Kabla hujazaa nje ya ndoa kumbuka manyanyaso ya mama wa kambo

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
10,344
14,114
Ujana ni nusu ya uwendaazimu ila mimi nasema hivi ujana ni wendaazimu kamili maana utakuta mtu enzi za ujana wake anajihusisha na mahusiano na mabinti tofauti tofauti akisha wapa ujauzito anawakimbia,baadae anarudi kudai watoto kama si wendaazimu huo ni nini? Mimi nadhani hii yote ni kutokana na upungufu wa imani na mporomoko wa maadili na hii ndio hupelekea watoto kunyanyasika na kujikuta wanakosa malezi bora ya wazi wawili. Asikwambie mtu hakuna kitu kizuri kwa mtoto kama kulelewa na wazazi wake wote wawili {ukiacha kufariki}
hqdefault.jpg

Tuwahurumieni watoto jamani ukiwa kama kijana hakikisha unapanga uzazi na mtu sahihi ambaye ndie utakaeanzisha nae familia kinyume na hapo utamuathiri mtoto kisaikolojia maana atatamani sana malezi ya wazazi wake wawili atakosa ata ukisema umchukue mwanao uishi nae mara nyingi wazazi wakufikia huwa hawana urafiki kabisa na watoto wasiokuwa wakwao,mtoto atanyanyasika sana na wengine hupoteza kabisa muelekeo wa maisha.
11-30-2015Central_African.jpg

Vijana wenzangu tuutumie ujana wetu vizuri, kama wewe umelelewa na wazazi wako wote wawili kwanini umtafutie mwanao matatizo? Nimegundua chanzo kikubwa siku hizi cha watoto kukosa maadili kwa kiasi kikubwa kinachangiwa sana na kukosa malezi ya wazazi wote wawili sijui ni ujinga maana elimu ya uzazi tunaanza kufundishwa tokea tukiwa darasa la 5 lakini bado tu haitusaidii kuepuka mimba zisizotarajiwa.
lonely-african-child.jpg

Baadae mtoto akikuwa anakuja kuwa jambazi anakuchukia mzazi wake au anakuja kufanikiwa baba umepigika unaanza kujirudisha kisa mtoto kawa super nyota kutwa anasomwa magazetini na redioni anasikilizwa,hii ni aibu kubwa sana maana malipo siku zote ni hapa hapa duniani,kuyaepuka hayo hakikisha unapanga uzazi na mtu sahihi ambae utakuwa teyari kuanzisha nae safari ya maisha.
 
ujana ni nusu ya uwendaazimu ila mimi nasema hivi ujana ni wendaazimu kamili maana utakuta mtu enzi za ujana wake anajihusisha na mahusiano na mabinti tofauti tofauti akisha wapa ujauzito anawakimbia...baadae anarudi kudai watoto kama si wendaazimu huo ni nini..? mimi nadhani hii yote ni kutokana na upungufu wa imani na mpolomoko wa maadili. na hii ndio upelekea watoto kunyanyasika na kujikuta wanakosa malezi bora ya wazi wawili. asikwambie mtu akuna kitu kizuri kwa mtoto kama kulelewa na wazazi wake wote wawili {ukiacha kufariki}
hqdefault.jpg

tuwahurumieni watoto jamani ukiwa kama kijana hakikisha unapanga uzazi na mtu sahihi ambae ndie utakaeanzisha nae familia kinyume na hapo utamuathiri mtoto kisaikorojia maana atatamani sana malezi ya wazazi wake wawili atakosa ata ukisema umchukue mwanao uishi nae mara nyingi wazazi wakufikia huwa hawana urafiki kabisa na watoto wasiokuwa wakwao...mtoto atanyanyasika sana na wengine hupoteza kabisa muelekeo wa maisha....
11-30-2015Central_African.jpg

vijana wenzangu tuutumie ujana wetu vizuri, kama wewe umelelewa na wazazi wako wote wawili kwanini umtafutie mwanao matatizo...? nimegundua chanzo kikubwa siku hizi cha watoto kukosa maadili kwa kiasi kikubwa kinachangiwa sana na kukosa malezi ya wazazi wote wawili...sijui ni ujinga maana elimu ya uzazi tunaanza kufundishwa tokea tukiwa darasa la 5 lakini bado tuu haitusaidii kuepuka mimba zisizotarajiwa
lonely-african-child.jpg

baadae mtoto akikuwa anakuja kuwa jambazi anakuchukia mzazi wake...au anakuja kufanikiwa baba umepigika unaanza kujirudisha kisa mtoto kawa super nyota kutwa anasomwa magazetini na redioni anasikilizwa...hii ni aibu kubwa sana maana malipo siku zote ni hapa hapa duniani...kuyaepuka hayo hakikisha unapanga uzazi na mtu sahihi ambae utakuwa teyari kuanzisha nae safari ya maisha...
Ila ni mara chache na kwa watu wachache hutokea wakapanga na kudhamiria kuzaa au kuzalisha kabla ya kuoa au kuolewa toafauti na hapo hakuna anaye jua atakuwa single mother au single father kama wapo lakin,,hivyo hayo uyasemayo si mabaya bali ni ni nadharia zaidi ,maana waweza olewa au oa kabla ya kuzaa na tena wote mkiwa bikra lakin mwisho wake ukajikuta umekuwa single mother/father na sababu wala isiwe kifo

Maisha hayana formula kama hesabu , kila mtu ana njia yake na haita wezekana wote tukapita njia moja hilo haliwezekani.
 
@Kikmondoa unaweza sema ni madharia sababu hayajakukuta...hujawahi ona mama wa kambo akitesa mtoto nadhani...yani wanawake wanaukatili next level...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom