Kabla ya kupelekana chaka zaidi ufafanuzi kuhusu binti mzazi kusoma

Rwaz

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,957
3,301
Naona joto la kusoma kwa bint mzazi limepanda mno hasa mitandaoni. Inawezekana ni kwa sabab za kisiasa au ni ufafanuz hafifu toka kwa wahusika. Kias kwamba kuna wengine wanatuaminisha serkal imezuia anayebeba mimba KUDIRIKI kusoma zaid ya hapo. Madhara ya mal-information kwa sasa ni makubwa mno.

Hii ni kwa sabab suala limebebewa bango kama vile ni sera mpya ndo imetungwa. Naomba ufafanuz kuhusu haya toka kwa mwerevu

1. Je, kabla ya sera mpya utaratib ulikuwaje?

2. Je, tunachotofautiana ni mwanafunz mwenye mtoto kuwa darasan na wenzake akiwa na mtoto au hata kama mtoto haonekan eneo la shule?

3. Je, tunatofautiana kuwa mtoto akishazaa serkali inamtoa mazma kwenye mfumo wake wa elim wa shule zake kama zamam ,isipokuwa chuo hata kama hana ratiba za kunyonyesha? Au tunagombania serkali kuanza kugharamia usomaj wa wazaz hao na katika shule za serkali walimo wenzao!

4. Je tunatoafautiana kuwa sera mpya ya kuwaendeleza waliobeba mimba kwa kuwapa elim ya kujitegemea kama kushona na kufuga ni sera ya kuwafanya wawe na mwerekeo wa kimaskin?

Hitimisho: ukiachilia mbali suala la fedha inaweza kutumika vibaya, ambapo baada ya uchaguz hofu hiyo inaisha, busara zangu za kiafrica zinaniambia sera ya serkali iwe kuwa na madarasa yenye mitaala ile ile ya primary au sekondary kwa wanaopata mimba au wanafunz wazaz, maadam atakayefaulu ataingia tena mfumo ule ule chuo kama alokuwa nao.

Maana utaratib wa siku zote wa ukibeba mimba kajijue ni mbaya kuliko hata huu tunaopinga kwa kuvua nguo.
 
Vijana wetu walio wasikivu ambao hawafanyi ngono zembe na kuzingatia masomo kwa wingi wao tunaangaika nao kuwawezesha wapate elimu bora alafu tuwaache twende kujitwisha zigo la wanafunzi wapenda ngono zembe wenye watoto ambao kwa kuwa mzazi tu anawajibika kunyonyesha na kukaa na mwanae si chini ya miaka miwili atawezaje huyu mzazi kuchangamana na wototo wetu? Hivi watu siku hizi wamekuwa mapunguani au vibaraka wa mabeberu wameongeza watu kwenye malipo (payroll) kutaka kuangamiza elimu ya vijana wetu? Za kuambiwa changanya na zako!
 
Binafsi naona watu wamebebwa na upepo wa kisiasa zaidi! Serikali haijawah kusema itamtoa kwenye mfumo mazima isipokuwa kuchangamana na watoto itakuwa mbaya zaidi kwa wale ambao hawajashika mimba.

Wazazi wanaweza kujiendeleza private kama utaratibu ulivyo huko nyuma na hatimae wanaweza kuingia mpaka vyuo vya serikali kama kawaida, pia wanaweza kujipatia elimu ya ufundi kama VETA etc wala serikali haijakataza, lakini mtoto wa darasa la sita kapata mimba alafu akishajifungua arudi shule tena aingie standard vi aendelee na masomo! The end of day standard vii itakuwa wahitimu wajawazito watakuwa 90%.

Jambo hili likipita elimu yetu tutaizika kabisa.
 
Programme ya QT mbona ipo jamani Serikali yetu ina utaratibu mzuri sana sema wanasiasa wajinga ndio wanapototosha kuna programme ya QT yaani unasoma Elimu ya Sekondari kwa miaka miwili hata memkwa yaani Elimu ya watu wazima mwanafunzi mwenye mtoto hawezi tena kuitwa mtoto anaitwa mama mzazi yaani mtu mzima hafu watu lazima wajue kuwa hatuwezi kuwa na formal Education wote
 
kiliboy kufanya zinaa na under 18 kisheria umembaka hatakama mulikubaliana na ndiyo maana adhabu yake jela mvua 30! Na kama mwanafunzi unikute jaji mwenyewe mimi nakupiga 55 shubamiti! Then mtoto wa kike ataendelea na QT na baadhi ya private zipo zinapokea aina ya watu wa type yake ila akichemka kabisa VETA hipo na imejengwa na Serikali.
 
Mimi binafsi, mwanangu wa kike akipata mimba na bado hajamaliza shule... siku hyo ndio itakuwa mwisho wa kumuhudumia kama mwanafunzi...(labda awe amebakwa)...

Kwa maana mpka kupata mimba, means kazamilia na kashakuwa mtu mzima...inabidi atafute ela mwenyewe ajisomesha, kwangu atakuwa nishamtoa.. siwez kusomesha mama na mtoto..

Tuacheni siasa, twende kwenye uhalisia... kama wewe mwanao kapata mimba, utachukua hatua gani, kwenye elimu yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani ilani ya CCM 2015-2020 inasemaje kuhusu watoto wa kike. Siwalituaidi wakijifungua watarudi shule sasa sijui ntawaambia nini mimi
 
Tatizo kubwa la watanzania hatuangalii tulipo jikwaa tunaangalia tulipo dondokea.sheria ya kifungo kwa aliyemtia mimba mwanafunzi anafungwa miaka 30.hili ndio tatizo kubwa ila watu hawalijui,hapo wanafunzi wakike wanajiachia,wanafanya watakalo na hawaogopi kwakuwa sheria haija wagusa na sasa wanata taka kuwapa jeuri zaidi kuwa hata nikipata mimba nitaendelea na shule.suluhisho;kwa mimi maoni yangu sheria iwe hivi (1)kama mwanafuzi wa kike amepata mimba kwa kubakwa,hapo aliye mtia mimba atawajibika kwenda jela miaka 30.na familia ya mtia mimba itawajibika kwenye malezi ya mama na mtoto na mwanafunzi atafanyiwa mpango wa kuludi shule. (1:2)kama mwanafunzi hakubakwa(inamaana kafanya kwa lidhaa yake/kapenda)basi wote wawili kwenda jela miaka 30.hii itasaidi kidogo maana vitoto vya siku hizi vinajiachia sana yaani hata heshima hawana wanajiona mpo sawa.etikisa kalala namtu hata wewe mwenyewe kakuzid umri..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Mama mmoja (Mtu mzima sasa) anasimulia alipata ujauzito akiwa form 2, akafukuzwa shule na kurudi nyumbani, wazazi wake wakamwambia kwa kuwa umechagua kuzaa kaa ujifungue ulee mwanao, sentesi hiyo aliichukulia nyepesi, ukafika muda wa kujifungua kazi ikaanzia hapo, kulea.
Kwa kuwa alikuwa mdogo kiumri hata umbo,wazazi walichohakikisha ni afya ya Mama na Mtoto iko sawa lakini kulea ikabaki kazi yake mzazi, usumbufu wote wa watoto wachanga aliubeba, ikafika mahali akakumbuka Shule, akakumbuka maonyo ya wazazi wake aliyopewa mwishowe akahamishia hasira kwa mzazi mwenzake,
akachukia wanaume ,akaomba radhi kwa wazazi wake nao wakamsisitizia tulisha kusamehe ila ulee mtoto wako uliekuwa unamhitaji!
Kufupisha ni kwamba Mama huyu alijiunga na shule binafsi baada kufaulu usaili na alijiendeleza hadi Chuo kikuu, sasa ni mmoja wa wahandisi wakubwa tu, alijaliwa kupata watoto 2 wa kiume, mmoja ni Daktari na mwingine ni Mhandisi wa maji,
Kwa hiyo Mfumo Rasmi wa Elimu haujazuiwa kwa wajawazito waliokwisha jifungua kutopata Elimu au kujiendeleza ni upotoshaji tu wa Waganga njaa kama zitto kuaminisha watu uongo kwa maslahi binafsi.
Binafsi naona watu wamebebwa na upepo wa kisiasa zaidi! Serikali haijawah kusema itamtoa kwenye mfumo mazima isipokuwa kuchangamana na watoto itakuwa mbaya zaidi kwa wale ambao hawajashika mimba.

Wazazi wanaweza kujiendeleza private kama utaratibu ulivyo huko nyuma na hatimae wanaweza kuingia mpaka vyuo vya serikali kama kawaida, pia wanaweza kujipatia elimu ya ufundi kama VETA etc wala serikali haijakataza, lakini mtoto wa darasa la sita kapata mimba alafu akishajifungua arudi shule tena aingie standard vi aendelee na masomo! The end of day standard vii itakuwa wahitimu wajawazito watakuwa 90%.

Jambo hili likipita elimu yetu tutaizika kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Mama mmoja (Mtu mzima sasa) anasimulia alipata ujauzito akiwa form 2, akafukuzwa shule na kurudi nyumbani, wazazi wake wakamwambia kwa kuwa umechagua kuzaa kaa ujifungue ulee mwanao, sentesi hiyo aliichukulia nyepesi, ukafika muda wa kujifungua kazi ikaanzia hapo, kulea.
Kwa kuwa alikuwa mdogo kiumri hata umbo,wazazi walichohakikisha ni afya ya Mama na Mtoto iko sawa lakini kulea ikabaki kazi yake mzazi, usumbufu wote wa watoto wachanga aliubeba, ikafika mahali akakumbuka Shule, akakumbuka maonyo ya wazazi wake aliyopewa mwishowe akahamishia hasira kwa mzazi mwenzake,
akachukia wanaume ,akaomba radhi kwa wazazi wake nao wakamsisitizia tulisha kusamehe ila ulee mtoto wako uliekuwa unamhitaji!
Kufupisha ni kwamba Mama huyu alijiunga na shule binafsi baada kufaulu usaili na alijiendeleza hadi Chuo kikuu, sasa ni mmoja wa wahandisi wakubwa tu, alijaliwa kupata watoto 2 wa kiume, mmoja ni Daktari na mwingine ni Mhandisi wa maji,
Kwa hiyo Mfumo Rasmi wa Elimu haujazuiwa kwa wajawazito waliokwisha jifungua kutopata Elimu au kujiendeleza ni upotoshaji tu wa Waganga njaa kama zitto kuaminisha watu uongo kwa maslahi binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfumo wa kujiendeleza kielimu kwa wazazi tangu zamani hadi sasa hupo na wengi wameutumia na kutoka kimaisha. Tunachopinga ni kuchanganya wanafunzi na wazazi kusoma shule za msingi na secondary darasani pamoja
 
nAOMBA KUULIZA PIA:
1: Mzazi Mwanafunzi ninaruhusiwa kumzalisha tena? Kwa mtazamo wangu namuona kama si Mwanafunzi maana anajua utamu wote.
2;Kwa maana ya umri atakuwa chini ya umri lakini sio mwanafunzi rasmi. Je, nitashitakiwa kumlala ?
3: Ataangukia category gani?
a) Mwanafunzi?
b) Mzazi
c) Mkubwa mwenzetu( wakiitwa wazazi kwenye mkutano wa kijiji tutaenda wote.
 
Hipo siku watakuja kusema ata wale wanaopata Division 0 nao waendelee A-Level cos nao wanahitaji second chance! Sijui tumelogwa na nani watz!
Hili mbona lipo sana tu, na limewekwa na mfumo wa elimu, kimsingi mwanafunzi hakutakiwa kupanda darasa bila kufikisha alama flani. Iwepo pass mark kwa kila darasa, badala ya la nne, Saba, form 2? na 4.
 
Naomba tuhubiri tabia njema kwa binti zetu na kujitunza huku tukiwaonesha mifano hai ya madhara ya kuingia kwenye mahusiano.

Ikitokea kwa Hali yoyote ile binti akapata ujauzito akiwa bado ni Mwanafunzi, utaratibu usio rasmi wa elimu uendelee kutumika mpaka hapo atakapofaulu kuingia tena kwenye mfumo rasmi (Vyuo) kwani huko wapo wanaoenda wakitokea kwenye maisha ya utu uzima.

Hapa naona kama tunagombea fito wakati tunajenga Banda moja.

Kauli za Nani AUWAWE, hiyo ni Jinai kama Jinai aliyofanya kijana wa Singida kusema atamuua Rais Magufuli na akahukumiwa kifungo jela.

Wabunge waliotoa kauli za kuuawa kwa ZZK, Sheria iliyotumika kumfunga kijana wa Singida, itumike pia kwao.
 
Vijana wetu walio wasikivu ambao hawafanyi ngono zembe na kuzingatia masomo kwa wingi wao tunaangaika nao kuwawezesha wapate elimu bora alafu tuwaache twende kujitwisha zigo la wanafunzi wapenda ngono zembe wenye watoto ambao kwa kuwa mzazi tu anawajibika kunyonyesha na kukaa na mwanae si chini ya miaka miwili atawezaje huyu mzazi kuchangamana na wototo wetu? Hivi watu siku hizi wamekuwa mapunguani au vibaraka wa mabeberu wameongeza watu kwenye malipo (payroll) kutaka kuangamiza elimu ya vijana wetu? Za kuambiwa changanya na zako!
Kwa mchango wako huo nimechukua pointi hizi kutoka kwako!
1.shida ni ngono zembe,ila kama wanatumia kondomu au wanatumia vidonge vya majira basi hawa ni safi kabisa na wanastahili kupata elimu rasmi!Ila wale ambao hawatumii kondomu au vidonge na wakashika mimba basi ndio shauri yao!
Hapa unashauri watoto wasifanye ngono zembe,bali wajikinge dhidi ya mimba wakati wa tendo la kungonoka!

2:Ulishafanya utafiti na kujua madhara ya mtoto aliyejifungua akisoma na mtoto ambaye hajajifungua anamuathiri vipi?

Kwa mwendo huu sioni ajabu siku mkisema watoto wapimwe ukimwi ili wenye nao wasiruhusiwe kusoma na ambao hawana!

Si kila jambo ni kuiga kutoka kwa Jiwe,wenzetu kenya na Uganda wanawap fursa sawa watoto wanaopata ujauzito,cha ajabu pamoja na hilo wametuacha mbali sana kwenye sekta ya elimu!Kama ingekuwa kuna madhara hayo unayohofia basi yangeonekana huko!

Suala lingine hapa,CCM walikaa chini na kuja na ilani itakayowapa watoto watakaojifungua fursa ya kuendelea na masomo,hamkupinga sera hiyo kwenye ilani ya uchaguzi aliyotembea nayo JPM nchi nzima kuinadi!
Amekuja kuigeuka ilani yake mwenyewe na kusema kwenye utawala wake hilo haliwezekani,basi CCM wooote wameunga mkono,mtu unajiuliza so ni hawa hawa waliotunga ilani?Iweje leo wafeuke mawazo yao?
Shida hapa ni nidhamu ya woga kwa JPM,inawafanya watu mnajitoa ufahamu wenu!

3.Kodi ni zetu sote wananchi na tunachangia kwa namna tofauti,so kusema mnabebeshwa zigo la kusomesha waliojifungua sio sahihi maana kodi tunachangia wananchi wote bila kujali huyu mtoto wake amejifungua au la!
 
Mimi binafsi, mwanangu wa kike akipata mimba na bado hajamaliza shule... siku hyo ndio itakuwa mwisho wa kumuhudumia kama mwanafunzi...(labda awe amebakwa)...

Kwa maana mpka kupata mimba, means kazamilia na kashakuwa mtu mzima...inabidi atafute ela mwenyewe ajisomesha, kwangu atakuwa nishamtoa.. siwez kusomesha mama na mtoto..

Tuacheni siasa, twende kwenye uhalisia... kama wewe mwanao kapata mimba, utachukua hatua gani, kwenye elimu yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Sheria za nchi yetu,mtoto chini ya miaka 18 akipata ujauzito maana yake amebakwa!Hata kama amefungua mapaja yake kwa hiari,mbele ya sheria inaonekana ni mtoto ambaye hajui alitendalo!
Mnyime fursa mwanao akipata ujauzito,wengine ikitokea hiyo bahati mbaya tutasomesha!Sitapenda kuona namkatia tamaa mbegu niliyoileta duniani!
 
Back
Top Bottom