Kabla ya kubomolewa nyumba zenu wakazi mijini ipelekeni serikali mahakamani kwa uzembe kupanga miji

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Kila kona tunasikia bomoabomoa na wananchi wakilia. mfano katika jiji la Dar es salaam tulisikia wakazi wa maeneo ya jangwani waliviziwa wakabomolewa nyumba zao, juzi tumesikia wananchi waliojenga karibu na reli wakilia, temeke tumesikia manispaa ikiwatisha watu waliojenga bila vibali kuwa nyumba zao zitabomolewa.

Hivi watanzania mnaoishi mijini ni kwa uzembe wa nani miji yetu inajengeka holela?

Ukitazama miji yetu inaonyesha huko zamani miji ilikuwa inapangwa, nyumba zilijengwa kwa mpangilio maalumu na viwanda vilikuwa sehemu moja. Lakini sijui kuanzia wapi serikali waliacha kupanga miji na usipopanga miji bila shaka wananchi wanajenga holela.

Ipo miji ambayo ilijitahidi kuendeleza jadi hii ya kupanga miji mfano manispaa ya kigoma, unakuta kuna mitaa nyumba za tofali za tope zote lakini nymba zimepangwa vizuri, kuna mitaa na barabara, ingawa kutokana na kutokuwa na fedha ya kuzijenga barabara hazipitiki lakini zinaonekana kuwa uwazi huu umeachwa kwa ajili ya barabara.

Ukitazama mifumo ya maisha ya mwananchi wa kawaida jinsi mtu anavyotafuta kiwanja akinunua katika utaratibu usio rasmi, wanauziana wao kwa wao, mtu anajipanga taratibu kuanza kujenga kwa kutumia mbinu duni kabisa maana ni kazi ngumu kupata fungu la pamoja la kujenga nyumba, mfano mkopo ambalo mtu anaweza kupiga bajeti za kutumia wataalamu na vifaa vya kisasa ili akamilishe na kuanza kulipa kidogokidogo.

Mtu akipata mshahara ananunua bati anaweka kwenye nyumba anayoapanga, akipata fedha kidogo anafyatua tofali, taratibu anapata vifaa anatafuta fedha ya fundi. Ki msingi mazingira ya kujenga nyumba kwa watu wengi ni magumu mno.

Kwa upande mwingine serikali inawajibu wa kupanga miji kubainisha maeneo ya makazi, maeneo ya biashara, na shughuli zote zinazofranyika mijini lakini kwa bahati mbaya sana serikali haifanyi hivi. inapofanya inajikita katika kufanya biashara inapima viwanja vichache na vinauzwa kwa bei ghali ambazo watumishi walio katika sekita rasmi na wafanya biashara wakubwa tu ndio wanaweza kumudu gharama za viwanja hivi.

Bado wanapima viwanja vichache sana ambavyo vinagubikwa na urasimu wa hali ya juu kuvipata kutokana na demand kuwa kubwa sana kuliko supply hivyo mtu wa kawaida ni ndoto kupata kiwanja kilichopimwa ingawa vingi ya viwanja hivi vimepimwa lakini havijapangwa kwa maana maeneo yanayovizunguka bado yanakuwa makazi holela na huduma huwa shida kupatikana.

Katika hili la makazi holela ni wazi tunakuwa na makazi holela katika miji yetu kutokana na uzembe wa serikali wasiotimiza wajibu wao wa kupanga miji.

inasikitisha kuona wazembe hawa wanawabebesha wananchi dhamana ya kupanga miji kwa kuendesha bomoabomoa pale wanapotaka kutekeleza mradi kwa kisingizio cha nia nzuri ya mradi au sheria zinasemaje.

Utawasikia tunabomolea watu wa mabondeni kuwalinda maana hatuwezi kukuacha uhatarishe maisha yako na sisi viongozi tukuangalie bali tunakubomolea ili kukunusuru. Kwanza kabisa ni kiongozi gani anakuacha unatumia kutokujua kwako unajenga bondeni nyumba inaisha, unakaa ndio anaibuka na kukubomolea eti kukusaidia. ni kwa nini hakukuonyesha kabla hujajenga mahali sahihi pa kujenga?

Zipo sababu nyingi zinaleta mafuriko ikiwemo ujenzi holela usiozingatia kiwango cha maji ikijumuisha kuziba mikondo ya maji na hivyo mvua zinaponyesha kubwa na kasi ya uondokaji maji kuwa ndogo mafuriko hutokea. ujenzi wa makazi holela, ujenzi wa barabara usioweka miundombinu sahihi ya kusafirisha maji mfano ma culvati madogo, yote haya huchangia kuleta mafuriko. Ni nani anayetakiwa kuwaongoza hawa wote wanapokuwa wanatekeleza shughuli zao kuhakikisha wanafanya kitu sahihi ili kuepusha jamii jamii na athari za mafuriko?

Bila shaka ni serikali na aliye mbele katika hili ni Wizara ya makazi na nyumba kuhakikisha inabainisha mkondo wa maji ni upi? si kwa jina bali kutazama kiwango cha maji cha juu katika mkondo husika na kusema kianzia mstari huu makazi wekeni hapa, shughuli za biashara wekeni hapa na kubainisha eneo la kila kitu. Inapokuwa serikali haifanyi unategemea wananchi wanawezaje kukaa maeneo sahihi?

Kama wananchi hawajakaa sehemu sahihi ni kwa makosa ya nani aliyetakiwa kuwaongoza au mwananchi mwenyewe? Wananchi wanatakiwa waongozwe kabla ya wao kujenga waonyeshwe maeneo sahihi, huo ndio uongozi na sio kusubiri wamejenga alafu kuwatia hatiani kama wamefanya viongozi wanavyowaza au tofauti sijui hii tunaweza kuita nini maana ni wazi sio uongozi.

Hebu fikiria mwananchi wa kawaida anamiriki genge mitaani leo hii unamwambia kwa mujibu wa sheria ya Tanroad mwananchi anatakiwa kukaa mita kadhaa nje ya barabara za tanroad, kwa mujibu wa sheria za manispaa mwananchi anatakiwa kukaa mita kadhaa kutoka barabara za manispaa. Eti kwa mujibu wa sheria ya Reli makazi yanatkiwa kukaa umbali fulani. Ki msingi hakuna jinsi ambavyo mtu wa kawaida mitaani anaweza kujua sheria hizi. Sheria hizi serikali ikisha zitunga inazifungia makabatini na wananchi wanaendelea na shughuli zao wakija kubomoa ndio wanatauhukumu kwanza kuwa tumekosea na kutufahamisha sheria zinavyosema.

Bila kuendesha bomoabomoa ya reli hakuna ambaye angekuwa anajua hapa sheria zinasemaje kama unabishi niambie kwa sheria za viwanja vya ndege watu wanatakiwa kukaa umbali kiasi gani? kwa sheria inayoongoza depoti za mafuta watu wanatakiwa kukaa umbali gani kutokea maeneo hayo?

Je, serikali huwa inatoa ushirikiano iwapo wananchi wanakwenda katika ofisi hizo kutafuta habari hizi? je wananchi wanajua waende wapi kupata habari gani?

Ki msingi serikali imelala usingizi wa fofofo katika swala la makazi na usingizi huo ndio unasababisha wananchi kujenga barabarani, kujenga kwenye reli au kuingilia maeneo wasiyostahili kuweka makazi na bado waliokaa maeneo sahihi kwa bahati nasibu wamevuruga kiasi hakuna maeneo ya kutolea huduma.

Hili ni tatizo la nani?
inakuwaje serikali bado imelala haitimizi wajibu huu bali ikikurupuka ni kuwasomea wananchi sheria ambazo kwao ni impossible kuzijua na kuwahukumu kwa hizo?

Lengo la kuipeleka mahakamani ni kuilazimisha serikali kutekeleza wajibu wake na kutambua kuwa uzembe wa serikali ni uzembe wa jamii nzima maana hata wananchi wenyewe wanayo nguvu ya kuiwajibisha serikali pale wanapoona haitimizi wajibu wake. kama wananchi wao wangekuwa wanaona kupanga miji yao ni muhimu bila shaka wangekuwa tayari washaelekeza serikali zao kupanga kwa kutumia nguvu zao za udhibiti kama kura lakini nao wamekaa kimya maana yake ni tatizo la jamii.

Inapokuwa ngoma droo hakuna mwenye makosa basi tukubaliane sisi wananchi na serikali yetu kuwa ndani ya miaka kadhaa serikali itimize wajibu wao wa kupanga na kutufahamisha sisi wananchi matumizi sahihi ya ardhi katika miji na vijiji na sisi wananchi tupewe mda wa kutekeleza mipango hiyo.

Upangaji huu mpya uzingatie miundombinu na makazi yaliyokwisha kujengwa.

Serikali ibuni mpango wa kuhakikisha inafanya jambo hili kama huduma ili kuondoa tatizo lililopo tayari na kulifanya kama biashara kutizama ni kiasi gani cha fedha wanaweza kutengeneza katika mradi huu, fikra ambazo ndio chanzo cha kuvuruga miji yetu hivyo vyanzo vya mapato ya kuendesha kuendesha mpango huu vibuniwe kwa njia ambayo kila mwananchi mpaka yule wa kipato cha chini kabisa atapata eneo la makazi lililopangwa na sio kubuni vyanzo ambavyo vitakuwa tatizo mfano inaweza kanzishwa kodi ya kupanga makazi na gharama hizi zitumike kuwajengea wale tu wanaohamishwa ili kupisha maeneo ya huduma kama barabara, masoko, shule na unabomolewa nyumba unajengewa nyumba kwa gharama nafuu pengine na jkt au magereza, wizara, manispaa ziajiri wataalamu wa kufanya kazi hizi na isiwe mpango wa kupiga dili kwa kulipana p/d au kutoa tenda za ajabu.

Mahakama ndiyo pekee inayoweza kulazimisha wazembe hawa kutambua uzembe wanaoufanya, fikra zao zote ni kupiga dili hivyo wao kupanga makazi wanawaza tukope mabilioni kutoka WB wapige dili tu au ni kukaa tu ofisini na kuwabomolea waliojenga holela kwa uzembe wao.

Wanaharakati tusaidieni kuwalazimisha hawa tuwe na muhafaka wa kupanga makazi yetu, tukiwa na nia tunaweza kuondoa makazi holela

Kama ni kuje
 
Wamepewa viwanja Mabwepande, cement na mabati bure kisha wameuza na kurudi jangwani, ujinga huo hakuna serikali ipo nyumba za mabondeni zitavunjwa tu.
 
Acha blah blah.. Watu waliopo mabondeni waondolewe, haiwezekani kila masika ni kutoa msaada kwa watu hao
 
Wamepewa viwanja Mabwepande, cement na mabati bure kisha wameuza na kurudi jangwani, ujinga huo hakuna serikali ipo nyumba za mabondeni zitavunjwa tu.

unamtizama wa jangwani wewe je ulipojenga unajua pamepangiwa nini?

ni raisi sana kusema mtu kajitakia lakini ukijua hakuna mtu anayependa kutake such risk kwa kujenga sehemu isiyoruhusiwa ila ni kwa kukosa namna.

wakija kubomolewa wa barabarani mnaibuka na stori zilezile, wakibomolewa wa relini mnaibuka na stori zilezile hivi kwa nini msijiweke kwenye viatu vyao? kwa nini msijiulize tatizo liko wapi?
 
Acha blah blah.. Watu waliopo mabondeni waondolewe, haiwezekani kila masika ni kutoa msaada kwa watu hao

nyinyi ndio wapanga miji mnaoacha kupanga miji mkipima viwanja vichache na kujirundikia viwanja kibao mkiuza wenyewe kwa manufaa binafsi huku jamii ikijenga holela. waliokaa mabondeni ni kwa uzembe wa serikali hivyo serikali kurudi kwenye kupanga na miji ndio suluhisho.

asilimia 80 ya watu wanaojenga mijini wako katika maeneo hayajapangwa na katika hawa kuna watu wako mabondeni, kuna watu wako milimani, kuna watu wako kwenye hifadhi za barabara, kuna watu wako kwenye maeneo ya wazi.

wenye macho katika jamii hawaangalii tatizo moja moja na kuwalaumu wahanga bali hutizama tatizo kwa pamoja na kujiuliza ni kwa nini kila sehemu kuna matatizo ya watu kujenga sehemu zisistahili? kiini cha tatizo ni nini? bila shaka mhusika anayestahili kubainisha mahali sahihi pa kila kitu alikuwa amesinzia na je leo amesinzia bado au kaamuka.
 
Naunga mkono hoja. Mfano mji wa kawe serikali ya mtaa ilikuwepo. Meya wa jiji alikiwepo.mkuu wa wilaya alikuwepo.mkuu wa mkoa yupo huko bunju kerege au kiaraka watu wanajijengea tuu hawasemi chochote kukishaharibika ndio utasikia bomoabomoa. Hii ni dhuluma kubwa kwa wananchi na upokwaji wa haki ya kuishi vizuri
 
Back
Top Bottom