Ahsante kaka mkubwa.Nianze na maandiko matakatifu Yohana 8:32 Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Watanzania wenzangu tuna tatizo kubwa sana katika nchi yetu, ambalo sasa limekuwa ugonjwa sugu, Woga unaozaa dhambi ya UNAFIKI. Kiwango hiki cha unafiki tulichofikia ni kibaya sana ambacho kinasababisha kuambiwa ole wenu ninyi watanzania mnaopindisha kweli kwa kumwogopa JPM. Hii ni laana kufikia kiwango hiki, tunajua wazi kuwa utawala wa awamu ya tano unaongoza nchi kwa kuvunja katiba na sheria za nchi.
Kuna watu wengi wanaosema kuwa JPM anachapa kazi na kutetea raslimali za nchi, hii siyo sababu ya kuvunja sheria na kukandamiza uhuru wa watu kutoa mawazo na vyama kufanya matakwa yao
Sasa tumwambie JPM ukweli.
1-Hatawali nchi kwa kufutuata katiba na sheria za nchi. Ni kifungu gani cha katiba kinachozuia vyama vya siasa visifanye mikutano ya hadhara hadi 2020?
2-Anatumia theocracy kwenye nchi ambayo imekubaliana na mfumo wa democracy hii ni hatari anataka akiamua kitu watu wote waseme ndio. Anayetakiwa atawale kwa theocracy ni Mungu peke yake.
3-Anapandikiza chuki kati ya watanzania, kati ya vyama vya siasa, kati ya makabila na pia kati ya kanda na kanda. Watu wanajitahidi kutetea lakini ukweli wanaujua kuwa nchi inakoelekea siko
4-Amekuwa mara kwa mara akitamka maneno ya kuchochea vyombo vya dola kutumia nguvu dhidi ya raia wasio na silaha, na huku akijizungushia ulinzi mkali kama walivyo marais waovu duniani.
5-Amekuwa akiwashambulia wale wanaopinga hadharani hata kuwaita majina mabaya kama wasaliti, wapinga maendeleo na wasiokuwa wazalendo, huku akijihami kwa kuwakamata wale wote wanakusudia kumjibu.
6-Amekuwa na tabia ya wafalme wenye kiburi kama Nebukadneza, Farao na Herode waliotaka kusifiwa tu, na kuwatesa na kuwaua wale wote walijitahidi kuwakosoa.
7-Anawalazimisha watu waamini kuwa yeye tu ndiye mwenye uwezo na mzalendo wa kweli katika nchi ya Tanzania.
8-Anafikiri neno lake ndio katiba na sheria halali ya kuongoza nchi.
Lazima Aambiwe ukweli kwanza kabla ya kukimbilia kumrarua Lissu
Sent using Jamii Forums mobile app