Kabla ya kodi za nyumba tungeanza na ada elekezi

Genius Messi

Member
Oct 14, 2017
74
52
Serikali kujipanga kuanza kwa mamlaka ya nyumba ni mpango mzuri utakao punguza makali ya maisha kwa watanzania wengi, hatua ya kupongezwa.

Lakini pia ingekua vizuri wangeanzia kwenye ada(fees) kuangalia upande huo kuanzia nursery hadi vyuo vikubwa watu binafsi wamekua wakijipangia viwango vya juu mno watakavyo inaumiza sana.

Tukisaidiwa huko na wakipita kwenye afya angalau kila mtanzania awe na bima kwa malipo yasioumiza.
 
Kama ada una shindwa kulipa kwenye shule ambayo hukupeleka hata tofali mlete mwanao huku govt. Sisi walimu wa kawaida tutamfundisha mwanao KKK ingawa maslai yetu hamtupi.
Kwenye nyumba ni sawa kupanga kodi stahiki ukizingatia watu wanaopangisha wengi ni wasanii
 
Pambana na hali yako maana hamna namna, we kama huna uwezo unataka mtoto wako akasome Feza kwa mlango wa ada elekezi?

Ujamaa ulishajifia naona watu mnataka muurudishe kiaina sababu mpo masikini.
 
Pambana na hali yako maana hamna namna, we kama huna uwezo unataka mtoto wako akasome Feza kwa mlango wa ada elekezi?

Ujamaa ulishajifia naona watu mnataka muurudishe kiaina sababu mpo masikini.
Mkuu hoja ya jamaa ipo sawa kabisa hata wewe kama hauna hela si ubaki huko kijijini kwenu mjini waacheni wenye nyumba zao kama wataamua kufugia kuku ni zao wenyewe lakini sio mambo ya kupangiana jinsi ya kupokea kodi.

Ukizangatia kila mtu anataka elimu bora na mahali pazuri pa kulala pia so kuwe na uwiano sawa kwenye hili sio wanaangalia tu nyumba zetu au wameshahisi tunafaidika sana ndio wanataka tuanze kuishi kama mashetani na sisi wenye nyumba.
 
Hii ishu ya kodi elekezi naipuuza kama nilivyo puuza Ada elekezi. Kama wameshindwa kurasimisha makazi holela, kutoa hati miliki katika maeneo yasiyopimwa hawato weza hili. Matamko haya yatapita kama yalivyopita mengine. Wawaache wazee wetu viwasaidie vikodi vyao mana walijinyima wakajenga leo hii vinawasaidia uzeeni.
 
Serikali kujipanga kuanza kwa mamlaka ya Nyumba ni mpango mzuri utakao punguza makali ya maisha kwa wstanzania wengi,hatua ya kupongezwa
lakini pia ingekua vizuri wangeanzia kwenye ada(fees) kuangalia upande huo kuanzia Nursery hadi vyuo vikubwa watu binafsi wamekua wakijipangiaviwango vya juu mno watakavyo..inaumiza sana
Tukisaidiwa huko na wakipita kwenye Afya angalau kila mtanzania awe na bima kwa malipo yasioumiza.
Kwani kwenye afya..... Bima kwa mwaka mzima si inagharimu almost 50400 mbn serikali imekusaidia hapo ndugu
 
Kama ada una shindwa kulipa kwenye shule ambayo hukupeleka hata tofali mlete mwanao huku govt. Sisi walimu wa kawaida tutamfundisha mwanao KKK ingawa maslai yetu hamtupi.
Kwenye nyumba ni sawa kupanga kodi stahiki ukizingatia watu wanaopangisha wengi ni wasanii
robo tu ya wanafunzi wakitoka shule binafsi shule za serikali hazitaweza kuwamudu serikali haina shule za kutosha
 
Serikali kujipanga kuanza kwa mamlaka ya nyumba ni mpango mzuri utakao punguza makali ya maisha kwa watanzania wengi, hatua ya kupongezwa.

Lakini pia ingekua vizuri wangeanzia kwenye ada(fees) kuangalia upande huo kuanzia nursery hadi vyuo vikubwa watu binafsi wamekua wakijipangia viwango vya juu mno watakavyo inaumiza sana.

Tukisaidiwa huko na wakipita kwenye afya angalau kila mtanzania awe na bima kwa malipo yasioumiza.
Mkuu huko kwenye ada za mashule tulishamaliza...hukumbuki tulitoa tamko takriban miaka 2 nyuma?
 
Bima ya afya ni sawa. Ada ni maamuzi. Utakuja kulia huko juu maana mikopo ni ya watoto wa maskini.

Kodi hiyo iwe Kwa mwezi ni sawa. Tumalizane mwanzo wa mwezi tu.
 
Kama ada una shindwa kulipa kwenye shule ambayo hukupeleka hata tofali mlete mwanao huku govt. Sisi walimu wa kawaida tutamfundisha mwanao KKK ingawa maslai yetu hamtupi.
Kwenye nyumba ni sawa kupanga kodi stahiki ukizingatia watu wanaopangisha wengi ni wasanii
Hata nyumba kumuingilia mwenyewe ambaye hujamsaidia kwa lolote si sawa. Haya ni mambo ya kisiasa zaidi .
 
Usiache mpa mwanao elimu Bora kwa kigezo cha eti elimu ya juu atakosa mkopo. Tambua mkuu wapo wtt wengi wa maskin tena waliopt Education na walikoswa mkopo. Tambua hata hii mikopo miaka kadhaa ijayo haitakuwepo kwa wote kama zilivyo anza kupotea ajira.
 
Kama ada una shindwa kulipa kwenye shule ambayo hukupeleka hata tofali mlete mwanao huku govt. Sisi walimu wa kawaida tutamfundisha mwanao KKK ingawa maslai yetu hamtupi.
Kwenye nyumba ni sawa kupanga kodi stahiki ukizingatia watu wanaopangisha wengi ni wasanii
Kwani wewe ulileta tofali kwenye nyumba hiyo unayopanga.huwezi nipangia bei wakati hujaniuliza hata gharama ya ujenzi na maintanance ikoje.wasiotaka waende wakapange hizo za NHC.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom