Kabla ya mapambazuko ni mapambano sharti apingwe ni mkoloni hata kama wazo lake ni zuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kabla ya mapambazuko ni mapambano sharti apingwe ni mkoloni hata kama wazo lake ni zuri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by UWEZO_WAKO, Apr 16, 2012.

 1. UWEZO_WAKO

  UWEZO_WAKO Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnyonge mnyongeni lakini ukweli Arusha imeonyesha kuwa Bengazi ya ukweli. Matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru mashariki umefungua ukurasa mpya kabisa wa mapambano dhidi ya haki na uonevu. Huwezi kuamini kilichokuwa kinatokea maana kilichotokea huko huwa ni hatua ya juu kabisa kihistoria wakati ukoloni unashindwa. Kwanza katika hatua hiyo watu huwa wanajitolea kwa kiasi kikubwa sana kwa kutoa michango ya hali, mali na hata maisha. Yaani wakati mkoloni anatumia fedha za kodi ya wananchi ili aendeleze utawala wake dhalimu, wananchi waliochoka na maonevu walikuwa wakichanga fedha kuwezesha kumg'oa mkoloni.
  Moja ya hotuba za Mwalimu akieleza mapambano yalivyokuwa dhidi ya mkoloni ni kwamba walikuwa kazi moja nayo ni kumpinga na kumpinga, ni kupinga tuuuuu hata kama mkoloni akija na wazo zuri ni mkoloni kazi ilikuwa ni kumpinga tu. Mwanasiasa mzuri wakati huo alijulikana kwa uwezo wake wa kupinga. Lengo kubwa la Mwalimu kutoa hotuba hiyo mara baada ya uhuru ni kuwataka wanasiasa wa kipindi hicho kuwa sasa muda wa kupinga kila jambo umekwisha, mwanasiasa bora sasa ni mwenye mawazo na sera nzuri za kujenga nchi. Mimi naona sasa ni kipindi cha kupinga na ndicho kilichotokea Arumeru Mashariki, wananchi wameshaelemishwa na wakamjua mnyonyaji/mkoloni wao ni nani kwa hiyo walikuwa na kazi moja ya kumpinga kwa kila jambo...Mpingeni shetani kwa nguvu zote naye atawakimbia (neno la Bw linasema hivyo). Shetani hana jipya hata yale mazuri anayokuonyesha au kukuahidi ni hila tu mwisho wa siku ni kukuangamiza tu.

  Mkoloni kishajulikana (hata wao wenyewe wanajijua na sasa wanasema mara kujivua gamba, mara kuna mpasuko, mara udini, nk) kazi ni kumpinga tu hata akija na wazo zuri apingwe tu alikuwa wapi miaka yote hiyo 50. Wakizuia mikutano mkoa huu, kimbileni mji mwingine, Bunge likisha huku rudini tena, kitaeleweka tu. Mwaka 2015 tutakuwa na muda mfupi wa mapumziko lakini ndio utakuwa ukurasa mpya wa kazi ngumu kujaribu kujenga nchi iliyoharibiwa na mkoloni...wakati huo pia makanda wote waliopoteza maisha watakumbukwa tena kwa machozi kwa mchango wao katika vita dhidi ya mkoloni mweusi. Sasa hivi hakuna kulala, tutakuwa na mapumziko mafupi mara baada ya uchaguzi 2015.
   
Loading...