Kabla ya Halima Mdee na wenzake kukimbilia mahakamani wajikumbushe kesi ya Zitto iliyotupiliwa mbali na Mahakama Kuu

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
20,854
45,766
Mwaka 2014, Zitto Kabwe aliitwa na Kamati Kuu ya Chadema akitakiwa kujibu tuhuma za usaliti dhidi ya chama lakini hakuitikia wito huo.

Badala yake Zitto kupitia kwa wakili wake Arbert Msendo alifungua kesi Mahakamani akiomba zuio la muda asivuliwe uanachama wake ambapo mahakama ilikubali, lakini Mawakili wa Chadema Peter Kibatala, Lissu na John Mallya waliwasilisha hoja kumpinga Zitto.

Hoja zilizowasilishwa;

1. Kitendo cha Zitto kufungua kesi katika mahakama za kisheria amekiuka Katiba ya chama.

“Kanuni za kusimamia shughuli, mwenendo na maadili ya wabunge wa Chadema (2006), kifungu cha 8.0 (a) (x); zinasomeka ifuatavyo; “Chadema itashughulikia matatizo ya viongozi na wanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama”.

2. Mashitaka yamekiuka kifungu cha 13 cha Sheria ya Kanuni ya Mwenendo wa Kesi za Madai, Sura ya 33, kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.

Zitto alipaswa kusajili kesi yake katika Masjala ya Mahakama ya Wilaya na sio Masjala ya Mahakama Kuu, kama alivyofanya.

Kwa hoja hizo mbili, Jaji Mziray alisema kuwa hoja hizo zinatosha kutupilia mbali shauri hilo na kwamba hakuwa na haja ya kuendelea na hoja nyingine za pingamizi.

Angalizo: Kesi ya kina Halima Mdee na wenzake ni karibu zinafanana na aliyofungua Zitto, wasije wakarudia makosa.
 
S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,113
1,516
Labda C.19 Watazingatia hukumu hii... ya nini kulazimishwa kupendwa ili hali mume amekubwaga mtama chini miguu juu na kufanya yeke., amekuacha tu uende ukajisafishe bafuni na uvae nguo zako... options zilizopo ni tatu... Waende either ccm, ACT, umoja party; Watubu na kusamehewa na au waanzishe chama chao wenyewe... Inapaswa sasa wajifunze toka kwa akina Membe, Sofia simba, Lowasa, Rostam, Nyarandu, Masha, Waitara na wengine wote waliorejea ccm bila kwenda mahakamani...
 
Ngorunde

Platinum Member
Nov 17, 2006
3,234
5,689
Nazidi kuwakumbusha kina Mdee, kwa mujibu wa katiba ya Chadema ukishafungua shauri mahakamani dhidi ya chama chako automatically umejitoa uanachama.
Walishafukuzwa uanachama hata kabla ya kwenda mahakamani.

Btw, sidhani kama chadema wana lolote tena la kujadili kuhusiana na hawa watu..sana sana wanaweza kujadili matumizi mabaya ya pesa za umma zinazopewa watu walioko bungeni kinyume na katiba.
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
64,601
68,549
Mwaka 2014, Zitto Kabwe aliitwa na Kamati Kuu ya Chadema akitakiwa kujibu tuhuma za usaliti dhidi ya chama lakini hakuitikia wito huo.

Badala yake Zitto kupitia kwa wakili wake Arbert Msendo alifungua kesi Mahakamani akiomba zuio la muda asivuliwe uanachama wake ambapo mahakama ilikubali, lakini Mawakili wa Chadema Peter Kibatala, Lissu na John Mallya waliwasilisha hoja kumpinga Zitto.

Hoja zilizowasilishwa;

1. Kitendo cha Zitto kufungua kesi katika mahakama za kisheria amekiuka Katiba ya chama.

“Kanuni za kusimamia shughuli, mwenendo na maadili ya wabunge wa Chadema (2006), kifungu cha 8.0 (a) (x); zinasomeka ifuatavyo; “Chadema itashughulikia matatizo ya viongozi na wanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama”.

2. Mashitaka yamekiuka kifungu cha 13 cha Sheria ya Kanuni ya Mwenendo wa Kesi za Madai, Sura ya 33, kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.

Zitto alipaswa kusajili kesi yake katika Masjala ya Mahakama ya Wilaya na sio Masjala ya Mahakama Kuu, kama alivyofanya.

Kwa hoja hizo mbili, Jaji Mziray alisema kuwa hoja hizo zinatosha kutupilia mbali shauri hilo na kwamba hakuwa na haja ya kuendelea na hoja nyingine za pingamizi.

Angalizo: Kesi ya kina Halima Mdee na wenzake ni karibu zinafanana na aliyofungua Zitto, wasije wakarudia makosa.
Lengo ni kuchelewesha muda wafike 2025
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
26,987
30,112
Nazidi kuwakumbusha kina Mdee, kwa mujibu wa katiba ya Chadema ukishafungua shauri mahakamani dhidi ya chama chako automatically umejitoa uanachama.
halafu chama kinahubiri uhuru wa maoni.

udictator ni angle tu uliyokaa.
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
64,601
68,549
Walishafukuzwa uanachama hata kabla ya kwenda mahakamani.

Btw, sidhani kama chadema wana lolote tena la kujadili kuhusiana na hawa watu..sana sana wanaweza kujadili matumizi mabaya ya pesa za umma zinazopewa watu walioko bungeni kinyume na katiba.
CHADEMA walishamaliza kazi yao
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom