JF kwa yeyote anaejua juu ya kaburi hili tena limejengwa kwa marumaru nyeupe anipe ufafanuzi! Je, lina uhusiano wowote na ukombozi wa taifa hili?

Je, lina uhusiano wowote na jiji la Dar? Je, lina uhusiano wowote na CCM?

Natumia simu ningeweza kupost na picha yake ila kama kuna mdau aliye jirani na eneo hilo anaeweza kupost picha naomba afanye hivyo!
 
Mimi nalijua vizuri sana lipo maeneo ninako ishi. Marehemu ni MTANZANIA wa kwanza kuwa IMAMU ktk miaka hiyo ya 1800. Usisahau maunganisho yale ni ya mitaa ya Msikiti na India na yanaendelea hadi Samora. Jina lake silikumbuki. Asante. kaburi hili limekuwa kama limetupwa lakini ni historia nzuri sana. Japo linatunzwa hakuna kibao chochote cha kuonyesha historia ya IMAMU wetu huyu.
 
Mimi nalijua vizuri sana lipo maeneo ninako ishi. Marehemu ni MTANZANIA wa kwanza kuwa IMAMU ktk miaka hiyo ya 1800. Usisahau maunganisho yale ni ya mitaa ya Msikiti na India na yanaendelea hadi Samora. Jina lake silikumbuki. Asante. kaburi hili limekuwa kama limetupwa lakini ni historia nzuri sana. Japo linatunzwa hakuna kibao chochote cha kuonyesha historia ya IMAMU wetu huyu.
Uislamu nijuavyo ulianzia kule Kilwa iweje huyu mtz azikwe pale? Je huko kilwa hakuna watz wa mwanzo kabisa walioamini uislamu? Kwanini waislamu hawamuenzi Imam wao wa mwanzo badala yake wanakaa kueneza udini kupitia kwa Alhaj JK mkweree?
 
Waungwana kwa yeyote anaejua vizuri jiji la dar maeneo ya posta kuna kaburi moja tu la kipekee makutano ya samora street na india street karibu na clock tower, pembeni kidogo kuna bank ya NMB,Jmoo au maarufu kama harbour view! Pana kontena la voda hivi! Hili kaburi nimejaribu kwa mda mrefu kuwauliza wale wanaoshinda eneo hilo hasa madereva tax wamesema hawajui ni la nani!Sasa ndugu wana jf kwa yeyote anaejua juu ya kaburi hili tena limejengwa kwa marumaru nyeupe anipe ufafanuzi!Je lina uhusiano wowote na ukombozi wa taifa hili?Je lina uhusiano wowote na jiji la dar?Je lina uhusiano wowote na ccm -majangili-mamafia-mumiani? Natumia simu ningeweza kupost na picha yake ila kama kuna mdau aliyejirani na eneo hilo anaeweza kupost picha naomba afanye hivyo!

JMoo ndo jengo gani? Mi nnavyojua JMoo ni jina la msanii wa HipHop Tanzania. Hilo jengo ni J. Mall. Usichanganye Tui na Maziwa siku nyingine.
Asante kwa kunielewa.
 
Idadi ya watu waliokwishakufa toka dunia imeumbwa ni wengi sana kulingana na makaburi yaliyoko sasa, nahisi kuna makaburi mengi sana yalifutika bila sisi kufahamu.
So possible hata hapo mliopo kuna makaburi chini ya nyumba mnayoishi
 
Niliwahi sikia juu ya hilo kaburi, hapo palikuwa na nyumba ya mhindi -Mtanzania. Alifiwa na mkewe na akuwa na mtoto, wala mrithi mwingine. Hivyo alikabidhi eneo hilo kwa Mwl. nyerere, akamwambia watu wapunzike katika eneo lile, pasijengwe chechote, mpaka hati yake ya ardihi itakapokwisha., ndipo mwl akawakabibidhi hlmashauri ya Jiji walitunze
 
Niliwahi sikia juu ya hilo kaburi, hapo palikuwa na nyumba ya mhindi -Mtanzania. Alifiwa na mkewe na akuwa na mtoto, wala mrithi mwingine. Hivyo alikabidhi eneo hilo kwa Mwl. nyerere, akamwambia watu wapunzike katika eneo lile, pasijengwe chechote, mpaka hati yake ya ardihi itakapokwisha., ndipo mwl akawakabibidhi hlmashauri ya Jiji walitunze
Kuna walakini na hoja yako ndugu!
 
Mimi nilisikia kuwa hilo ni jaribio la kutwaa eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya nyumba ya ibada ya dini mojawapo hapa tanzania. Nilijuzwa kuwa hakuna kaburi wala nini ni kwamba baada ya watu wa dini hiyo kuona kuwa ni la wazi waliamua wajenge kaburi hilo ili baadaye wawezejenga nyumba yao ya ibada. mwanzoni jiji waliondoa ujenzi huo lakini wenyewe wakarudi kwa kasi na kulijenga na kuwatisha wote watakao jaribu kuzuia mpango huo.

Hivyo hiyo ni mpango mkakati wa muda mrefu ya kutwaa eneo hilo la wazi. Kabla ya mpango huo miaka ya 1999/2000 hakukuwa na kitu hapo. Jamaa mmoja alisema hata ukichimba hapo hakuna kitu kama mabaki ya binadamu wala nini.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom