Mwaka 2014, Zitto Kabwe aliitwa na Kamati Kuu ya Chadema akitakiwa kujibu tuhuma za usaliti dhidi ya chama lakini hakuitikia wito huo.
Badala yake Zitto kupitia kwa wakili wake Arbert Msendo alifungua kesi Mahakamani akiomba zuio la muda asivuliwe uanachama wake ambapo mahakama ilikubali, lakini Mawakili wa Chadema Peter Kibatala, Lissu na John Mallya waliwasilisha hoja kumpinga Zitto.
Hoja zilizowasilishwa;
1. Kitendo cha Zitto kufungua kesi katika mahakama za kisheria amekiuka Katiba ya chama.
“Kanuni za kusimamia shughuli, mwenendo na maadili ya wabunge wa Chadema (2006), kifungu cha 8.0 (a) (x); zinasomeka ifuatavyo; “Chadema itashughulikia matatizo ya viongozi na wanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama”.
2. Mashitaka yamekiuka kifungu cha 13 cha Sheria ya Kanuni ya Mwenendo wa Kesi za Madai, Sura ya 33, kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.
Zitto alipaswa kusajili kesi yake katika Masjala ya Mahakama ya Wilaya na sio Masjala ya Mahakama Kuu, kama alivyofanya.
Kwa hoja hizo mbili, Jaji Mziray alisema kuwa hoja hizo zinatosha kutupilia mbali shauri hilo na kwamba hakuwa na haja ya kuendelea na hoja nyingine za pingamizi.
Angalizo: Kesi ya kina Halima Mdee na wenzake ni karibu zinafanana na aliyofungua Zitto, wasije wakarudia makosa.