Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,487
- 51,064
My take:
1. Nyerere katupa katiba ya Kidikteta ya mwaka 1977, Hata alivyoitengeneza, wakati wake aligoma Haki za binadamu zisiingie ndani ya hiyo katiba
2. Mwaka 1995 Nyerere alihusika kuharibu demokrasia Zanzibar na kutengeneza precedent mbaya visiwani kila baada ya Uchaguzi
3.Sera za Nyerere za Ujamaa zilituletea Umasikini wa kutisha, watu kuvaa midabwada
4. Nyerere alituondolea mfumo wa vyama vingi na kusimika mfumo wa chama kimoja
5. Nyerere aliunga mkono maasi ya Biafra, alitaka nchi ya Nigeria igawanyike wakati yeye akidai anataka umoja wa Afrika
6. Nyerere badala ya kutumia pesa za serikali kujenga shule za Sekondari yeye akataifisha za makanisa na kuacha kujenga mpya za kutosha matokeo yake shule za sekondari zikaendelea kuwa chache, na waliobahatika kuchaguliwa kuendelea na sekondari walikuwa wachache kulinganisha na wale "waliofaulu" lakini "hawakuchaguliwa
7. Nyerere ndiye aliyekuwa kinara kuongoza Kupinga wazo la Nkrumah la Afrika kuwa nchi moja immediately, matokeo yake tumeendelea kukumbatia vinchi vidogo vidogo vyenye mipaka iliyochorwa na mkoloni!, Leo hii tungepewa heshima zaidi duniani tungekuwa linchi limoja likubwa kuliko tulivyo hivi sasa.
Conclusion:
Nyerere alikuwa kiongozi mzuri wa wastani Kisiasa, alikuwa mzuri kidiplomasia na kiukombozi dhidi ya ukoloni lakini alikuwa very poor kiuchumi.