Kabla ya mabadiliko kutimia kuna uwezekano wa kumwaga damnu ya viongozi wa kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kabla ya mabadiliko kutimia kuna uwezekano wa kumwaga damnu ya viongozi wa kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Sep 9, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,041
  Likes Received: 37,834
  Trophy Points: 280
  Watanzania wenzangu taifa letu liko katika kipindi cha mpito kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli.Ni katika kipindi hiki tutarajie mambo mengi ambayo wengi hatukuyazoe kuyaona bali kuyasikia ktk mataifa mengine.

  Hata hivyo, nchi yetu si kisiwa.Yanayotokea katika mataifa mengine hata hapa kwetu yanaweza kutokea.Teyari tuna mifano ya wananchi wanaouwawa kikatili katika mikutano ya kisiasa kwa sababu zinazoniwa kuwa ni za kisiasa.Mabadiliko ya kiutawala ktk nchi nyingi huambatana na umwagaji mkubwa wa damu.Mifano ni mingi si hitaji kuitaja.

  Mtu anaeweza kuua kitoto kichanga anaweza pia kuua mtu mzima.Ukatili wa kuua binadamu hauna mipaka.Ukiwa na roho ngumu ya kuua binadamu basi binadamu yoyote unaweza kumuua tu.

  Viongozi wa vyama vya kisiasa muwe makini si ajabu kesho ikawa zamu yenu.Leo wanauwawa wanachama na wafuasi wa kawaida ila mjue nanyi kesho hamko salama.Chukueni tahadhari.Pia mjiulize ni kwanini hakuna uwajibikaji kwa mauaji haya.Mjiulize ni kwanini hawataki kuunda tume huru.

  Wakati mnaendeleza harakati za mabadilko mjue na hatari inayowakabili.

  Hii ni vita bubu.
   
Loading...