Kabla ya kufikiria harusi, weka haya akilini!

bf8852f5aa6c3b1693eb3a25bbe2c43f.jpg

WENGI wakiwaza kuhusu kufunga ndoa, mawazo yao huenda moja kwa moja kwenye namna sherehe ya harusi itakavyokuwa! Anataka gari kali la maharusi, ukumbi wa gharama, vyakula vya bei mbaya, wasanii maarufu wa kutumbuiza n.k.

Ni kweli ni vema kuifanya siku hiyo maalum na ya pekee maishani kuwa yenye kumbukumbu isiyofutika! Watu wanapenda kufanya sherehe kubwa ambayo itawafurahisha watu.

Katika kufanikisha hilo, huwa kunakuwa na kamati ya maandalizi ambayo ndiyo huratibu shughuli nzima. Katika kikao cha kwanza cha kuwaita wanakamati kuwaeleza nia yako ya kutaka kuoa, ahadi huwa nyingi sana.

Huyu atasema atagharamia gari la maharusi, mwingine atasema atasimamia usafiri wa wazazi, yule atasema mapambo nk, mradi kila aliyefika kwenye shughuli hiyo ya mwanzo wa maandalizi ya harusi ametoa ahadi yake.

Hapo huwa mwanzo wa mikikimikiki ya kukusanya fedha za michango na kuweka sawa mipango ya harusi. Ni safari ambayo huwa si ya chini ya miezi mitatu. Usipokuwa makini, kabla ya ndoa, bwana harusi anaweza kukonda kutokana na changamoto za kukimbizana na maandalizi.

Mwisho wake ni nini? Sherehe ya saa nne tu ukumbini, mamilioni yanakuwa yameshakatika. Kuna ishu nyingine ambayo vijana wanaotarajia kuoa huwa hawajiandai nayo kabla.

Baadhi ya watu huwa hawakamilishi walivyoahidi, mwisho wake unajikuta shughuli imekaribia na mambo hayajakamilika. Kwa kuwa lazima mambo yaende kama yalivyopangwa, ndipo bwana harusi mtarajiwa hujikuta akiingia kwenye mzigo wa madeni!

Yaani anachukua mke, anaanza naye maisha, badala ya kuanza na kuangalia maendeleo ya familia, anaanza kulipa madeni. Wakati mwingine madeni aliyojitengenezea yanaweza kuzalisha ugomvi ndani ya ndoa hiyo changa.

CHUKUA HII

Ndoa ina thamani kubwa kuliko sherehe ya kifahari ya saa chache. Sherehe yako haitakuwa na maana ikiwa ndoa itakuwa na migogoro. Mwanaume mjanja, hufikiria zaidi kumfurahisha mkewe, kuishi maisha ya amani na kuangalia maendeleo kuliko sherehe ya kifahari kwa lengo la kuwafurahisha watu.

Kama kweli uko vizuri, una fedha za kutosha, unaweza kuandaa sherehe kubwa; au kama una marafiki wenye ushirikiano mzuri, ‘wasio na pesa za mawazo’ unaweza kufanya sherehe kubwa, muhimu usiruhusu sherehe iwe chanzo cha kukupotezea furaha baada ya kutumia fedha nyingi.

MIFANO HAI

Ipo mifano ya watu wengi maarufu duniani wenye fedha zao, ambao hufanya sherehe ndogo.

Unaweza kuita kikao kidogo cha watu wako wa karibu kabisa – marafiki na jamaa mnaoshirikiana kwa shida na raha, mkaandaa hafla ya kawaida tu ya watu wasiozidi 100 (kwa mfano) na ukaweka kumbukumbu nzuri kwenye maisha yako.

Hii ni safu yetu sisi wanaume, kwa hiyo nimeongea kiume. Wanawake hata uwaeleze nini, hiki nilichokiandika hawawezi kukielewa. Nachukua time!

Mkuu! Unaakili nyingi mno...%100 naunga mkono ushauri wako..wanawake najuwa hawatakuelewa..
 
Ushauri mzuri, mi nadhani mtu afanye sherehe kulingana na uwezo wake tu, asiumize kichwa sana mpaka kuingia madeni ili watu wale mpaka wavimbiwe kwenye sherehe ,afu baadaye uanze kulia na madeni, ila kama uwezo upo its ok kufanya sherehe hata angani huko!
 
Harusi ni ya wawili,shida ya wengi aim ya kufanya sherehe kwa maharusi wengi

Tamaa ya mazawadi na vitu watakavyopewa,yani wengi hutaka Harusi(sherehe) kama kupata mtaji wa Kununulia mahitaji

ya kuanzia kama Kabati,fridge,vitanda,nk nk yani zile asset kubwa kubwa

Watu wanagharamika kualika watu wengi ili COST irudi na FAIDA juuu

Harusi imekua kama Biashara siku hizi
 
Hayo yote yanawezakana...

Tatizo ni mwanamke na wazazi..., mara nyingi hawapendi vitu vidogo... wanataka sherehe kubwa haswa...

Cc: mahondaw
 
Naomba nkutongoze hapa....ah ah kuna kitu watanzania kinakucost kuiga.. .ukienda mahotel yote makubwa.new Africa,mediteraneo,Whitesands Serena Tec unaweza andaa dinner chini ya elfu 50 wakakupa ukumbi na. mapambo we unaishia pambana na cocktails tu.....ila nut anataka ukumbi sinza millin4 mapombe,chakula....mwisho budget million 30 wakati ingeweza fanyika chini million 10
True
 
bf8852f5aa6c3b1693eb3a25bbe2c43f.jpg

WENGI wakiwaza kuhusu kufunga ndoa, mawazo yao huenda moja kwa moja kwenye namna sherehe ya harusi itakavyokuwa! Anataka gari kali la maharusi, ukumbi wa gharama, vyakula vya bei mbaya, wasanii maarufu wa kutumbuiza n.k.

Ni kweli ni vema kuifanya siku hiyo maalum na ya pekee maishani kuwa yenye kumbukumbu isiyofutika! Watu wanapenda kufanya sherehe kubwa ambayo itawafurahisha watu.

Katika kufanikisha hilo, huwa kunakuwa na kamati ya maandalizi ambayo ndiyo huratibu shughuli nzima. Katika kikao cha kwanza cha kuwaita wanakamati kuwaeleza nia yako ya kutaka kuoa, ahadi huwa nyingi sana.

Huyu atasema atagharamia gari la maharusi, mwingine atasema atasimamia usafiri wa wazazi, yule atasema mapambo nk, mradi kila aliyefika kwenye shughuli hiyo ya mwanzo wa maandalizi ya harusi ametoa ahadi yake.

Hapo huwa mwanzo wa mikikimikiki ya kukusanya fedha za michango na kuweka sawa mipango ya harusi. Ni safari ambayo huwa si ya chini ya miezi mitatu. Usipokuwa makini, kabla ya ndoa, bwana harusi anaweza kukonda kutokana na changamoto za kukimbizana na maandalizi.

Mwisho wake ni nini? Sherehe ya saa nne tu ukumbini, mamilioni yanakuwa yameshakatika. Kuna ishu nyingine ambayo vijana wanaotarajia kuoa huwa hawajiandai nayo kabla.

Baadhi ya watu huwa hawakamilishi walivyoahidi, mwisho wake unajikuta shughuli imekaribia na mambo hayajakamilika. Kwa kuwa lazima mambo yaende kama yalivyopangwa, ndipo bwana harusi mtarajiwa hujikuta akiingia kwenye mzigo wa madeni!

Yaani anachukua mke, anaanza naye maisha, badala ya kuanza na kuangalia maendeleo ya familia, anaanza kulipa madeni. Wakati mwingine madeni aliyojitengenezea yanaweza kuzalisha ugomvi ndani ya ndoa hiyo changa.

CHUKUA HII

Ndoa ina thamani kubwa kuliko sherehe ya kifahari ya saa chache. Sherehe yako haitakuwa na maana ikiwa ndoa itakuwa na migogoro. Mwanaume mjanja, hufikiria zaidi kumfurahisha mkewe, kuishi maisha ya amani na kuangalia maendeleo kuliko sherehe ya kifahari kwa lengo la kuwafurahisha watu.

Kama kweli uko vizuri, una fedha za kutosha, unaweza kuandaa sherehe kubwa; au kama una marafiki wenye ushirikiano mzuri, ‘wasio na pesa za mawazo’ unaweza kufanya sherehe kubwa, muhimu usiruhusu sherehe iwe chanzo cha kukupotezea furaha baada ya kutumia fedha nyingi.

MIFANO HAI

Ipo mifano ya watu wengi maarufu duniani wenye fedha zao, ambao hufanya sherehe ndogo.

Unaweza kuita kikao kidogo cha watu wako wa karibu kabisa – marafiki na jamaa mnaoshirikiana kwa shida na raha, mkaandaa hafla ya kawaida tu ya watu wasiozidi 100 (kwa mfano) na ukaweka kumbukumbu nzuri kwenye maisha yako.

Hii ni safu yetu sisi wanaume, kwa hiyo nimeongea kiume. Wanawake hata uwaeleze nini, hiki nilichokiandika hawawezi kukielewa. Nachukua time!
In light of this
Naomba nishare na nyie kitabu kizuri sana kwa watarajiwa

Jina:Things I Wish i'd Known Before We Got Married
Mwandishi: Gary Chapman

Nimeshindwa kuattach ila atakaeweza atuwekee
Nadhani hii ndo elimu ya msingi ya watu kuipata kabla ya kuingia kwenye hii taasisi
 
Back
Top Bottom