CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 244
- 312
KABLA HUJAANZA KUDAI TUME HURU AU KUVUNJA TUME ILIYOPO TAFADHALI TUSAIDIENI KUJIBU MASWALI HAYA. UKIKOSA MAJIBU YAKE BASI UTAKUWA HUNA TOFAUTI NA JAMAA WA TIGRIS AND EUPHRATES WALIORUHUSU MGENI KUJENGA KWENYE KIHAMBA CHA UKOO.
Disclaimer: huenda kweli tunahitaji tume "nyingine". Nasema "huenda" na natumia neno "nyingine". Nasema 'huenda' kwa kuwa sijathibitishiwa umuhimu wa kubadili iliyopo. Nasema 'nyingine' maana sijasikia kwa kina ni vipi "Uhuru" wa hiyo tume "huru" utakuwa tofauti na uhuru wa tume iliyopo. Huenda majibu yatanibadilisha mwelekeo?
1. Wajumbe watapatikanaje?
2. Nani atawateua?
3. Watawajibika kwa nani ambaye atakuwa huru utakavyo?
4. Nini kilifanya iliyoitwa tume huru kule Zanzibar ife? Walikosea wapi?
5. Unadhani kuna mtanzania ambaye hana chama au mapenzi na chama au mapenzi na mtu? Kama hakuna tume huru itapatikanaje?
6. Unapendekeza taasisi gani zinafaa kutoa wajumbe wa tume ili iwe huru? Taasisi hizo ni huru?
7. Je, kwa nini Kenya ambayo inasifiwa kuwa na tume huru bado walioshindwa hawaridhiki?
8. Je, unadhani hivi vyama vya upinzani vina watu wenye sifa ya kuwa wajumbe wa tume? Toa sababu na walau wataje mtu mmoja kila chama anayefaa kuwa mjumbe wa hiyo tume huru? Kwa yeye kuwa chama cha siasa sio kwamba tayari si mtu huru?
9. Ikitokea wajumbe wa tume wamehitilafiana kama ilivyokuwa Zanzibar Serikali ifanye nini kuepusha nchi isiingie kwenye machafuko?
10. Je, ili tume iwe huru na yenye ufanisi wajumbe wawe wangapi? Wanawake wawe %ngapi? Je makabila na dini yawakilishwe kwenye tume? Ikitokea tume ina wanaume au wanawake tupu, waislamu tupu au wakristo tupu au asilimia kubwa itafaa? Nini kifanyike ili isitokee time ina maaskofu au mashehe tupu au kwa wingi kama kwenye dua au maombi?
11. Utaratibu wa sasa wa tume uendelee? Uwepo wake Una hasara au faida? Yaani hata kama Una hasara lakini faida ikiwa kubwa tuendelee nao au tuachane nao?
12. Je nchi hizi za kiafrika hata tume ingeundwa na malaika na mitume kuna desturi ya kukubali matokeo? Naomba ututajie walau watu 10 tu watanzania ambao unadhani wanaweza kuunda tume huru na kukubalika walau na 70% ya watanzania?
ONYO: Tusipoyajibu maswali haya bila muku, mihemko, migebuka, mbeke au uchama itakuwa hatari kukurupuka na kubadili tume iliyopo. Mihemko aina hii ndio inawakumba Iraq sasa! Kuruhusu mgeni ajenge kwenye kihamba cha ukoo!