Kabla ya Kuwashtaki kwa "Uhujumu Uchumi" Wachawi Wetu; Swali hili Serikali ilijibu kwanza..

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwani kwa nini tuliacha kulipa deni ambalo tulishakubali kuwa ni halali na tulishaanza kulilipa?

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com


Hitimisho lako lina swali la msingi sana. Kabla ya kuendelea na hatua nyingine yeyote, yapasa majibu mazuri yatolewe na serikali kuhusu hilo swali.

Ikiwa kutokulipa ilikuwa ni maamuzi halali ya serikali; basi bila shaka walijua tukio kama hili lingeweza tokea na tayari walijipanga. Kufeli kokote ama hasara itayopatikana wakubali kupokea lawama zote wao kama ambavyo watapongezwa wakifaulu.

Ikiwa ni mtu mmoja au kikundi cha watu na sio maamuzi yaliyofuata taratibu zinazotakiwa, basi hao watu ama hiko kikundi wawajibishwe kwa kadiri ya hasara iliyoingizwa. Wao ndo watakuwa watu sahihi wa kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.

Twende kukata mzizi, tusihangaike na matawi.

 
JPM kazungumzia lini swala la ndege? kuwa anahujumiwa?

Kingine jaribu kuwa na heshima kwa mtu mzima, achilia mbali rais. Ungekuwa aliyekuzaa alibakwa na umekuzwa mtaani sawa, try to prove otherwise
Mtu mzima gani unamuongelea wewe Lumbu buku 7?? Mzee Meko???
 
Kwani huyo ndo wa kwanza kuidai serikali? Kwani serikali haijazoea madeni?

Lazima wawajibishwe waliosuka mchongo kuibua swala ambalo muhusika binafsi hakua na mpango nalo, ingekua ni kwania njema angetoa taarifa kwanza kwa serikali ila kwakua alikua hajui chochote ni wanasheria wasio na nia njema walimjaza ujinga na kumshinikiza
Unasemaje mkulima hakuwa na mpango wakati aliandika barua pepe kuitahadharisha serikali atachukua uhamuzi wa kudai haki yake mahakama za nje ingawa hakupenda afikie hatua hiyo?

Tuache kifukia uvundo, kuna kiburi na uzembe ulifanywa na watanzania wenzetu wenye dhamana.

Hao wanasheria watanzania waliomshauri kama kweli ilikuwa hivyo wao walikuwa wanatafuta kipato chao wakilipwa gharama za ushauri.
 
Kama kweli hoja kuu juu ya kutaka ndege iachiliwe ni kwa vile inatumiwa na rahisi basi Ni wazi namna pekee ya kuiachilia ni kukaa chini na Steyn na kukubaliana ni kwa namna gani tutalipa deni lililobakia.
 
Kama kweli hoja kuu juu ya kutaka ndege iachiliwe ni kwa vile inatumiwa na rahisi basi Ni wazi namna pekee ya kuiachilia ni kukaa chini na Steyn na kukubaliana ni kwa namna gani tutalipa deni lililobakia.
Dawa kulipa tu hakuna mjadala
 
Kwa maoni yangu, bila kujali kuwa serikali haikulipa deni au ilikaidi deni, ushikwaji wa ndege ile ni makosa makubwa sana ambayo yanaweza kumfanya mdai ndiye awe mdaiwaji. Kwa SA, sheria ya madeni inamtaka mdai amuarifu mdaiwa na mahakama kwa pamoja kuwa mdai asipolipa deni kabla ya siku fulani basi anaiomba mahakama imchukulie hatua fulani. Sijaona hapa kama kweli mawasiliano hayo yalifanyika badala ya kukurupushana tu. Hata mahakama yenyewe inaweza kuwa imefanya makosa katika kutoa amri hiyo kama hakukuwapo mawasiliano ya aina hiyo, lakini ngoja tusubiri kwa vile mahakama ndiyo imeshika mpini sasa pamoja na kufanya makosa ya kutoa amri hiyo.

Kinachonishangaza ni ile shallowness ya wanasheria wetu, wanakimbilia kusukuma hoja za mambo madogo madogo tu badala ya kuchimba sheria nzima inayotawala kudaiana madeni ya South Africa
 
Naona Sasa MMkijiji umeelewa somo...ulisimama upande wa walipwe I hope kuna la kujifunza limekufikia.regime hii umekuwa safi sana kuitendea haki . kwa uturivu uliojenga kwa misingi kwamba unakubariana na uchapa kazi wenye mwelekeo wa yale unayo yaamini.Sijui hili la Mkoloni Styen na wapigaji wa Kibongo walikwaminisha nini hasa hadi ukaja na bandiko hili, ambalo sikuelewa ulipotoka wapi hadi kuwaza hayo uliyo waza.Anyway wakati mwingine watu wazima akikosea inabidi wadogo tukooe na si kuwakoromea.
 
Hii serikali inapesa za kuchezea tu,kama vile kukusanya watendaji wa kata nchi zima na kuanzisha dili la ununuz wa madiwan na wabunge ili uchaguz urudiwe wkt nchi inamadeni haiwapandishi madaraja watumishi na kama wko walo panda n wale wenye elements za ucccm! Sasa ndege imedakwa hafu wanalalamika wkt hamlip maiden ya nchi
 
Kama Magufuli anahujumiwa basi atakuwa anahujumiwa na Nyerere kwa kuwa yeye ndiye aliyetaifisha mashamba ya huyo mkulima na kumfukuza nchini. Aende akatambike kwenye kaburi la Nyerere kule Mwitongo, wilayani Butiama.
 
NONSESE! Watu wangapi walifungiwa kijijini kwao na kwa makosa yepi? Lakini pia, ipi in a ubinadamu zaidi, kufungiwa kijijini kwako au kufunguliwa kesi isiyokuwa na dhamana (uozee magereza hata kama utakuja kushinda!) au hata kuondolewa uhai? Nadhani tusipojihadhari tunakaribia ukingoni!
Hakuna dhambi mbaya kama usaliti, Malcolm X alimiminiwa risasi 15 kifuani mwake, aliandikwa katika gazeti la kiislam kwamba amewasaliti waislam weusi wa Marekani.

Yuda alijitundika kambani baada ya kushindwa kuishinda nafsi yake mwenyewe iliyomsuta.

Ukifanya usaliti usitegemee kulindwa na huruma ya kibinadamu, tukiwagundua wasaliti wetu basi na wawe tayari kukabiliana na kile walichokifanya.

Nchi za kiafrika zinabakia kuwa masikini, sababu mojawapo ni usaliti wa muafrika mwenyewe.
 
Back
Top Bottom