Kabul, Afghanistan: Roketi zatua karibu na Ikulu, Rais Ashraf Ghani aendelea na sala ya Eid bila kupagawa

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
332
1,000
Tarehe 20 Julai, 2021, takribani roketi tatu zilitua karibu na ikulu ya rais wa Afghanistan huko Kabul wakati Rais Ashraf Ghani alipokuwa akisali sala ya Eid al-Adha.

Ingawa hakukuwa na majeruhi waliotokana na kutua kwa roketi hizo, kilichonifanya kuwa interested na tukio hili ni pale Rais Ghani alivyoendelea na sala licha ya milipuko kusikika kwa sauti kubwa huku baadhi ya waumini wakipata tunachokiita “wenge.”

Makombora hayo, yaliyorushwa mida ya saa 2 asubuhi yalisikika na wakazi wengi wa eneo linaloitwa Green Zone, eneo ambalo ndipo ilipo Ikulu na balozi kadhaa, ikiwemo wa Marekani.

 

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,163
2,000
Taliban ndiyo yenye kwa sasa, na jana niliona Taliban delegation imepokelewa China. Taliban inawaalika wachina waje wajenge nchi na it seems wachina wako tayari kushirikiana nao. Sasa hivi ndiyo wana control barabara kuu wanakusanya kodi hiyo serikali haina mashiko
 

ze-dudu

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
15,022
2,000
Jamaa kanichekesha sana baada ya mlipuko wa kwanza kusikika kajikuta mwenyewe ndio kasimama wenzie wote wameenda chini kuendelea na sala
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom