Kabla ya kufikiria harusi, weka haya akilini!

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,438
bf8852f5aa6c3b1693eb3a25bbe2c43f.jpg

WENGI wakiwaza kuhusu kufunga ndoa, mawazo yao huenda moja kwa moja kwenye namna sherehe ya harusi itakavyokuwa! Anataka gari kali la maharusi, ukumbi wa gharama, vyakula vya bei mbaya, wasanii maarufu wa kutumbuiza n.k.

Ni kweli ni vema kuifanya siku hiyo maalum na ya pekee maishani kuwa yenye kumbukumbu isiyofutika! Watu wanapenda kufanya sherehe kubwa ambayo itawafurahisha watu.

Katika kufanikisha hilo, huwa kunakuwa na kamati ya maandalizi ambayo ndiyo huratibu shughuli nzima. Katika kikao cha kwanza cha kuwaita wanakamati kuwaeleza nia yako ya kutaka kuoa, ahadi huwa nyingi sana.

Huyu atasema atagharamia gari la maharusi, mwingine atasema atasimamia usafiri wa wazazi, yule atasema mapambo nk, mradi kila aliyefika kwenye shughuli hiyo ya mwanzo wa maandalizi ya harusi ametoa ahadi yake.

Hapo huwa mwanzo wa mikikimikiki ya kukusanya fedha za michango na kuweka sawa mipango ya harusi. Ni safari ambayo huwa si ya chini ya miezi mitatu. Usipokuwa makini, kabla ya ndoa, bwana harusi anaweza kukonda kutokana na changamoto za kukimbizana na maandalizi.

Mwisho wake ni nini? Sherehe ya saa nne tu ukumbini, mamilioni yanakuwa yameshakatika. Kuna ishu nyingine ambayo vijana wanaotarajia kuoa huwa hawajiandai nayo kabla.

Baadhi ya watu huwa hawakamilishi walivyoahidi, mwisho wake unajikuta shughuli imekaribia na mambo hayajakamilika. Kwa kuwa lazima mambo yaende kama yalivyopangwa, ndipo bwana harusi mtarajiwa hujikuta akiingia kwenye mzigo wa madeni!

Yaani anachukua mke, anaanza naye maisha, badala ya kuanza na kuangalia maendeleo ya familia, anaanza kulipa madeni. Wakati mwingine madeni aliyojitengenezea yanaweza kuzalisha ugomvi ndani ya ndoa hiyo changa.

CHUKUA HII

Ndoa ina thamani kubwa kuliko sherehe ya kifahari ya saa chache. Sherehe yako haitakuwa na maana ikiwa ndoa itakuwa na migogoro. Mwanaume mjanja, hufikiria zaidi kumfurahisha mkewe, kuishi maisha ya amani na kuangalia maendeleo kuliko sherehe ya kifahari kwa lengo la kuwafurahisha watu.

Kama kweli uko vizuri, una fedha za kutosha, unaweza kuandaa sherehe kubwa; au kama una marafiki wenye ushirikiano mzuri, ‘wasio na pesa za mawazo’ unaweza kufanya sherehe kubwa, muhimu usiruhusu sherehe iwe chanzo cha kukupotezea furaha baada ya kutumia fedha nyingi.

MIFANO HAI

Ipo mifano ya watu wengi maarufu duniani wenye fedha zao, ambao hufanya sherehe ndogo.

Unaweza kuita kikao kidogo cha watu wako wa karibu kabisa – marafiki na jamaa mnaoshirikiana kwa shida na raha, mkaandaa hafla ya kawaida tu ya watu wasiozidi 100 (kwa mfano) na ukaweka kumbukumbu nzuri kwenye maisha yako.

Hii ni safu yetu sisi wanaume, kwa hiyo nimeongea kiume. Wanawake hata uwaeleze nini, hiki nilichokiandika hawawezi kukielewa. Nachukua time!
 
Mwanaume pambama wewe....maisha ni kitu gani haya bana....kujibanabana...tafuta hela fanya harusi, andaa sherehe watu wafurahi, wale, wanywe....sherehe ya harusi ndo sehemu ambayo unakutanisha ndugu wa pande zote mbili kwa wakati mmoja..watu watajuana hapa....ndo maana wanatambulishana...Acheni kulialia vijana na kujifanya mnajua sana budget na kupanga maisha.

Andaa sherehe ,,chakula, maji etc..kwa ajili ya sherehe ya ndoa yako...na Mungu atawabariki na atawarudishia. Kuandaa harusi ndo kipimo cha kwanza cha mwanaume halisi....ni kipimo cha jinsi alivyo na ushirikiano na jamii na watu wanaomzunguka..
 
Kuna mtu aliandika hapa juzi kati kama itakulazimu kufanya sherehe basi garama nzima isizidi nusu ya kipato chako kwa mwaka. Nilimuelewa sana.
Hii michango inafanya tunashindwa hata kuwanunulia maharusi zawadi za kumbukumbu maana ukiwaza ulishangia mchango wa maandalizi. Zawadi umpelekee nani sasa.
 
Unadhani huwa tunawafaham pale ukumbini sasa. Watu washalewa. Wanaeza toka pale na wakatongozana. Ndio maana kuna siku ya utambulisho baada ya hayo masherehe au kabla ya hayo masherehe.
Mwanaume pambama wewe....maisha ni kitu gani haya bana....kujibanabana...tafuta hela fanya harusi, andaa sherehe watu wafurahi, wale, wanywe....sherehe ya harusi ndo sehemu ambayo unakutanisha ndugu wa pande zote mbili kwa wakati mmoja..watu watajuana hapa....ndo maana wanatambulishana...Acheni kulialia vijana na kujifanya mnajua sana budget na kupanga maisha....
Andaa sherehe ,,chakula, maji etc..kwa ajili ya sherehe ya ndoa yako...na Mungu atawabariki na atawarudishia....
Kuandaa harusi ndo kipimo cha kwanza cha mwanaume halisi....ni kipimo cha jinsi alivyo na ushirikiano na jamii na watu wanaomzunguka..
 
Ndoa Ina thamani zaidi ya sherehe lakini hii haimzuii mtu kufanya sherehe kubwa.
Kila mtu yupo na interest zake ..kuna wengine wanapenda sherehe,Kuna wengine hawapendi.
Cha muhimu watu wafanye wanavyotaka.
Kuna watu wanapenda sherehe halafu binafsi uwezo kugaramia hata nusu ya garama ya sherehe hawezi. Yani michango yake na familia yake na watu wake wa karibu na bado garama ya sherehe haitimii. Ndio hapo unaanza kuwapigia watu simu hata ulikua huna mawasiliano nao miaka kibao. Zaidi ya kuangaliana WhatsApp status hamna salamu.
 
Unadhani huwa tunawafaham pale ukumbini sasa. Watu washalewa. Wanaeza toka pale na wakatongozana. Ndio maana kuna siku ya utambulisho baada ya hayo masherehe au kabla ya hayo masherehe.
Naomba nkutongoze hapa....ah ah kuna kitu watanzania kinakucost kuiga.. .ukienda mahotel yote makubwa.new Africa,mediteraneo,Whitesands Serena Tec unaweza andaa dinner chini ya elfu 50 wakakupa ukumbi na. mapambo we unaishia pambana na cocktails tu.....ila nut anataka ukumbi sinza millin4 mapombe,chakula....mwisho budget million 30 wakati ingeweza fanyika chini million 10
 
bf8852f5aa6c3b1693eb3a25bbe2c43f.jpg

WENGI wakiwaza kuhusu kufunga ndoa, mawazo yao huenda moja kwa moja kwenye namna sherehe ya harusi itakavyokuwa! Anataka gari kali la maharusi, ukumbi wa gharama, vyakula vya bei mbaya, wasanii maarufu wa kutumbuiza n.k.

Ni kweli ni vema kuifanya siku hiyo maalum na ya pekee maishani kuwa yenye kumbukumbu isiyofutika! Watu wanapenda kufanya sherehe kubwa ambayo itawafurahisha watu.

Katika kufanikisha hilo, huwa kunakuwa na kamati ya maandalizi ambayo ndiyo huratibu shughuli nzima. Katika kikao cha kwanza cha kuwaita wanakamati kuwaeleza nia yako ya kutaka kuoa, ahadi huwa nyingi sana.

Huyu atasema atagharamia gari la maharusi, mwingine atasema atasimamia usafiri wa wazazi, yule atasema mapambo nk, mradi kila aliyefika kwenye shughuli hiyo ya mwanzo wa maandalizi ya harusi ametoa ahadi yake.

Hapo huwa mwanzo wa mikikimikiki ya kukusanya fedha za michango na kuweka sawa mipango ya harusi. Ni safari ambayo huwa si ya chini ya miezi mitatu. Usipokuwa makini, kabla ya ndoa, bwana harusi anaweza kukonda kutokana na changamoto za kukimbizana na maandalizi.

Mwisho wake ni nini? Sherehe ya saa nne tu ukumbini, mamilioni yanakuwa yameshakatika. Kuna ishu nyingine ambayo vijana wanaotarajia kuoa huwa hawajiandai nayo kabla.

Baadhi ya watu huwa hawakamilishi walivyoahidi, mwisho wake unajikuta shughuli imekaribia na mambo hayajakamilika. Kwa kuwa lazima mambo yaende kama yalivyopangwa, ndipo bwana harusi mtarajiwa hujikuta akiingia kwenye mzigo wa madeni!

Yaani anachukua mke, anaanza naye maisha, badala ya kuanza na kuangalia maendeleo ya familia, anaanza kulipa madeni. Wakati mwingine madeni aliyojitengenezea yanaweza kuzalisha ugomvi ndani ya ndoa hiyo changa.

CHUKUA HII

Ndoa ina thamani kubwa kuliko sherehe ya kifahari ya saa chache. Sherehe yako haitakuwa na maana ikiwa ndoa itakuwa na migogoro. Mwanaume mjanja, hufikiria zaidi kumfurahisha mkewe, kuishi maisha ya amani na kuangalia maendeleo kuliko sherehe ya kifahari kwa lengo la kuwafurahisha watu.

Kama kweli uko vizuri, una fedha za kutosha, unaweza kuandaa sherehe kubwa; au kama una marafiki wenye ushirikiano mzuri, ‘wasio na pesa za mawazo’ unaweza kufanya sherehe kubwa, muhimu usiruhusu sherehe iwe chanzo cha kukupotezea furaha baada ya kutumia fedha nyingi.

MIFANO HAI

Ipo mifano ya watu wengi maarufu duniani wenye fedha zao, ambao hufanya sherehe ndogo.

Unaweza kuita kikao kidogo cha watu wako wa karibu kabisa – marafiki na jamaa mnaoshirikiana kwa shida na raha, mkaandaa hafla ya kawaida tu ya watu wasiozidi 100 (kwa mfano) na ukaweka kumbukumbu nzuri kwenye maisha yako.

Hii ni safu yetu sisi wanaume, kwa hiyo nimeongea kiume. Wanawake hata uwaeleze nini, hiki nilichokiandika hawawezi kukielewa. Nachukua time!

Kwanza suala la michango limekuwa kero sana.

Kwa mwezi unapokea kadi 5. Unakumbushwa kama deni.

Kwa kweli wabongo tubadilike, tufanye vitu vya uwezo wetu. Unafanya harusi ya Mil 30 halafu baada ya miezi 2 unaanza kutuambia tukukopeshe pesa.

Harusi ni msikitini, au kanisani au serikalini na haigharimu hata laki 5 .

Hayo masherehe ya kupata picha za kupost ni uwendawazimu tu , kama unapenda Hayo mambo make sure husumbui watu, umetangaza nia kwa starehe zako , usiwe burden kwa wengine. Plain truth!
 
Kuna watu wanapenda sherehe halafu binafsi uwezo kugaramia hata nusu ya garama ya sherehe hawezi. Yani michango yake na familia yake na watu wake wa karibu na bado garama ya sherehe haitimii. Ndio hapo unaanza kuwapigia watu simu hata ulikua huna mawasiliano nao miaka kibao. Zaidi ya kuangaliana WhatsApp status hamna salamu.
Hahahahaha..
Ni muhimu pia kufanya sherehe unayoweza kuafford.
 
Back
Top Bottom