Kabudi ungeisikiliza dhamira yako sasa viongozi wako wa dini wamekuingiza cha kike

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Siku zote dhamira ndio uhai na kioo cha nafsi ya mtu. Ndio maana dhamira ikifa mtu hugeuka kuwa kama mnyama.

Dhamira ndio mizania aliyotuwekea Mungu kupima mema na mabaya.

KABUDI wakati anaongea ikulu kwenye kutiliana saini na twiga company alisema dhamira yake ilimuambia ajiuzulu. Na alifikia mbali kusema alishaandika barua ya kujiuzulu ula barua hiyo ikachanwa na mtu fulani.baada ya hapo KABUDI akasema aliwashirikisha wazee wa kanisa na maaskofu wa kianglikana anakosali.

Maaskofu wakamwambia asifanye hivyo kwasababu atampa rais mzigo.

Hapa ndio KABUDI alipochemka maana yeye aliongozwa na dhamira ambayo ni uvuvio wa kimungu kwenye akili ya binadamu unaotusaidia kutambua mema na mabaya. Sasa akaacha kuisikiliza sauti ya kimungu yeye akawasikiliza maaskofu wake ambao wanaweza kuingizwa na maslahi yao binafsi ya kiulimwengu.

Pengine maaskofu walipima wakaona KABUDI ni msimamizi wa maslahi yao Sasa akiondoka itakuwaje? Hivyo ushauri wao kwa KABUDI ulikuwa na maslahi ya kibinadamu wakati uamuzi wa KABUDI ulikuwa na pumzi ya kimungu.

Sasa KABUDI angalia saa ya ukutani unazama na jahazi mtoto wa jalalani.Hii ngoma ya kupigwa ban haiishii kwa makonda na mkewe inakuja mpk ofisi namba ........ Nawewe ndio mtu pekee wa kuinasua nchi hapa.

KABUDI pole Sana jumba bovu linakuangukia na umeingizwa Cha kike na maaskofu wapigaji went maslahi ya kibinadamu Kama lile jamaa lenye mapengo !!

Mchelea mwana kulia hulia yeye!
 
Ofisi namba moja ijitafakari, ichukue hatua haraka ikiwemo kutangaza publicly kuwa mikutano ya vyama vya siasa ipo huru kufanyika pmj na kutangaza taratibu za kuanzisha tume huru ya uchaguzi. Vyenginevyo wasibiri waone kinachofata.
 
Kazi ya dhamiri (conscience) ni kukushauri utende lililo sahihi. Ukilitenda inakupa satisfaction, usipolitenda inakusuta.
 
Kazi ya kutambua mema na mabaya ipo kwenye akili (intellect). Jaribu kurekebisha hapo mkuu.
 
Back
Top Bottom