Kabla ya kumjadili Kenani Kihongosi turejee kisa cha Hayati Samwel Sita na harakati zake pale UDSM

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau!

Juzi watu walikuwa wanapiga kelele kitendo cha mkuu wa wilaya Kenani Kihongosi kutandika viboko wale wahuni walioiba madawati ya shule.

Binafsi nikawa na cheka tu maana akanikumbusha kisa cha Hayati Mwalimu JK Nyerere na mzee wetu spika wa mstaafu Hayati Samweli Sita (Mungu awalaze pema peponi).

Kifupi mimi sikuwapo kipindi hicho ila wakati nipo pale UDSM miaka ya nyuma nafanya shahada yangu ya kwanza jamaa yangu mmoja kuna siku tulikuwa tunapita pale Fuculty of Law au kwa jina jingine Kitivo cha sheria a.k.a "kitivo" wakati tunatembea alinishika bega na kunionyesha sehemu ambayo inasadikika Mwl aliamtandika mzee Hayati Samwel Sitta viboko kipindi hicho mzee Sitta alikuwa mwanafunzi wa chuo pale UDSM, na kisa kilikuwa kama hivi.

Sitta amesoma shahada yake kwa miaka 7 kwa sababu mwaka 1966, wakati yuko mwaka wa pili na akiwa kiongozi wa wanafunzi UDSM, wanafunzi waligoma na kuandamana kupinga kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kukatwa mishahara yao baada ya JKT. Hoja ya wanafunzi ilikuwa na mantiki kubwa, kwamba mbona vigogo wa serikali na wanasiasa wanalipwa mishahara minono na marupurupu makubwa?

Baada ya shinikizo hilo la wanafunzi Mwalimu Julius Nyerere alikubali kupunguza mshahara wake wa Sh4,000 bila kodi akaagiza pia mishahara ya mawaziri ipunguzwe kwa asilimia mbili. Miezi miwili baadaye akatangaza Azimio la Arusha (Februari 5, 1967) kuyapa uzito malalamiko ya wanafunzi hao.

Watukutu wawili – Sitta na Wilfred Mwabulambo (sasa marehemu) na wengine kadhaa – waliojitia wazimu na kutetea kile walichokiita haki zao, (haki za wakulima na wafanyakazi), walimshutumu Mwalimu Nyerere kwa maneno makali wakidai “…ni heri wakati wa ukoloni kuliko utawala wa Mwalimu”.

Mwalimu Nyerere alikasirika na kuwafukuza chuo wanafunzi wote 400 kwa kile alichokiita “kwenda kufunzwa adabu majumbani mwao”. Miezi kumi baadaye, baada ya Nyerere kushawishiwa na hasira kutulia akaamua kuwarudisha chuoni wanafunzi 392. Viongozi wa mgomo; Sitta na wenzake 7 walitiliwa ngumu, hawakurejeshwa chuoni.

Busara za viongozi wa chuo zilifanya Mwalimu aliliwe zaidi na kuandikiwa barua mbili maalumu na chuo zenye Kumb. Na. C3/Sa.13 ya 2/3/1967 na C3/Ss.13 ya 9/07/1967. Mwalimu alikubali kilio hicho na kuwaruhusu vijana hao wanane warudi kwa sharti kwamba wale watukutu wawili (Sitta na Mwabulambo) watandikwe viboko na “Mwalimu Nyerere” mwenyewe. Hii ndiyo ilikuwa pona ya Sitta ambaye alirejea UDSM na kuendelea na masomo kwa miaka kadhaa hadi alipohitimu mwaka 1971.

Turudi kwenye mada yetu. Je, wanaomkosoa Kenani Kihongosi wanaijua hadithi hii? Je, hawa wahuni na wezi wa mali za umma hawakustahili viboko?
 
Wewe umehusisha vitu viwili tofauti. Wale akina Sita hawakufanya jinai bali ulionekana ni utovu wa nidhamu lakini hawa wa Kihongosi wamefanya jinai ambayo ni prosecutable. Ni wapi unaweza kumshitaki mtu anayekulalamikia kwamba hujamtendea haki? Akina Sita walikuwa wana malalaniko na waliyotendewa haikuwa haki pia kwani mwenye malalamiko husikilizwa na si kutandikwa.
 
Mgomo wa chuo kikuu DSM Chanzo cha Azimio la Arusha.

Hii story imepotoshwa sana.
Aliyeadhibiwa viboko na Mwalimu Nyerere hakuwa Samwel sitta.

Mwalimu aliumia sana na ule mgomo Baada ya kusoma Bango linalosema HERI UKOLONI KULIKO UHURU.

KWAHERI UDSM.

tafuta hiyo barua uisome
 
Ndio maana ya specialization unadhani nilikaa darasani miaka zaidi ya 30 kusomea kiswahili au literature km ww??,ndio nyinyi mtu akiongea kiingereza mnamuona msomi..???

Kwahiyo sijui tofauti ya kiingereza na usomi? Hatujui ww ni mbobezi wa nini, hapa tunaangalia ulichoandika na majigambo yako ya kilimbukeni.
 
Habari wadau..!
Juzi watu walikuwa wanapiga kelele kitendo cha mkuu wa wilaya Kenani Kihongosi kutandika viboko wale wahuni walioiba madawati ya shule.

Binafsi nikawa na cheka tu maana akanikumbusha kisa cha Hayati Mwalimu JK Nyerere na mzee wetu spika wa mstaafu Hayati Samweli Sita (Mungu awalaze pema peponi).

Kifupi mimi sikuwapo kipindi hicho ila wakati nipo pale UdSM miaka ya nyuma nafanya shahada yangu ya kwanza jamaa yangu mmoja kuna siku tulikuwa tunapita pale Fuculty of Law au kwa jina jingine Kitivo cha sheria a.k.a "kitivo" wakati tunatembea alinishika bega na kunionyesha sehemu ambayo inasadikika Mwl aliamtandika mzee Hayati Samwel Sitta viboko kipindi hicho mzee Sitta alikuwa mwanafunzi wa chuo pale UDSM, na kisa kilikuwa kama hivi.

-Sitta amesoma shahada yake kwa miaka 7 kwa sababu mwaka 1966, wakati yuko mwaka wa pili na akiwa kiongozi wa wanafunzi UDSM, wanafunzi waligoma na kuandamana kupinga kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kukatwa mishahara yao baada ya JKT. Hoja ya wanafunzi ilikuwa na mantiki kubwa, kwamba mbona vigogo wa serikali na wanasiasa wanalipwa mishahara minono na marupurupu makubwa?

Baada ya shinikizo hilo la wanafunzi Mwalimu Julius Nyerere alikubali kupunguza mshahara wake wa Sh4,000 bila kodi akaagiza pia mishahara ya mawaziri ipunguzwe kwa asilimia mbili. Miezi miwili baadaye akatangaza Azimio la Arusha (Februari 5, 1967) kuyapa uzito malalamiko ya wanafunzi hao.

Watukutu wawili – Sitta na Wilfred Mwabulambo (sasa marehemu) na wengine kadhaa – waliojitia wazimu na kutetea kile walichokiita haki zao, (haki za wakulima na wafanyakazi), walimshutumu Mwalimu Nyerere kwa maneno makali wakidai “…ni heri wakati wa ukoloni kuliko utawala wa Mwalimu”.

Mwalimu Nyerere alikasirika na kuwafukuza chuo wanafunzi wote 400 kwa kile alichokiita “kwenda kufunzwa adabu majumbani mwao”. Miezi kumi baadaye, baada ya Nyerere kushawishiwa na hasira kutulia akaamua kuwarudisha chuoni wanafunzi 392. Viongozi wa mgomo; Sitta na wenzake 7 walitiliwa ngumu, hawakurejeshwa chuoni.

Busara za viongozi wa chuo zilifanya Mwalimu aliliwe zaidi na kuandikiwa barua mbili maalumu na chuo zenye Kumb. Na. C3/Sa.13 ya 2/3/1967 na C3/Ss.13 ya 9/07/1967. Mwalimu alikubali kilio hicho na kuwaruhusu vijana hao wanane warudi kwa sharti kwamba wale watukutu wawili (Sitta na Mwabulambo) watandikwe viboko na “Mwalimu Nyerere” mwenyewe. Hii ndiyo ilikuwa pona ya Sitta ambaye alirejea UDSM na kuendelea na masomo kwa miaka kadhaa hadi alipohitimu mwaka 1971.

Turudi kwenye mada yetu je wanaomkosoa Kanani Kihongosi wanaijua adithi hii???Je hawa wahuni na wezi wa mali za umma hawakustahiri viboko?
Ndugu yangu unachanganya mambo hapa,
Kumpinga Mwalimu,na kugoma kwa wanafunzi wa chuo sio kosa la jinai,
Pili Mwalimu kuwatandika fimbo Sita na wenzie,ni matumizi mabaya ya madaraka pia,kwa vile alifsnya Mwalimu,haihalalishi hiyo adhabu,
Turudi kwa DC mpuuzi na mjinga kihongosi,Wale jamaa,wamefsnya kosa la jinai!inabidi wafikishwe mahakamani wapate haki yao,hata Hakimu akitoa adhabu ya viboko,anaetekeleza sio DC,na wala haitekelezwi hadharani,ule ni udhalilishaji.
Inaonekana wewe hiyo shahada yako Wala haikusaidii kutafakali,unalinganisha kipindi Cha Mwalimu 1960!na leo 2020!!
Mazingira ya 1960 ni tofauti sana na leo,bila kupeleka vijana JKT,unafikiri jeshi la akiba lingetoka wapi.
Unamkamata mwizi wa dawati,au kuku unamchapa viboko,Tena hadharani,lakini wezi wa Qnet,Mr KuKu,DECI,Richmond,Escrow!
Uliona wapi wanachapwa viboko hadharani,wanaperekwa mahakamani.
Jinai ni jinai tu,lazima uperekwe mahakamani,
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom