Kabla ya kuwaondoa bungeni akina Halima Mdee, CHADEMA ni lazima kwanza ipokee ruzuku na ikubali kupeleka majina mengine 19

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,747
139,531
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ni Wasaidizi wake wanaelewa fika ni Kwanini Halima Mdee na wenzake wako bungeni ijapokuwa majina yao hayakupitishwa na CC ya chama hicho chenye makao makuu yake Ufipa St

Itoshe tu kusema CHADEMA pokeeni ruzuku

CHADEMA thibitisheni kuzijaza hizo nafasi zitakazoachwa wazi

Kisha, mtanishukuru siku moja!
 
Huu ni mtego hatari sana kwa Freeman na CDM...
Wakikubali wamekwisha....
Wakikataa wawe na Plan B.....otherwise....
Uzuri mambo haya yanazungumzika...
 
Hii umeitengeneza kichwani kwako bwashee au upo kwenye meza ya mazungumzo?

Hoja yako inaweza kuingia kwenye ile dhana ya kwamba kwenye mazungumzo ni sharti uwe tayari kupata kidogo na kupoteza kidogo.

Muhimu CCM wajue, kuendelea kukaa na kina Mdee bungeni wanazidi kuonesha walivyo wavunja sheria namba moja hapa Tanzania.
 
CDM ni chama cha kisiasa cha hiari, wanachama wake wamejiwekea sheria na miiko ambayo anayetaka kujiunga nacho ni muhimu azitekeleze kinyume chake itakua vurugu ,chama dola kipo vile kikitegemea zaidi dola to deal na watu kama covid 19 MPs, ndio maana police na Tiss heshima yao imepotea mno maana badala ya kulinda nchi wao wanalinda zaidi Lumumba,Mdee &others wamefukuzwa uanachama kwa vikao halali vya CDM, push back ya Mdee&others inatoka zaidi nje ya CDM kuliko within,hii ni very strange
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ni Wasaidizi wake wanaelewa fika ni Kwanini Halima Mdee na wenzake wako bungeni ijapokuwa majina yao hayakupitishwa na CC ya chama hicho chenye makao makuu yake Ufipa St

Itoshe tu kusema CHADEMA pokeeni ruzuku

CHADEMA thibitisheni kuzijaza hizo nafasi zitakazoachwa wazi

Kisha, mtanishukuru siku moja!
Chadema haitaishi kwa ruzuku bali Chadema inaishi kwa sababu iko kwenye mioyo ya wanachama wake
 
Mada hii nashindwa kujua kichwa chake kiko wapi achilia mbali miguu yake. Mbona tunachoshana wandugu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom