Kabla ya MaDC kufukuzwa kwa baa la njaa tujiulize nani aliuza ardhi ya vijiji? Walengwa walime wapi?

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Wana Jf,

Nawaonea huruma sana MaDC kwa kuishi kimashaka kama ikitokea kwao baa la njaa likawakumba, pengine ni kutokana na jiographia kuwa wananchi wazazi wao walipopachagua kuishi na kupaita kwao ni full ukame na wanaishi hapo kwa kutangatanga kufuatia urithi walioukuta. Wengine walinyanganywa ardhi ikafanywa poli la akiba.

Wengine kutokana na kabila zao walizaana sana Ardhi haiwatoshi na mashamba no madogo. Mfano walimala ndizi wote kagera na Kilimanjaro Ardhi haiwatoshi kabisa, kama makabila ya wahaya na wachaga wangeambiwa kila MTU arudi kwao la hasha hapatoshi kabisa.

Ardhi nyingi za vijiji ambavyo Nyerere aliviacha ili isaidie watu kulima mazao ya kimkakati kama vile mtama, ulezi, karanga, mihogo michungu yote wameuziwa matajiri na kupanda miti ya mipaini. Nakumbuka mwaka 1982 kulitokea njaa kali, Nyerere akaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia wanakijiji kila mtu aonyeshe shamba robo heka la viazi vitamu na mihogo, mkoa wa Kagera magari ya jeshi yalikuwa yanatumika kusambaza mbegu za mihogo lakini siku hizi kulima kumepewa kisogo na matajiri wakapata fursa ya kijitwalia ardhi.

Kwa sasa ukiwambia walime maskini ndio wakwanza kukwama.

Kabla ya kuwafukuza madc waanze kurejesha ardhi za vijiji zilizopolwa na wahusika wachukuliwe hatua
 
Lakini hio si kwa maeneo yote.
Unakumbuka kilimo cha kufa na kupona sikumbuki mwaka lakini njaa iliondolewa baada ya kuambiwa majeshi yasimamie Lila Kijana mwenye umri miaka 18 aonyeshe shamba la mihogo au viazi vitamu
Kuwa iko hivyo.
 
Unakumbuka kilimo cha kufa na kupona sikumbuki mwaka lakini njaa iliondolewa baada ya kuambiwa majeshi yasimamie Lila Kijana mwenye umri miaka 18 aonyeshe shamba la mihogo au viazi vitamu
Mi nazungumza kuhusu mashamba. Kuuzwa
 
Back
Top Bottom