Kabudi, Gavana wakaliwa kooni

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Kabudi, Gavana wakaliwa kooni

Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma jana hotuba kuhusu makadirio ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka ujao wa fedha, Cecil Mwambe, kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo, Anthony Komu, alisema uamuzi huo umeisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani milioni 500 (Sh. trilioni 1.1).

Waziri kivuli huyo alilieleza Bunge kuwa Juni, mwaka jana, serikali ilizindua awamu ya pili ya mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo ambao unatekelezwa kwa miaka 10 ambao malengo yake ni pamoja na kuongeza tija katika uzalishaji na kufanya kilimo kiwe cha kibiashara.

Hata hivyo, wakati serikali ikifanya hivyo, Mwambe aliliambia Bunge kuwa mapema mwaka huu, serikali kupitia Bodi ya Nafaka Mchanganyiko (CPB), iliingia makubaliano na kampuni hiyo ya Kenya kwa ajili ya ununuzi wa korosho tani 100,000 kwa bei ya Dola za Marekani milioni 180.2 (Sh. bilioni 418).

Alisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya mipango, mikakati na maelekezo ya serikali kuhusu korosho kushindwa kutekelezeka na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima wa zao hilo wanalolitegemea kama zao la biashara.

"Hata hivyo, miezi minne baadaye serikali imevunja mkataba na kampuni hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa kampuni hiyo kushindwa kutekeleza mkataba huo," alisema.

Mwambe alisema mkataba huo ambao serikali iliingia, ulitiwa saini mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria (kipindi hicho Prof. Palamagamba Kabudi), Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Innocent Bashungwa, na Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda.

Tukio la kutiwa saini kwa mkataba huo jijini Arusha Januari 30, pia lilishuhudiwa na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Prof. Florens Luoga, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu na makatibu wakuu wa wizara zinazohusika.

"Lakini tunaamini pia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vina jukumu katika mikataba hii ambayo taifa linaingia. Taarifa za kwamba kampuni hii imeshindwa kutekeleza vifungu vya kimkataba inatia ukakasi kwa kuwa lilikuwa wajibu wa serikali kwa kutumia vyombo vyake kufanya uchunguzi wa kampuni hiyo.

"Haiingii akilini kwamba vyombo vyote walishindwa kujua uwezo wa kampuni husika. Ni kwa bahati mbaya haya yanatokea na mawaziri waliohusika wako ofisini utadhani hakuna kilichotokea
"Pamoja na udhaifu huo, matamko na maelekezo ya serikali kuhusu biashara ya zao la korosho yamesababisha hasara kubwa kwa wakulima na taifa kwa sababu ambazo zingeweza kuepukwa.

"Kutokana na sakata hili la korosho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inawataka wahusika wote wajitafakari kama wanatosha kuendelea kushika nyadhifa walizo nazo ama wanapaswa kupisha ofisi hizo za umma kuongozwa na watu wengine kwa kuwa uamuzi wa CCM umelisababishia taifa hasara ya Sh. trilioni 1.18.

"Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pia inataka kufahamu ni gharama kiasi gani ambazo serikali ilitumia kukusanya zao hili la kibiashara kutoka kwa wakulima na kuzipeleka kwenye maghala ya serikali?
"Baada ya gharama zote zilizotumiwa na serikali, je, serikali ilitegemea kuuza korosho kwa bei gani? Mwambe alihoji.

Waziri Kivuli huyo pia alisema kambi yao inaishauri serikali kuboresha kwanza sekta ya kilimo na kujielekeza katika viwanda ambavyo vitaongeza thamani katika mazao ya mifugo kama vile maziwa, nyama, ngozi, damu, kwato, pembe na kusindika mazao yatokanayo na uvuvi.

Mwambe pia aliitaka serikali kuongeza bajeti ya wizara hiyo huku akiitaka ilieleze Bunge kiwango ambacho viwanda vyote vilivyopo nchini vinachangia kwenye Pato la Taifa.

Mwambe pia alisema bado wafanyabiashara wanakumbana na kadhia utitiri wa kodi na manyanyaso kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA).

Alisema kwa kipindi kirefu, TRA imeshindwa kubuni mkakati wa makusanyo ya kodi na badala yake wanatumia vibaya mamlaka katika kutekeleza majukumu na kusababisha malalamiko ya kuwapo vitendo vya rushwa.
 
wehu wa matawala ya maccm yako kama vle maviziwi,lkn upnzan mkipanga vzr nch hii 2020 n yenu,huku mtaan hal sio nzur kwa maccm,maguful kaanzisha utaratib wa kuwakama wamama wauza mboga mboga kisa kitambulisho tsh20 wamama wanalaum balaa,omb langu wabunge wote wa upnzan muwe na muda wa kurud majimbon kwenu kujua kero na kuzitolea maelekezo hl litawasaidia sana kueleweka hapo mbelen! kitendo cha kuwakamata wamama wauza mboga2 tena kanunua elf mbl we2 unamataka awe na kitambulisho cha tsh20! shame on u maccm
 
Wahujumu wakuu ndiyo hao wako ndani ya Serikali bila katiba mpya na uchaguzi huru na wa haki basi watadumu milele huku wakiendelea kuifilisi Nchi.

Utamaduni wa kuwajibika uliondoka na kina mzee Mwinyi waliobaki mpaka wafurushwe kwa aibu lakini je ninani atawatimua "wahujumu wakuu..."
 
Wahujumu wakuu ndiyo hao wako ndani ya Serikali bila katiba mpya na uchaguzi huru na wa haki basi watadumu milele huku wakiendelea kuifilisi Nchi.
Tusipopitisha katiba mpya na sheria mpya kuhusu wahujumu na mafisadi wa mali na miradi ya umma kama walivyofanya malaysia na Singapore maendeleo tutaendelea kuyasikilizia kwenye zidumu... kidumu... adumu...
Maendeleo hayana chama...!!!
 
Maendeleo watakuwa nayo hao wahuni wachache na familia zao kwa kuendelea kugawana keki ya Taifa miongoni mwao na kuwasahau mamilioni ya Watanzania wanaowaita wanyonge. Wako madarakani miaka 58, nchi imejaaliwa utajiri mkubwa sana sasa iweje karibu miaka 60 bado kuna wanyonge nchini? Nani anauyesababisha unyonge huo?

Tusipopitisha katiba mpya na sheria mpya kuhusu wahujumu na mafisadi wa mali na miradi ya umma kama walivyofanya malaysia na Singapore maendeleo tutaendelea kuyasikilizia kwenye zidumu... kidumu... adumu...
Maendeleo hayana chama...!!!
 
Maendeleo watakuwa nayo hao wahuni wachache na familia zao kwa kuendelea kugawana keki ya Taifa miongoni mwao na kuwasahau mamilioni ya Watanzania wanaowaita wanyonge. Wako madarakani miaka 58, nchi imejaaliwa utajiri mkubwa sana sasa iweje karibu miaka 60 bado kuna wanyonge nchini? Nani anauyesababisha unyonge huo?
Ati na wao WANASHANGAA NCHI KUWA MASKINI WAKIJISAHAULISHA KWAMBA WAO MIAKA 58 NDIO WATAWALA... WALISHASHINDWA KULETA MAENDELEO WAKABAKI NA NYIMBO ZISIZOISHA "MAKABWELA... MABWANYENYE... WANYONGE... MAKABAILA... MABEPARI UCHWARA... MABEBERU..."
 
Kabisa Mkuu wameshakuwa wajanja wa kutuzuga na lugha zao tamu tamu huku wakikwepa uwajibikaji wao kwa miaka chungu nzima sasa. Hizi korosho hadi leo hii hazijauzwa nani atawajibika?

Ati na wao WANASHANGAA NCHI KUWA MASKINI WAKIJISAHAULISHA KWAMBA WAO MIAKA 58 NDIO WATAWALA... WALISHASHINDWA KULETA MAENDELEO WAKABAKI NA NYIMBO ZISIZOISHA "MAKABWELA... MABWANYENYE... WANYONGE... MAKABAILA... MABEPARI UCHWARA... MABEBERU..."
 
Katika ule mchakato sikutegemea kabisa apite. Na wengi tulijua jamaa ni bomu sana, lakini haya maovu yake mengine na udikteta hatukuvijua kabisa. Kikwete na Mkapa wametuletea balaa kubwa sana nchini.

Namshukuru Mungu sikupoteza kura yangu kumpigia JIWE
 
Lakini katika mazingira kama haya tutamkumbuka mzee Kingunge,alidai Jiwe hafai kushika uongozi wa nchi bali aendelee kuwa nyapala wa mabarabara then waliowengi walidhani mzee yule kateleza but today his words are real!! Huku niliko watu wamefunga biashara zao ni hasara tu ! Na ukumbuke awamu hii it has been so hard to start a new business compare as it was before! Biashara kibao zinakufa,potential investors wanaingia mitini but huku tunarishwa matango pori kuwa uchumi unapaa! Hatari mkuu
Katika ule mchakato sikutegemea kabisa apite. Na wengi tulijua jamaa ni bomu sana, lakini haya maovu yake mengine na udikteta hatukuvijua kabisa. Kikwete na Mkapa wametuletea balaa kubwa sana nchini.

Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
 
Na cha kusikitisha na kushangaza wanavyomuogopa kuliko hata wanavyomuogopa Mungu wao hawasemi kitu bali ni kuendelea kumpamba tu.

Waseme kweli jamaa ni bomu na anakoipeleka nchi siko kabisa ili ashinikizwe asigombee tena 2020.

Lakini katika mazingira kama haya tutamkumbuka mzee Kingunge,alidai Jiwe hafai kushika uongozi wa nchi bali aendelee kuwa nyapala wa mabarabara then waliowengi walidhani mzee yule kateleza but today his
words are real!! Huku niliko watu wamefunga biashara zao ni hasara tu ! Na ukumbuke awamu hii it has been so hard to start a new business compare as it was before! Biashara kibao zinakufa,potential investors wanaingia mitini but huku tunarishwa matango pori kuwa uchumi unapaa! Hatari mkuu

Sent from my GT-I9500 using JamiiForums mobile app
M
 
Back
Top Bottom