Kabudi, Gavana wakaliwa kooni

Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
4,645
Points
2,000
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
4,645 2,000
Kabisa Mkuu wameshakuwa wajanja wa kutuzuga na lugha zao tamu tamu huku wakikwepa uwajibikaji wao kwa miaka chungu nzima sasa. Hizi korosho hadi leo hii hazijauzwa nani atawajibika?
Koroshow.. mbaazi... makinikia... udart... sgr... epz... na... na... na...
Kama si homa kuna kuumwa kichwa...
Mungu atusaidie...
 
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Messages
6,207
Points
2,000
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2010
6,207 2,000
Cheki jinsi dili lilipoanzia, likaunganishwa, likatengenezwa na kusimuliwa 'live /mubashara ' ktk video clip :
Palamagamba ni mtu wa kutengeneza ma - deal / madili

Rahisi sana kuwatapeli kina Sultan 'Mangungo', ukija kufanya deal kodisha private jet , shuhudia zoezi zima la utiaji saini na 'siasa' nyingi ktk video hapo chini :

Mfanyabishara atua na Ndege binafsi kununua tani 100,000 za Korosho

30 Jan 2019

Bodi ya Nafaka na mazao imetia saini na Kampuni ya Indo Power Solution ya kwa ajili ya Ununuzi wa Korosho Tani laki moja ambapo viongozi mbalimbali wameshuhudia mkataba huo akiwemo Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi ,Waziri wa Viwanda na biashara, Joseph Kakunda na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa mkoani Arusha.
 
Pakawa

Pakawa

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
5,040
Points
2,000
Pakawa

Pakawa

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
5,040 2,000
Maendeleo watakuwa nayo hao wahuni wachache na familia zao kwa kuendelea kugawana keki ya Taifa miongoni mwao na kuwasahau mamilioni ya Watanzania wanaowaita wanyonge. Wako madarakani miaka 58, nchi imejaaliwa utajiri mkubwa sana sasa iweje karibu miaka 60 bado kuna wanyonge nchini? Nani anauyesababisha unyonge huo?
Akina naliliii 65+ eti mpaka leo ni viongozi! ? Wapo kujineemesha na familia zao
Kuna wakati moyo unaumaaa kuyaona haya a lakini baada najiambia kila mtu atalipwa ujira wake siku atakapoiacha dunia Hii na mambo yake.
Kama jehanamu ipo nawaombea moto wa milele uwafunike ( Biblia inasema mwombee adui yako hahahhh naomba kwa mtindo huu)
 
O

Optic nerve

Member
Joined
Mar 18, 2019
Messages
5
Points
45
O

Optic nerve

Member
Joined Mar 18, 2019
5 45
Kabudi, Gavana wakaliwa kooni

Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma jana hotuba kuhusu makadirio ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka ujao wa fedha, Cecil Mwambe, kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo, Anthony Komu, alisema uamuzi huo umeisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani milioni 500 (Sh. trilioni 1.1).

Waziri kivuli huyo alilieleza Bunge kuwa Juni, mwaka jana, serikali ilizindua awamu ya pili ya mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo ambao unatekelezwa kwa miaka 10 ambao malengo yake ni pamoja na kuongeza tija katika uzalishaji na kufanya kilimo kiwe cha kibiashara.

Hata hivyo, wakati serikali ikifanya hivyo, Mwambe aliliambia Bunge kuwa mapema mwaka huu, serikali kupitia Bodi ya Nafaka Mchanganyiko (CPB), iliingia makubaliano na kampuni hiyo ya Kenya kwa ajili ya ununuzi wa korosho tani 100,000 kwa bei ya Dola za Marekani milioni 180.2 (Sh. bilioni 418).

Alisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya mipango, mikakati na maelekezo ya serikali kuhusu korosho kushindwa kutekelezeka na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima wa zao hilo wanalolitegemea kama zao la biashara.

"Hata hivyo, miezi minne baadaye serikali imevunja mkataba na kampuni hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa kampuni hiyo kushindwa kutekeleza mkataba huo," alisema.

Mwambe alisema mkataba huo ambao serikali iliingia, ulitiwa saini mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria (kipindi hicho Prof. Palamagamba Kabudi), Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Innocent Bashungwa, na Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda.

Tukio la kutiwa saini kwa mkataba huo jijini Arusha Januari 30, pia lilishuhudiwa na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Prof. Florens Luoga, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu na makatibu wakuu wa wizara zinazohusika.

"Lakini tunaamini pia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vina jukumu katika mikataba hii ambayo taifa linaingia. Taarifa za kwamba kampuni hii imeshindwa kutekeleza vifungu vya kimkataba inatia ukakasi kwa kuwa lilikuwa wajibu wa serikali kwa kutumia vyombo vyake kufanya uchunguzi wa kampuni hiyo.

"Haiingii akilini kwamba vyombo vyote walishindwa kujua uwezo wa kampuni husika. Ni kwa bahati mbaya haya yanatokea na mawaziri waliohusika wako ofisini utadhani hakuna kilichotokea
"Pamoja na udhaifu huo, matamko na maelekezo ya serikali kuhusu biashara ya zao la korosho yamesababisha hasara kubwa kwa wakulima na taifa kwa sababu ambazo zingeweza kuepukwa.

"Kutokana na sakata hili la korosho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inawataka wahusika wote wajitafakari kama wanatosha kuendelea kushika nyadhifa walizo nazo ama wanapaswa kupisha ofisi hizo za umma kuongozwa na watu wengine kwa kuwa uamuzi wa CCM umelisababishia taifa hasara ya Sh. trilioni 1.18.

"Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pia inataka kufahamu ni gharama kiasi gani ambazo serikali ilitumia kukusanya zao hili la kibiashara kutoka kwa wakulima na kuzipeleka kwenye maghala ya serikali?
"Baada ya gharama zote zilizotumiwa na serikali, je, serikali ilitegemea kuuza korosho kwa bei gani? Mwambe alihoji.

Waziri Kivuli huyo pia alisema kambi yao inaishauri serikali kuboresha kwanza sekta ya kilimo na kujielekeza katika viwanda ambavyo vitaongeza thamani katika mazao ya mifugo kama vile maziwa, nyama, ngozi, damu, kwato, pembe na kusindika mazao yatokanayo na uvuvi.

Mwambe pia aliitaka serikali kuongeza bajeti ya wizara hiyo huku akiitaka ilieleze Bunge kiwango ambacho viwanda vyote vilivyopo nchini vinachangia kwenye Pato la Taifa.

Mwambe pia alisema bado wafanyabiashara wanakumbana na kadhia utitiri wa kodi na manyanyaso kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA).

Alisema kwa kipindi kirefu, TRA imeshindwa kubuni mkakati wa makusanyo ya kodi na badala yake wanatumia vibaya mamlaka katika kutekeleza majukumu na kusababisha malalamiko ya kuwapo vitendo vya rushwa.
Kabudi anajua kula na wakubwa!Jamaa ukimuona anaongea utafikir anajua sana,issue ya makinikia iliishia wap alituaminisha pesa tutakayolipwa si ya kitoto.Kabudi endelea kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Mavipunda

Mavipunda

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Messages
5,605
Points
2,000
Mavipunda

Mavipunda

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2012
5,605 2,000
Mpaka Jiwe aje kustuka kwamba Kabudi ni kimeo basi itakuwa too late
 
Nkenangere

Nkenangere

Member
Joined
Mar 22, 2019
Messages
45
Points
95
Nkenangere

Nkenangere

Member
Joined Mar 22, 2019
45 95
Wapinzani wadandia hoja
Jina lako Jingalao linarandana na sifa yako kuu. Ujinga ni kukosa uelewa au kuea na uelewa mdogo wa jambo/mambo husika.
Susla la korosho lilipigiwa sana kelele bungeni na wapinzani. Serikali ikakurupuka kwa kudandia hoja ya upinzani ambao walipinga kutaifisha mfuko wa korosho uliokuwepo kisheria kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa korosho.
Serikali ikatumia rasilimali nyingi zikiwemo za jwtz (magari, nk.) kukusanya na kusomba korosho za wakulima bila kuwalipa. Wanunuzi wakawekwa binafsi kando kwa madai kuwa walikuwa wanawapunja wakulima.
Serikali ikaenda mbali zaidi. Ikaaminisha wananchi kuwa ingesimamia kikamilifu ubangunguaji na uuzaji nje ya nchi. Matokeo yake si siri tena: wizi na ufisadi wa kiwango cha kutisha.
Ikumbukwe kuwa serikali ilijitoa kufanya biashara. Suluhisho rahisi kwa mambo magumu!
 
Nkenangere

Nkenangere

Member
Joined
Mar 22, 2019
Messages
45
Points
95
Nkenangere

Nkenangere

Member
Joined Mar 22, 2019
45 95
Kabudi anajua kula na wakubwa!Jamaa ukimuona anaongea utafikir anajua sana,issue ya makinikia iliishia wap alituaminisha pesa tutakayolipwa si ya kitoto.Kabudi endelea kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
Napata taabu sana na wasomi wa nchi hii hususan maprofesa wengi. Ujianza na Lip . . . . Shivji na CAG ni tofauti.
 
Songambele

Songambele

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2007
Messages
4,083
Points
2,000
Songambele

Songambele

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2007
4,083 2,000
Hapa wapinzani wameogopa lawama zoote anastahili Jiwe mwenyewe hawa kina kabudi ni wacheza shoo tu.
Hiyo kampuni ilihusishwa na mgombea wa nchi jirani ambaye ni kindakindaki na Jiwe.
 
F

Froida

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2009
Messages
8,527
Points
2,000
F

Froida

JF-Expert Member
Joined May 25, 2009
8,527 2,000
Kabudi zero kabisa mwongo mkubwa
 
Tabutupu

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Messages
7,059
Points
2,000
Tabutupu

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2010
7,059 2,000
Kabudi, Gavana wakaliwa kooni

Akiwasilisha bungeni jijini Dodoma jana hotuba kuhusu makadirio ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka ujao wa fedha, Cecil Mwambe, kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo, Anthony Komu, alisema uamuzi huo umeisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani milioni 500 (Sh. trilioni 1.1).

Waziri kivuli huyo alilieleza Bunge kuwa Juni, mwaka jana, serikali ilizindua awamu ya pili ya mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo ambao unatekelezwa kwa miaka 10 ambao malengo yake ni pamoja na kuongeza tija katika uzalishaji na kufanya kilimo kiwe cha kibiashara.

Hata hivyo, wakati serikali ikifanya hivyo, Mwambe aliliambia Bunge kuwa mapema mwaka huu, serikali kupitia Bodi ya Nafaka Mchanganyiko (CPB), iliingia makubaliano na kampuni hiyo ya Kenya kwa ajili ya ununuzi wa korosho tani 100,000 kwa bei ya Dola za Marekani milioni 180.2 (Sh. bilioni 418).

Alisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya mipango, mikakati na maelekezo ya serikali kuhusu korosho kushindwa kutekelezeka na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima wa zao hilo wanalolitegemea kama zao la biashara.

"Hata hivyo, miezi minne baadaye serikali imevunja mkataba na kampuni hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa kampuni hiyo kushindwa kutekeleza mkataba huo," alisema.

Mwambe alisema mkataba huo ambao serikali iliingia, ulitiwa saini mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria (kipindi hicho Prof. Palamagamba Kabudi), Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Innocent Bashungwa, na Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda.

Tukio la kutiwa saini kwa mkataba huo jijini Arusha Januari 30, pia lilishuhudiwa na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Prof. Florens Luoga, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Balozi wa Kenya nchini, Dan Kazungu na makatibu wakuu wa wizara zinazohusika.

"Lakini tunaamini pia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vina jukumu katika mikataba hii ambayo taifa linaingia. Taarifa za kwamba kampuni hii imeshindwa kutekeleza vifungu vya kimkataba inatia ukakasi kwa kuwa lilikuwa wajibu wa serikali kwa kutumia vyombo vyake kufanya uchunguzi wa kampuni hiyo.

"Haiingii akilini kwamba vyombo vyote walishindwa kujua uwezo wa kampuni husika. Ni kwa bahati mbaya haya yanatokea na mawaziri waliohusika wako ofisini utadhani hakuna kilichotokea
"Pamoja na udhaifu huo, matamko na maelekezo ya serikali kuhusu biashara ya zao la korosho yamesababisha hasara kubwa kwa wakulima na taifa kwa sababu ambazo zingeweza kuepukwa.

"Kutokana na sakata hili la korosho, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inawataka wahusika wote wajitafakari kama wanatosha kuendelea kushika nyadhifa walizo nazo ama wanapaswa kupisha ofisi hizo za umma kuongozwa na watu wengine kwa kuwa uamuzi wa CCM umelisababishia taifa hasara ya Sh. trilioni 1.18.

"Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pia inataka kufahamu ni gharama kiasi gani ambazo serikali ilitumia kukusanya zao hili la kibiashara kutoka kwa wakulima na kuzipeleka kwenye maghala ya serikali?
"Baada ya gharama zote zilizotumiwa na serikali, je, serikali ilitegemea kuuza korosho kwa bei gani? Mwambe alihoji.

Waziri Kivuli huyo pia alisema kambi yao inaishauri serikali kuboresha kwanza sekta ya kilimo na kujielekeza katika viwanda ambavyo vitaongeza thamani katika mazao ya mifugo kama vile maziwa, nyama, ngozi, damu, kwato, pembe na kusindika mazao yatokanayo na uvuvi.

Mwambe pia aliitaka serikali kuongeza bajeti ya wizara hiyo huku akiitaka ilieleze Bunge kiwango ambacho viwanda vyote vilivyopo nchini vinachangia kwenye Pato la Taifa.

Mwambe pia alisema bado wafanyabiashara wanakumbana na kadhia utitiri wa kodi na manyanyaso kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA).

Alisema kwa kipindi kirefu, TRA imeshindwa kubuni mkakati wa makusanyo ya kodi na badala yake wanatumia vibaya mamlaka katika kutekeleza majukumu na kusababisha malalamiko ya kuwapo vitendo vya rushwa.
Kabudi hayupo makini anapenda sana sifa.. Gavana wa BOT alitakiwa kuikataa ile kazi kwa sababu alikua anajua amepelekwa pale kutetea maslahi ya kisiasa.

Magavana siku zote huwa wanakua watalaam kwa maana ya uzoefu kwenye financial institution kwenye mashirika ya kimataifa.

Anajipendekeza kwa mambo ambayo hayahitaji hata utalaam.
 
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
4,645
Points
2,000
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
4,645 2,000
Kabisa Mkuu wameshakuwa wajanja wa kutuzuga na lugha zao tamu tamu huku wakikwepa uwajibikaji wao kwa miaka chungu nzima sasa. Hizi korosho hadi leo hii hazijauzwa nani atawajibika?
Watakaowajibishwa kwenye suala la korosho ni wakulima wenyewe ili kufidia "uzembe na hujuma zinazofanywa juu yao" KWA MAANA WAO NDIO WANYONGE
 
O

Onjwaria

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
565
Points
500
O

Onjwaria

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
565 500
Mdee alishasema ni professor wa hovyo ila anaula sababu kila akipewa muda lazima atumie dk 10 na ushee kumsifia rais halafu 10 nyingine kuiponda upinzani. Hii ndiyo style ya kuula ukiwa serikali ni ila ukitaka mambo yako yasinyooke thubutu kuacha kutaja jina la mheshimiwa. Tazama bungeni, wabunge wa ccm makusudi hawajikiti kuibana serikali ila wanaangaika kusifia juhudi hadi dk zao za kuchangia zinaisha
 
O

Onjwaria

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Messages
565
Points
500
O

Onjwaria

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2016
565 500
Suala la korosho alaumiwe rais Magufuli kwa kina lake na kutumia vibaya madaraka yake. Waziri Mkuu alikuja na pendekezo ajabu akatoa amri pale pale na kuwapa JWTZ kukusanya korosho chini ya amri yake. Matokeo ndiyo hii ya hasara tunayoiona sasa. Tatizo hapa ni katiba kumpa rais madaraka makubwa mno. Hili suala la korosho asingejiingiza na hii yote ni kutowaamini walioko chini yake.
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
90,108
Points
2,000
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
90,108 2,000
Ndiyo kawaida ya hawa wahuni Mkuu. Wakishafanya maamuzi ya kipuuzi yanayotugharimu Watanzania miaka yote hukingiana vifua.

Watakaowajibishwa kwenye suala la korosho ni wakulima wenyewe ili kufidia "uzembe na hujuma zinazofanywa juu yao" KWA MAANA WAO NDIO WANYONGE
 
K

Kilangila

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Messages
1,350
Points
2,000
K

Kilangila

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2013
1,350 2,000
Wapinzani wadandia hoja
Hujui hata kazi ya upinzani bungeni halafu unajifanya mtetezi was CCM! Kiukweli wewe ni mpotoshaji was CCM. CCM itaingia hasara kubwa kama itawaamini watu kama wewe. Kilangila.
 
K

Kilangila

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Messages
1,350
Points
2,000
K

Kilangila

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2013
1,350 2,000
Kati ya viongozi wa hovyo kuwahi kutokea nchini Prof. Kabudi ni mmoja wapo
Uko sahihi maana amesahau yote aliyokuwa anaongea wakati anapigania katiba mpya. Kilangila.
 
K

Kilangila

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Messages
1,350
Points
2,000
K

Kilangila

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2013
1,350 2,000
Tusipopitisha katiba mpya na sheria mpya kuhusu wahujumu na mafisadi wa mali na miradi ya umma kama walivyofanya malaysia na Singapore maendeleo tutaendelea kuyasikilizia kwenye zidumu... kidumu... adumu...
Maendeleo hayana chama...!!!
Tunaona jinsi ambavyo wenzetu wa Kenya wanavyo songa mbele kwa spidi ya Jet. Kilangila.
 
K

Kilangila

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Messages
1,350
Points
2,000
K

Kilangila

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2013
1,350 2,000
Ati na wao WANASHANGAA NCHI KUWA MASKINI WAKIJISAHAULISHA KWAMBA WAO MIAKA 58 NDIO WATAWALA... WALISHASHINDWA KULETA MAENDELEO WAKABAKI NA NYIMBO ZISIZOISHA "MAKABWELA... MABWANYENYE... WANYONGE... MAKABAILA... MABEPARI UCHWARA... MABEBERU..."
Najiuliza kila siku kwani miaka yote hiyo nchi hii ilikuwa chini ya utawala was chama gani? Kilangila.
 
Forum statistics

Threads 1,295,954
Members 498,495
Posts 31,228,989
Top