Kabla ya wanasiasa kusema machinga ni nani, kuwapatia maeneo ni kazi ngumu sana

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,492
2,000
Duniani kote "mmachinga" ni yule mtu anaetembeza bidhaa zake kwa kutembea nazo mikononi mwao au kwenye begi la mgongoni akitafuta waliko wanunuzi. Yaani badala ya mnunuzi kufuata bidhaa (dukani), mara hii mwenye bidhaa (duka) ndiye anaemfuata mnunuzi. Wafanyabiashara wa aina hii sio kero sana na hawahitaji kupewa maeneo.

LAKINI kuna watu wanasiasa wanawaita machinga pia kimakosa. Hawa ni wale wenye bidhaa nyingi kiasi cha kushindwa kuzibeba zote mikononi au kwenye begi la mgongoni hivyo wanazipanga chini au kujenga vibanda ili kuziuzia hapohapo walipozipanga. Bidhaa hizi ni nyingi kiasi kwamba zinahitaji ulinzi dhidi ya wezi, jua na mvua. Zinahitaji eneo (space), mwanga usiku na mchana, vifaa vya kuweka taka, vyoo, sehemu ya kula ya karibu na yenye miundombinu mingine.

Hawa sio machinga bali ni watu waliostahili kufungua viduka kwenye fremu hukohuko kwenye mitaa wanakoishi mijini na vijijini kama wanavyofanya wengine ili walipe kodi ya kukadiriwa. Watu hawa ndio kero halisi kwakuwa wanahitaji nafasi ili kupanga na kuuza bidhaa zao sehemu zenye wanunuzi, hivyo kusababisha kutumia maeneo yasio rasmi. Huyu sio machinga, ni mkora tu ambae anafuata wateja kwa kunyanganya haki za watu wengine kama vile kupanga bidhaa zake eneo ambalo lina matumizi ya watu wengine, kuweka bidhaa kwenye vumbi na tope na kuhatarisha afya za wengine, na kusababisha ajali kwa watu wengine.

Serikali haipaswi kuwatafutia maeneo hawa wanaopanga chini na kujengea shelters bidhaa zao, badala yake serikali ilinde na kusimamia mipango miji yake; itoe marufuku watu kufanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa basi. Wafanyabiashara wa hivi waende kwa maofisa biashara wa vilaya, tafara, kata na vijiji wakaelekezwe utaratibu wa kufungua biashara zao kwenye maeneo yatakayokaguliwa. Maana hawa ni watu ambao idadi yao haifahamiki, hivyo huwezi kuwatengea maeneo ikatosha. Wanatoka vijijini na mijini kila siku baada ya kumaliza darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita, na vyuo.

Lazima tutoe tafsiri halisi ya nani ni machinga na nani sio machinga huko mitaani, vinginevyo ni kuwatwisha zigo wakuu wa mikoa wasiloliweza. Maeneo ya kutosha kujenga vibanda wenye badhaa nyingi watayatoa wapi? kwanini wasiende kufungua viduka mitaani sawa na wengine?
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,606
2,000
Nyie endeleeni kupotea tu na msijue kwa Tz neno machinga sahivi ni neno pana na lenye maana pana sana. Walivyo 95% ya wanakijiji kuwa wakulima ndivyo ilivyo wafanyabiashara wadogo wote kuwa machinga haijalishi anauza amekaa, amesimama ama anatembea. Na hawa ni dada zetu, mama zetu, shangazi zetu, kaka zetu, baba zetu na wajomba zetu.

Hawa ndo sisi wanyonge 90% parcel. Kwahiyo unapodili na machinga unadili na wanyonge wa nchi hii ambao wanasomesha, wanaleta chakula, wanauguza na ndo hao hao wanaolipia wenye nyumba hizo tozo zenu za wizi kupitia nyumba za kupanga.. Kuweni makini kabla kitumbua hakijaingia mchanga
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,492
2,000
Nyie endeleeni kupotea tu na msijue kwa Tz neno machinga sahivi ni neno pana na lenye maana pana sana. Walivyo 95% ya wanakijiji kuwa wakulima ndivyo ilivyo wafanyabiashara wadogo wote kuwa machinga haijalishi anauza amekaa, amesimama ama anatembea. Na hawa ni dada zetu, mama zetu, shangazi zetu, kaka zetu, baba zetu na wajomba zetu. Hawa ndo sisi wanyonge 90% parcel. Kwahiyo unapodili na machinga unadili na wanyonge wa nchi hii ambao wanasomesha, wanaleta chakula, wanauguza na ndo hao hao wanaolipia wenye nyumba hizo tozo zenu za wizi kupitia nyumba za kupanga.. Kuweni makini kabla kitumbua hakijaingia mchanga
Sera zetu ndizo zilizotufikisha hapo tulipo, kila sehemu ina baa na kila sehemu ina biashara, hata maofisini watu wanachuuza tu na hata wenye ajira hawazithamini kazi zao kwakuwa ajira hazitoi majibu kwa maswali yao mengi ya maisha na matumizi. Hata hivyo, ukosefu wa ajira ni changamoto ya ulimwengu lakini ufumbuzi wake sio huu wa kuwaacha watu wachuuze kila sehemu yenye nafasi. kufanya hivi ni kuahirisha tatizo kwa muda na kutengeneza tatizo kubwa zaidi.

Iko siku machinga hawa watakuja uana wenyewe kwa wenyewe wakigombea nafasi na wateja, wataungana na kuana na waenda kwa miguu na wenye magari waliokanyaga bidhaa zao, watauana na polisi na wanasiasa kwa kuwaambia wasogeze bidhaa zao, watauana na wafanyabiashara wakubwa kwa kuingiliana kwenye biashara.

Unapomwambia Mkuu wa Mkoa awatafutie maeneo hawa jamaa ni porojo tu za kisiasa, kwakuwa hawa jamaa hawana idadi maalumu na wanaongezeka kila siku, wiki, mwezi na kila mwaka. Hayo maeneo yako wapi? atayapata wapi?. Je, machinga complex inatosha machinga wangapi?

Kifupi, CCM haiwezi kulitatua tatizo la wamachinga kwakuwa ni sehemu kamili ya tatizo lenyewe. Open spaces zote zimevamiwa na watu wa aina hiyo na viongozi wa CCM wana watu wao miongoni mwa wavamizi wa maeneo ya wazi na yale yasiyofaa. Hata barabara ya airport, Nyerere road watu wamejenga vibanda na kukoka moto wa kupika makongoro ya vingunguti
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,606
2,000
Waliikataa siasa ya ujamaa na kibaya zaidi wakaikataa sera ya kujitegemea kwa kuiga mifumo ya kibepali. Haya sasa nchi ina kundi moja tu la nguvu kazi, wamachinga. Na bado hawana mda wa kurekebisha sera na kwa akili ndogo wanapambana na matawi na kuacha mzizi wa matatizo
 

muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
1,499
2,000
kuna machinga wengine wameweka bidha barabarani ila ukiangalia bidhaa zao ni zaidi ya duka zima
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,492
2,000
kuna machinga wengine wameweka bidha barabarani ila ukiangalia bidhaa zao ni zaidi ya duka zima
Tunawatwisha wakuu wa mikoa mzingo usiostahili na wasiouweza. Mtu aliyesimika banda la biashara yake kwenye mtaro wa majitaka na njia za waenda kwa miguuwa mkuu wa mkoa atatumia muujiza gani kuwaondoa hapo bila kulazimika kutumia nguvu?

Nchi nzima inachuuza, hata professor wa nchi lazima awe na mabanda ya kufugia nguruwe na kuku ili awe na afadhali. Mtu kama huyu hawezi kufocus wala ku concentrate kwenye taaluma yake, anakuwa common person kwenye kazi zake, maana kazi yake inashindwa kumpatia majibu yote ya maisha kama msomi. Wanajamii wananunua maji ya kisima nyumbani kwa professor.
 

muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
1,499
2,000
Tunawatwisha wakuu wa mikoa mzingo usiostahili na wasiouweza. Mtu aliyesimika banda la biashara yake kwenye mtaro wa majitaka na njia za waenda kwa miguuwa mkuu wa mkoa atatumia muujiza gani kuwaondoa hapo bila kulazimika kutumia nguvu?

Nchi nzima inachuuza, hata professor wa nchi lazima awe na mabanda ya kufugia nguruwe na kuku ili awe na afadhali. Mtu kama huyu hawezi kufocus wala ku concentrate kwenye taaluma yake, anakuwa common person kwenye kazi zake, maana kazi yake inashindwa kumpatia majibu yote ya maisha kama msomi. Wanajamii wananunua maji ya kisima nyumbani kwa professor.
sahihi kbs
 

J.wawatu

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
357
1,000
Hili tatizo la machinga wakizidi kuliweka kisiasa huko mbeleni ndiyo litakuwa baya zaidi.
Watu wataanza kukodi store badala ya frem za maduka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom