Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Tunaweza tukawa tunataka ku-push agenda tukiamini tunayetaka kumfikishia agenda hiyo ni mgeni na anahitaji vikao vyakumpitisha kwenye kile tunachokita. Naomba niwaambie we are wrong, hakuna sababu ya kikao kumfikishia ujumbe Mhe. Rais kuhusu katiba. Yeye anafahamu mwanzo mwisho wa mchakato uliopita kwa sababu alikuwa kiongozi Na. 2 kwenye Bunge la Katiba.
Nadhani tuamini kwamba kama mchakato wa awali ulifia mikononi mwake na Mzee Sita, jukumu letu la Kwanza nikumuuliza mama sababu zilizopelekea kufa kwa mchakato ule.
Tunapaswa kuhoji mchakato ule Kwanza kwa sababu, yawezekana sababu zilizopelekea kufa kwa mchakato wa awali zina nguvu Hadi Sasa. Na Kama Zina nguvu na zilimpelekea kukubaliana na kifo cha mchakato wa Katiba ya Warioba basi yeye siyo mtu sahihi kumpelekea agenda ya Katiba. Tusubiri mtu anayeweza kuamini na kukubaliana kwamba sababu za kufa kwa mcahakato wa awali hazina mashiko.
Hakuna mtu anayetaka kuendelea kutawala atakayetengeneza mazingira Bora ya watawaliwa. Atawaminya, ila tofayti yakuwaminya itatofautiana. Mama anatuminya kama wengine walivyotuminya isipokuwa yeye anatuminya kwa kisingizio cha kuboresha mfumo.
Mnaodai katiba hojini kuhusu ulipoishia mchakato wa awali. Watafteni akina Warioba mapema mzungumze nao ili jamii ielewe tulikwama wapi. Msipotumia fursa yakukwapua malighafi vichwani mwa wazee mtashangaa muda unaisha na wanaondoka na Siri ya kukwama kwa Katiba.
Mhe. Rais awe wa mwisho mkiwa mnajipanga kwenda kuzipangua hoja zilizokwamisha mchakato wa awali.