Kabrasha chumba cha kunyongea

Adhabu ya kunyongwa hadi kufa, ni mojawapo ya adhabu kongwe na ya kuogofya zaidi duniani... Na ndio adhabu ya juu zaidi.... Kunyongwa hadi ufe kabisa baada ya kuthibitishwa na mahakama tuhuma zako
Kuna taratibu ngumu na za muda mrefu hadi mtuhumiwa afikie kunyongwa kwakuwa kuhukumiwa kunyongwa ni jambo la kwanza lakini kutimizwa kwa adhabu ni jambo lingine... Unaweza ukahukumiwa kunyongwa na usinyongwe, ni mpaka mkuu wa nchi asaini hati yako ya kifo ndio unaweza kunyongwa!
Kabrasha la chumba cha kunyongea ni kubwa hivyo tuangalie dondoo zake wiki ya mwisho ya kutekeleza adhabu hasa masaa 72 ya mwisho...!!!! Maandalizi huwa mengi lakini haya ndio muhimu zaidi
. Viongozi wa dini huandaliwa kuja kuongea na wale wote wanaosubiri kitanzi..
. chumba cha kunyongea hufanyiwa ukarabati
Mnyongaji huandaliwa
. askari wasaidizi huandaliwa hawaambiwi kuna nini bali huambiwa wanaandaliwa kwa kazi maalum

Siku ya mwisho kuamkia kunyongwa
Ataanza Kiongozi wako wa dini kuongea nawe mara ya mwisho.. Kwa baadhi ya mazingira anaweza kuitwa hata rafiki yako ndani ya gereza
Utapewa chochote unachotaka hasa chakula na kinywaji... Baadhi hudai mpaka damu ya mnyama, sigara ama chakula chochote cha gharama.... Kwa sehemu kubwa hutimiziwa mahitaji yao haya...
Ni usiku wa kuamkia unyongaji, mnyongaji aliyeandaliwa huwekwa mahali pa pekeyake akipombeka usiku kucha
Kunapambazuka... Kiongozi wa chumba cha kunyongea hutoa amri ya wanyongwaji wote kuletwa chumba cha 'condemn' kazi hii hufanywa na wale askari wa kazi maalum
. chumba cha condemn mlangoni kina alama ya X nyekundu na fuvu kubwa...
Wanyongwaji wakiwa tayari na taarifa kuwa huo ndio mwisho wao wakishaingia tu hapa hufungwa vitambaa vyeusi usoni.. Na pingu kubadilishwa toka kufungwa kwa mbele mikononi na kufungwa kwa nyuma
Baada ya hapo huingizwa mlango wa pili kisha mlango wa tatu na wa mwisho ambako ndio kuna kitanzi
Baada ya kufika chumba cha kunyongea huvishwa kitanzi (kwa nchi nyingi za kiafrika) na mnyongaji hubonyeza kitufe kinachofungua milango ya sakafuni na mnyongwaji huning'inia na kitanzi kukaza shingoni na kunyonga....
Baada ya hapo mnyongaji anakuwa ameshaliza kazi yake, sasa kazi ya kwenda chini kufungua vitanzi na pingu na kuvuta miili juu ni ya askari wa kazi maalum... Kazi hii huwa ngumu na ya kutisha maana miili huwa na kila aina ya sura na miili mingine ikiwa bado inavuja damu.. ..
.Wakati wa kuivuta miili juu haivutwi kama unaopoa kitu majini bali hufungwa kamba miguuni na kuiweka mshazari na kuipandisha juu kama jeneza
Baada ya hapo huvuliwa nguo fasta na kuvalishwa shuka la sanda tena mwili ukiwa bado wa moto
Wafungwa walioandaliwa huchukua miili husika na kwenda kuizika fasta kwa makaburi yaliyokwisha chimbwa jana yake... Huko makaburini ni kufukiwa tu na si kuzikwa kwa heshima
Baada ya hapo wahusika wote hulipwa kulingana na majukumu yao na bwana mnyongaji hukamatwa na kupelekwa kizimabani na kusomewa mashtaka ya mauaji.... Naye hukiri kosa kwa kunukuu vifungu kadha vya Jamhuri ya nchi na hatimaye kuachiwa huru.....

Sehemu ijayo tutaendelea na vituko vya wanyongwaji
Asanteni

Kabrasha chumba cha kunyongea - JamiiForums
Kabrasha chumba cha kunyongea - JamiiForums

Nini dhana ya mnyongaji kukamatwq kufikishwa kizimban na kuachiwa huru!?
Kwann!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Licha ya kuwa ni kifo cha kuogopesha, kina faida nyingi sana ambazo si kila mmoja wetu anabahatika kuzipata.

1. Unajiandaa kwa kifo chako, unapata fursa ya kuagana na ndugu, jamaa na marafiki.

2. Muhimu zaidi, unakuwa kwenye hali ya toba, unapata nafasi ya kutengeneza na kuweka mambo sawa na muumba wako kwa kadri ya imani yako.

3. Unatumia muda mwingi kuwapa wengine maneno ya kuwaongeza imani, mafundisho na ushauri wa kuwa waumini wema.

Kwa ufupi, nimejifunza mambo makubwa sana kupitia huu uzi.

Shukrani Mshana Jr
 
Hiyo namba mbili tu

Jr
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom