Kabla ya kuoa au kuolewa, Utajuaje mchumba wako ni Mchawi au mshirikina?

Wako hivi
. Anapenda sana kusema fulani ananikwamisha ni mchawi
. Fulani ukikaa naye hufanikiwi
. Fulani anatumia chuma ulete
. Kuna watu hawapendi nifanikiwe wananikwamisha kwa uchawi.
. Kila limtokealo anasema sio la kawaida kuna jambo
. Mara nyingi anaenda kumuona mtaalamu
. Mara usitupe nywele maeneo ya wazi, ukiwaki weka mchanga
. Mara hili jambo ngoja niende home wakaliangalie hahaha
. Anapenda kuigiza anaumwa vitu ambavyo huwezi kuvielezea
. Ana mashart fulani yakutia mashaka
Kweli kabisa
 
Bibilia na vitabu vingine vya dini lazima ujuwe kufitafisiri, ndiyo maana kuna bible studies. Bible inasema we shall not kill, tusiuwe, wewe unasema wazee wanauwawa ni sawa. Zeruzeru wanauwawa bila ya sababu kwaajiri ya imani za kijinga. Kuna watu wanaitafisiri bibilia kwa kujitajirisha wenyewe. Kama story ya Gwajima kumufufuwa mtu aliyekufa Huu ni wizi sawa ya kujitajirisha muchawi. Mimi siamini kwasababu sijaona muchawi mwenye power yeyote, nitaamini ukinionyesha. Hakuna mtu yeyote mwenye hiyo power ya uchawi unayoisema, lakini kuna uonevu wa kikatili wa kuwauwa watu ambao hawajiwezi kama wazee kuwasingizia wachawi. Maana ya uchawi ni nini? Ukiangalia Tanzania sehemu ambazo zinaamini uchawi Hakuna maendeleo, watu ni masikini sana. Hii ndiyo shida kubwa sana Tanzania Kwani mpaka Viongozi wetu wanapiga suit na kuamini uchawi. Wameachilia haswa Wakati wa `Kikwete zeruzeru wengi kupoteza maisha bila ya kuwachukulia hatuwa wauwaji kwasababu ya kuamini uchawi. Naililia nchi yangu Tanzania kwa kukosa elimu ya kutosha, Na hili ndiyo tatizo kubwa hapa tusitafute muchawi. Ukiangalia sehemu za Tanzania watu hawaamini uchawi kuna maendeleo makubwa. Kama kuna uchawi prove to me. Hayo ni mawazo ya kipumbavu yanairufisha Afrika Nyuma. Kama kuna uchawi basi tuutumie kwa maendeleo, yako wapi? Jamani turudi shuleni na tujiekimishe kwa kusoma vitabu.

Nazani kama tunataka kwenda Sawa declare kwanza Kwamba Wewe ni mwamini Au siyo mwamini , na Kama ni mwamini useme unaamini ktk nini?! Maana huamini uchawi upo inamaana pia huamini uwepo wa Shetani ! Ila kuna baadhi ya points nakubaliana na Wewe ikiwepo ukosefu wa elimu , na fahamu kuwa tunaposema uchawi upo hatuna maana kuwa tunaifurahia kuwepo Kwa uchawi! Wachawi wako Kwenye shortlist ya makundi ya watenda dhambi ambao hawata urithi ufalme wa Mungu ,wenyewe ni wa Jehanam iwakayo moto! Unasema uchawi haupo ushawahi sikia Mtu anaumwa hana Raha akienda hospital ndani na nje ya nchi na kufanya vipimo ugonjwa haionekani kabisa? Hadi daktari anamwandikia prescription ya kwenda Kwenye maombi ! Una umri gani, umezaliwa na kukulia wapi? Ulaya? Kama uko bongo basi nakushauri endelea na hiyo Imani yako ni nzuri pia Ila pia omba Siku zote usiingie majaribuni! Kuna vijiji huko wachawi kazi Yao kufuatilia wale wanaoongoza Kwa kufaulu darasani wanatumiwa majini na kuwavuruga AKILI kisha wanakuwa wehu sasa hapo utasema hakuna uchawi?!
 
Kuna hizi mbinu mbili za msingi sana
1. Chukua ungo weka mwiko ndani yake kisha viweke uvunguni bila ya yeye kujua. Hii itamfanya aongee hovyo usiku kucha
2. Choma chumvi kwenye kona ya nyumba ya kulia bila yeye kujua. Ila kuwa makini maana kama yeye ni mchawi unaweza kuona vitu vya ajabu sana
Aiseee
 
Naililia Tanzania kwa mawazo yetu na imani zetu za kijinga ZINAZOTURUDISHA taifa hili nyuma. Kwa nchi zilizoendelea muchawi ni scientist. mutu ambaye utaenda kwakwe unaumwa atakupima na kujuwa kinachokusumbuwa. Mtu ambaye anaweza kukulaza kwa masaa NUSU KAPUTI, na KUKUPATIA kama ya upasuaji bila ya kusikia maumivu na ukaamuka salama na HUYU anaitwa daktari. Hakuna uchawi, ni wengi wetu kukosa elimu ndiyo tumekuwa na mawazo ya kijinga. Kungekuwa kuna uchawi Afrika tungetajirika, hiyo ni power sawa na kuwa na bomb la nukilia. Hizo nguvu tunazoamini za uchawi Hakuna lolote ni upungufu wa akili. . Hakuna uchawi wowote ni ujinga mtupu na kurudisha nchi nyuma. Binaadamu akizaliwa, lazima apambane na changamoto. Kuna wakati utafurahi, kuna wakati utalia, kunawakati utapata shida na kunawati utapata raha n.k. That is part of life. UKWELI HAKUNA UCHAWI FULL STOP. USIPOTEZE WAKATI WA KUTAFUTA JIBU. OWA MWANAMKE MWENYE ELIMU, SIO LAZIMA ZA KUSOMA ZA KUELEWA, LAKINI NA WEWE USIWE NA IMANI ZA KIJINGA.
posti ya kitoto kabisa kuwahi kuiona!
 
Kuna hizi mbinu mbili za msingi sana
1. Chukua ungo weka mwiko ndani yake kisha viweke uvunguni bila ya yeye kujua. Hii itamfanya aongee hovyo usiku kucha
2. Choma chumvi kwenye kona ya nyumba ya kulia bila yeye kujua. Ila kuwa makini maana kama yeye ni mchawi unaweza kuona vitu vya ajabu sana
Tahadhari Ndugu;hizi njia km mtu awezi au hajawahi ona mchawi asithubutu maana unaweza kuhama nyumba
 
Kuna hizi mbinu mbili za msingi sana
1. Chukua ungo weka mwiko ndani yake kisha viweke uvunguni bila ya yeye kujua. Hii itamfanya aongee hovyo usiku kucha
2. Choma chumvi kwenye kona ya nyumba ya kulia bila yeye kujua. Ila kuwa makini maana kama yeye ni mchawi unaweza kuona vitu vya ajabu sana
Nitajaribu hii...
 
Ndio maana wazazi wetu zamani, ukitaka kuolewa au kuoa unasema ukoo na sehemu waliyotokea anatumwa mtu kwenda kuchunguza mambo kama haya. .

Ila siku hz umjini mwingi, tunabebana tu, tushatundikana na mimba
 
posti ya kitoto kabisa kuwahi kuiona!

Utaiona wapi na wengi Tanzania tunaamini uchawi? Tunaishi kwenye Giza Wakati mataifa mengine yanaendelea. Uchawi tunao basi ututajirishe Kwani ingekuwa kweli hiyo ni power. Mawazo haya ni ukosefu wa elimu tu. Tutaedeleaje ikiwa Viongozi wanaamini uchawi badala ya elimu. Naionea huruma nchi yangu kwa kuwa gizani.
 
Kuna hizi mbinu mbili za msingi sana
1. Chukua ungo weka mwiko ndani yake kisha viweke uvunguni bila ya yeye kujua. Hii itamfanya aongee hovyo usiku kucha
2. Choma chumvi kwenye kona ya nyumba ya kulia bila yeye kujua. Ila kuwa makini maana kama yeye ni mchawi unaweza kuona vitu vya ajabu sana
 
Nazani kama tunataka kwenda Sawa declare kwanza Kwamba Wewe ni mwamini Au siyo mwamini , na Kama ni mwamini useme unaamini ktk nini?! Maana huamini uchawi upo inamaana pia huamini uwepo wa Shetani ! Ila kuna baadhi ya points nakubaliana na Wewe ikiwepo ukosefu wa elimu , na fahamu kuwa tunaposema uchawi upo hatuna maana kuwa tunaifurahia kuwepo Kwa uchawi! Wachawi wako Kwenye shortlist ya makundi ya watenda dhambi ambao hawata urithi ufalme wa Mungu ,wenyewe ni wa Jehanam iwakayo moto! Unasema uchawi haupo ushawahi sikia Mtu anaumwa hana Raha akienda hospital ndani na nje ya nchi na kufanya vipimo ugonjwa haionekani kabisa? Hadi daktari anamwandikia prescription ya kwenda Kwenye maombi ! Una umri gani, umezaliwa na kukulia wapi? Ulaya? Kama uko bongo basi nakushauri endelea na hiyo Imani yako ni nzuri pia Ila pia omba Siku zote usiingie majaribuni! Kuna vijiji huko wachawi kazi Yao kufuatilia wale wanaoongoza Kwa kufaulu darasani wanatumiwa majini na kuwavuruga AKILI kisha wanakuwa wehu sasa hapo utasema hakuna uchawi?!

Hata sijuwi kwa nini najadili uchawi, ni kitu cha kijinga sana. Imani zetu zinaturudisha nyuma sana. Majini, Nina miaka karibu 70 hapa duniani sijaona hayo majini mnayoyasema. Watu mnaowasema vijijini wamejawa na shida kubwa za maisha. Wazee wanauwawa bure kwa macho yao kuwa mekundu. Tanzania ni nchi mojawapo duniani ya ukatili kwa wazee, na Hii yote kwaajiri ya imani zetu za kijinga. Tunadanganyika kwa urahisi. Sio tu uchawi, hata kwa dini mpya zilizoingia Afrika nzima, mchungaji kusema anaweza kumufufua mtu aliyekufa, tunaamini na pesa zetu tunampa muchungaji, Hii yote ni ukosefu wa elimu ya kufikilia, Ndiyo maana kumudanganya mjinga ni rahisi. Tunauwa wazee wetu, kwa kuwa wana macho mekundu, mzee gani Afrika ambaye hana macho mekundu, shida nyingi zinazowakabili wazee, haswa vijijini, vumbi na ukosefu wa matunzo. Watu wengi wanapata vichaa kwaajiri ya shida nyingi zinaowakabili. Depression, hatujui Huu ugonjwa, wala hatuna masaikolojia nchini, ni ugonjwa unawapata watu wengi, ikiwa pamoja na wanafunzi wenye maisha magumu, wengi hawana hata watu wakusikiliza shida zao, kacha zetu, na Hii yote ukosefu wa elimu, mtoto tukishamukabidhi kwa Mwalim, Mwalim anabeba majukumu yote. Mtoto anapata depression. Ugonjwa huu ukitambuliwa mapema unatibika. Wazungu wanaita depression sisi tunaita kichaa ati amelogwa. Kwa ukosefu wa elimu bora na kukosa wataalamu nchini tunakimbilia njia rahisi ya uchawi. Kama kweli tuna power ya uchawi kwa nini tusiwaloge hawa wazungu wanaokuja kutuvurugua na kutudanganya uchumi wetu na Wakati tuna power kubwa ya uchawi. Hawa wachawi wako wapi Jamani, tunaibiwa makinikia yetu. Kwa nini tusipeleke power Hii ya uchawi kwenye mahakama za ulaya tunashindwa kesi kila Wakati tunalipa mabilioni. Wako wapi hawa wachawi wenye nguvu wawaloge hawa wahalifu. Hakuna, the more we believe nguvu za Giza tunazidi kurudu nyuma. Namuonea huruma Rais Magufuli ni shida kubwa sana kuongoza watu wenye upungufu wa elimu. Tunahitaji kuhama kwenye mawazo haya ya kijinga na kutambuwa binaadamu anaubwa lazima apambane na changamoto mbalimbali bila ya kuamini nani kamuloga. Wenye mawazo haya wengi hawaendelei. Huwezi kuendelea kama umaejaa hofu. Mimi ni mkristu, na sio mkristo wa wale wanaojiita wameokoka, ni mkiristo naamini kufanya mazuri, vitendo vyangu na sio kushinda kanisani. Nipata bahati kulelewa na wazazi waliokuwa na mawazo ya elimu, sio tu ya kusoma bali ya kufikilia. Ni vigumu manga ama wachungaji kunishauri kuwa wana uwezo mkubwa wa kuibadilisha maisha yangu kwa malipo na kukusanya pesa kwa masikini na kujinunulia magali makubwa, kwa mawazo yangu hawa hawana tofauti na watu wanaojiita wachawi, ni waongo, wanadanganya na wanawarudisha watu nyuma na kuwaongezea matatizo.
 
Utaiona wapi na wengi Tanzania tunaamini uchawi? Tunaishi kwenye Giza Wakati mataifa mengine yanaendelea. Uchawi tunao basi ututajirishe Kwani ingekuwa kweli hiyo ni power. Mawazo haya ni ukosefu wa elimu tu. Tutaedeleaje ikiwa Viongozi wanaamini uchawi badala ya elimu. Naionea huruma nchi yangu kwa kuwa gizani.
hata u freemason wa kinA bush ni uchawi pia
 
Utamjua kwa matendo yake tu ya utata,tena kama unasali sana lazima mgombane maana giza huwaga halipatani na nuru kamwe.
Wachawi ndio wanaongoza kwenda kanisani na misikitini. Na ndio walioshika dini sijui unalijua hili?
 
Back
Top Bottom