Kabla Rais Magufuli hajazama jumla, ajiulize kwanza kwanini Kagame na Kikwete walikuwa na mgogoro?

Mleta mada una wasiwasi kama nilionao! Si ajabu majeshi yetu congo ukasikiya yamerudi ma machafuko congo yakawa makubwa zaidi! Kingine ni kwamba urafiki wetu na rwanda ina maana ni kuipoteza congo! Kiuchumi wa bandari yetu congo ni muhimu kuliko Rwanda! Sioni ajabu mizigo bandarini kwetu dar imepungua coz mshirika muhimu tumempiteza
Umesema Kongo, unamaanisha DRC?
 
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameingia kwenye uhusiano wa kirafiki tena urafiki mkubwa na rais wetu John Magufuli. Urafiki huo unaonekana kuwa ulivutiwa kwa namna moja na Paul Kagame kwani ndiye aliyemualika rais Magufuli kwenda Rwanda kwenye kumbukumbu ya mauaji ya halaiki mwaka 1994.

Lakini tukiweka kumbukumbu sawa, ni juzi tu rais wetu mstaafu Jakaya Kikwete aliingia kwenye mgogoro mkubwa na wa aina yake na rais Paul Kagame wa Rwanda kiasi cha kupelekea vitisho cha waziwazi kwa kila upande.

Kwa msioelewa ni kuwa chimbuko la mgogoro huo ulielezwa kuwa ni Kikwete kujaribu kumshawishi Kagame kukaa meza moja na waasi wa FLDRA ili wafikie muafaka na hatimaye Rwanda iwe nchi moja ya amani na umoja. Hapo pakaanza kutolewa matamko kwa kila upande na kupelekea kuhasimiana vilivyo.

Lakini ukweli wa mgogoro huo na chimbuko lake ni hatua ya Kikwete kupeleka wanajeshi Congo na kuwa kiongozi mkuu wa kupambana na waasi wa M23 ambao walikuwa wakipigana na serikali ya Joseph Kabila serikali iliyovunjilia mbali uhusiano na Rwanda na kuwa kipenzi cha Jakaya Kikwete enzi za utawala wake.

Kama tutakumbuka ni kuwa rais wa Marekani Barack Obama aliituhumu Rwanda waziwazi kuwa inashirikiana na waasi wa M23 kuhujumu majeshi ya amani huko Congo na kufanya uhalifu wa rasilimali za Congo, aidha Obama aliituhumu zaidi serikali ya Kagame kuwa inaidhoofisha Congo na kutishia kuiwekea Rwanda vikwazo.

Aidha Obama aliendeleza tuhuma zake kwa Kagame pale ambapo alikuwa ndani ya ardhi ya Tanzania nadhani ni baada yakuulizwa swali na mwandishi wa DW. Kagame akaanza sana kuiandama Tanzania na kutishia kuisambaratisha EAC huku yeye akiwa bado ni mgeni kwenye jumuiya hiyo.

Kufuatia uhusiano huu ni lazima mheshimiwa rais ambaye kwa vyovyote vile neno "ugeni" kwake haliepukiki ajiulize na kuwaza sana kama ni uhusiano imara kweli? Je, chombo kama FBI kiweze kuubaini uhalisia wa Kagame, sisi hatukiamini? Tunacho imara zaidi ya hicho kiasi cha kupata intelijensia tofauti na hiyo?

Ni kwanini rais Kagame mbiombio aanzishe uhusiano na rais ambaye bado ni mpya kwa nchi ambayo kimsingi hakuwa na mahusiano mazuri nayo tena kutokana na sera zake za nje?

Ukweli ni lazima tujiulize, haiba ya Kagame mbele ya watu (kwa kuichambua kiumakini) inatushawishi sisi kama nchi kuzama wazimawazima kiasi hata cha kuomba wataalamu wake waisaidie Tanzania kwenye nyanja muhimu?

Time is everything, time tells!

=============
Je? Khabari hii inahusiana na haya yaliyotoke aCongo? kw awatanzznia kutekwa?
 
Mtajuana na mtakatifu wenu, mambo ya kutokushaurika au kutokutaka mawazo toka kwa mtu mda mwingine huleta madhara makubwa sana
 
Mleta mada una wasiwasi kama nilionao! Si ajabu majeshi yetu congo ukasikiya yamerudi ma machafuko congo yakawa makubwa zaidi! Kingine ni kwamba urafiki wetu na rwanda ina maana ni kuipoteza congo! Kiuchumi wa bandari yetu congo ni muhimu kuliko Rwanda! Sioni ajabu mizigo bandarini kwetu dar imepungua coz mshirika muhimu tumempiteza
Acha hizo wewe, kwani mizigo yote inayopita huko bandarini Dar ni ya serikali ya Congo au ya Kabila?,waagizaji mizigo ni raia wa Congo ambao hizo beef zenu wala hawazijui.
 
Hahahaaa hah
Kagame lazima awe muhimu awamu hii maana anatoa tactical advise jinsi ya kuminya uhuru wa kujieleza na technical expert opinion jinsi ya kukolimba wakosoaji. Kagame ni consultant awamu hii. Birds of the same feathers fly together. Hayo maswala ya uhusiano na Kongo nani atamwambia wakati wote wanamwogopa na huku yeye hajui hata Ghadafi alikuwa rais wa nchi gani?
 
Aliyeasisi ujenzi wa reli hadi Rwanda ni JK. Hivyo magufuli anatekeleza na hiyo ndo ccm
 
Juzi kagame na museveni walikuwa kwa Kenyatta .....leo walewale kama mapacha wamerudi kwa magufuli,hata kuivamia Congo walienda wawili...museveni na kagame,nkurunzinza wamemkosakosa juzi tu,kagame aliukwaa urais akitokea Uganda ambako alikuwa Mkuu wa intelijensia ya jeshi la Uganda kwa miaka mingi sana,hata RPF walifanya maandalizi ya kuivamia Rwanda wakitokea Uganda .....Hima Empire.

Tusishangae wanyamulenge,M23, na magenge mengine yaliyozimishwa na kikwete yakaibuka
Yataibuka!
 
Lazima na wale wahamiaji haramu na mifugo yao wanajiandaa kurudi tena Tanzania .....

Wahamiaji hawa hawana tofauti na wahamiaji waliokwenda Congo wakakaa muda mrefu baadae Congo ikahoji uraia wao.

Haikuchukua muda tayari wanyamulenge wakawa na silaha,walichofanya Congo kila mtu anajua.
Na ukanda wa Geita,Kagera na kigoma ni maeneo ambayo wametapakaa wanyarwanda na wana umoja wa hali ya juu sana.

Ni tishio kwa usalama kwa kuwa wamekataa hata kuji-intergrate na jamii hata kwa kuoleana.Na kuna madai mtanzania akioa mnyarwanda,huyo mnyarwanda hawezi kukubali kuzaa na mume wa kitanzania,atakachofanya atamwita kaka yake ampe mimba ili aendeleze kizazi cha pua nyembamba
Umesema kweli, wapo mpaka leo mapori yote ya Biharamuro, Karagwe hadi Misenyi.
 
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameingia kwenye uhusiano wa kirafiki tena urafiki mkubwa na rais wetu John Magufuli. Urafiki huo unaonekana kuwa ulivutiwa kwa namna moja na Paul Kagame kwani ndiye aliyemualika rais Magufuli kwenda Rwanda kwenye kumbukumbu ya mauaji ya halaiki mwaka 1994.

Lakini tukiweka kumbukumbu sawa, ni juzi tu rais wetu mstaafu Jakaya Kikwete aliingia kwenye mgogoro mkubwa na wa aina yake na rais Paul Kagame wa Rwanda kiasi cha kupelekea vitisho cha waziwazi kwa kila upande.

Kwa msioelewa ni kuwa chimbuko la mgogoro huo ulielezwa kuwa ni Kikwete kujaribu kumshawishi Kagame kukaa meza moja na waasi wa FLDRA ili wafikie muafaka na hatimaye Rwanda iwe nchi moja ya amani na umoja. Hapo pakaanza kutolewa matamko kwa kila upande na kupelekea kuhasimiana vilivyo.

Lakini ukweli wa mgogoro huo na chimbuko lake ni hatua ya Kikwete kupeleka wanajeshi Congo na kuwa kiongozi mkuu wa kupambana na waasi wa M23 ambao walikuwa wakipigana na serikali ya Joseph Kabila serikali iliyovunjilia mbali uhusiano na Rwanda na kuwa kipenzi cha Jakaya Kikwete enzi za utawala wake.

Kama tutakumbuka ni kuwa rais wa Marekani Barack Obama aliituhumu Rwanda waziwazi kuwa inashirikiana na waasi wa M23 kuhujumu majeshi ya amani huko Congo na kufanya uhalifu wa rasilimali za Congo, aidha Obama aliituhumu zaidi serikali ya Kagame kuwa inaidhoofisha Congo na kutishia kuiwekea Rwanda vikwazo.

Aidha Obama aliendeleza tuhuma zake kwa Kagame pale ambapo alikuwa ndani ya ardhi ya Tanzania nadhani ni baada yakuulizwa swali na mwandishi wa DW. Kagame akaanza sana kuiandama Tanzania na kutishia kuisambaratisha EAC huku yeye akiwa bado ni mgeni kwenye jumuiya hiyo.

Kufuatia uhusiano huu ni lazima mheshimiwa rais ambaye kwa vyovyote vile neno "ugeni" kwake haliepukiki ajiulize na kuwaza sana kama ni uhusiano imara kweli? Je, chombo kama FBI kiweze kuubaini uhalisia wa Kagame, sisi hatukiamini? Tunacho imara zaidi ya hicho kiasi cha kupata intelijensia tofauti na hiyo?

Ni kwanini rais Kagame mbiombio aanzishe uhusiano na rais ambaye bado ni mpya kwa nchi ambayo kimsingi hakuwa na mahusiano mazuri nayo tena kutokana na sera zake za nje?

Ukweli ni lazima tujiulize, haiba ya Kagame mbele ya watu (kwa kuichambua kiumakini) inatushawishi sisi kama nchi kuzama wazimawazima kiasi hata cha kuomba wataalamu wake waisaidie Tanzania kwenye nyanja muhimu?

Time is everything, time tells!

=============

Do not trust Tanzanians ambao mada sasa imekuwa ni magufuli tu. Yani mnachokonoa hata yasiyo na msingi mradi muntaje. mkuu wetu. Why. Heshima iko wapi Mbona wazazi wetu hatuwaaniki. Unataka kusema hawana makosa. Kosa La msingi hasa ambalo linakuuma binafsi ni lipi. MTU kuwa na nia njema ya kuipigania Nchi. Hivi Tz sisi tunaojijua wapiga dili kuanzia mlinZi mpka mkurugenzi tunaweza kweli kukaa kumnyoshea kiongozi anayetetea maslahi ya Nchi. Unaweza wewe sema hapa uaminifu gani uliokuwepo. Tz haingaliwi kwa manufaa ya siku mbili. What about the next generation. Tunajikweza sana kama vile tuko sawa na hao wameamerika. CApitalist is always a Capitalist. No love there. So be careful what you wish for.
 
Wazazi wetu? Mkuu unaongea nini? Hapa tunamkosoa Mkuu wa nchi. Kama hataki aache Urais. Hakuna kiongozi asiyekosolewa. Ukiona ukosoaji umezidi basi ujue kweli unapotea na si kuanza kulalama eti usikosolewe. Rais Magufuli awe humble na asikilize ushauri na maoni kama kiongozi mzuri. Kama hataki ajue he will face continuous resistance. That's how leadership works.
 
hatuko salama sana kwnyew uhusiano na Kagame..... inatubidi kuwa makini sana kucheza hili game
 
Do not trust Tanzanians ambao mada sasa imekuwa ni magufuli tu. Yani mnachokonoa hata yasiyo na msingi mradi muntaje. mkuu wetu. Why. Heshima iko wapi Mbona wazazi wetu hatuwaaniki. Unataka kusema hawana makosa. Kosa La msingi hasa ambalo linakuuma binafsi ni lipi. MTU kuwa na nia njema ya kuipigania Nchi. Hivi Tz sisi tunaojijua wapiga dili kuanzia mlinZi mpka mkurugenzi tunaweza kweli kukaa kumnyoshea kiongozi anayetetea maslahi ya Nchi. Unaweza wewe sema hapa uaminifu gani uliokuwepo. Tz haingaliwi kwa manufaa ya siku mbili. What about the next generation. Tunajikweza sana kama vile tuko sawa na hao wameamerika. CApitalist is always a Capitalist. No love there. So be careful what you wish for.
are u out of ur mind? mfia chama mnafiki mkubwa unadhani Tz ni familia yake hadi asikosolewe? embu tuondolee ubashite wako mfia tumbo hata kwenye familia anakosolewa sembuse nchi , kama kweli amechoka na hataki kukosolewa mwambieni aachie ngazi
 
Back
Top Bottom