Kabla hujaolewa fikiria miaka 10 ijayo itakuwaje! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kabla hujaolewa fikiria miaka 10 ijayo itakuwaje!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Jul 16, 2012.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ndege wa tabia moja huruka pamoja! Ujana ni fahari pia ni wakati wa kufanya maamuzi muhimu kumchagua yule utatumia muda wako wote unaobaki duniani.
  Pia mapenzi ni matamu, na kupendwa kutamu, wakati mwingine mapenzi huanza polepole na inafika siku yanakuja yanakufagia miguu yote, hata kabla hujajitambua vizuri unajikuta tayari upo kwenye ndoa kupitia kasi ya ajabu kwa jina la "Love is Blind"

  Ndoa ni kupenda, ni commitment ya maisha, kukubali ndoa maana yake ni kukubali kwamba upo tayari kutoa kila kitu na kijikabidhi kwa mtu mmoja tu maisha yako yote, ndoa ni ahadi na agano la kumpenda yeye sasa na hadi kifo kitakapo watenganisha.

  Ndoa ni zaidi ya unavyojisikia (feelings) ni zaidi ya mguso unaoupata ndani ya nafsi yako, ndoa ni kuudhihirishia ulimwengu kwamba umechagua kumpenda mtu mmoja, maisha yako yote, na kabla hujaanza kuvuna unachopanda sasa ni vizuri kufikiria kwanza huku ukiwa na akili timamu ili usije siku ukamlaumu mtu hahaha nisikutishe hakuna kitu kitamu kama ndoa!

  UMERIDHIKA NA TABIA YAKE?
  Naamini mpenzi wako ni the sweetest, cutest, lovable, barafu la moyo wako, is a real honey na majina mengine mengi tu, anakupa raha na unajisikia hakuna mwanaume kama yeye duniani anayekupa ridhiko la moyo ila ni yeye tu, kweli uchumba ni mtamu, ukitaka chochote anakupa, anapenda akuone kila wakati.

  Kabla hujafika mbali na kutoa maamuzi jaribu kufikiria kwanza kwa makini zaidi zile tabia ambazo unahisi hujaridhika nazo.
  Unajifariji kwa kuwa anakupenda basi ukiolewa naye utambadilisha au ataacha tu.

  Uzoefu unaonesha kwamba vitu vingi ambavyo unaona sasa ndiyo vinakuvutia kwake kama vile jinsi anavyoongea, jokes zake, n.k vinaweza kukupa raha kwa muda mfupi sana wakati huu lakini ukishazoena naye baada ya kuoana naye, utatamani awe na kitu kipya kitu ambacho kwake haitawezekana na wewe utaanza kuwa bored.

  Utani na jokes ni raha kwa unaposikia kwa mara ya kwanza au kwa mtu unayekuwa naye kwa mara ya kwanza, ila akishazoeleka ukajua kila kitu kuhusu yeye inakuwa kwisha kabisa anakukinai.
  Kama ni mwanaume mwenye utani na jokes basi inabidi uwe una develop new skills za jokes zako kila baada ya muda fulani kabla ya expire date.

  Vile vitu umekuwa unavipenda kwake sasa vinaweza kuwa usumbufu miaka 2 ijayo.

  Ni vizuri kuangalia tabia endelevu ambazo hata baada ya miaka 10, 15 au 20 bado kwako hazitaleta shida.

  Wazo kuu ni kwamba angalia miaka 10 ijayo maisha na yeye yatakuwaje kama unaona yatakuwa supper basi ingia kichwakichwa maana hakuna shida ila ukihisi unaona mawingu please think twice!

  Inawezekana anamwamini mama yake kuliko wewe mke mtarajiwa na amekwambia bayana linapokuja suala la maamuzi mama yake ndiye top,
  Inawezekana amekuahidi kwamba yupo tayari kuacha dini yake kwa ajili yako, hata hivyo uwe makini kwani suala la dini ndilo linafanya watu wauane duniani,
  Inawezekana anajua kuutwika na sasa ametulia kidogo anasubiri uingie ndani ya 18 na wewe umejifariji kwamba utambadilisha, mara nyingi baada ya kuingia kwenye ndoa wanawake ndio hubadilika.
  Inawezekana anavuta sana sigara na kwa sasa anavuta sigara moja kwa siku kwa sababu anakupenda, kumbuka wote wanaovuta sigara ukiwauliza watakwambia wanataka kuacha kuvuta sigara, fikiria maana bedroom inaweza kuwa tray vipisi vya sigara zake.

  Inawezekana unajidanganya eti anakupenda hivyo tabia zake mbovumbovu ataacha unajifariji tu au unawezekana ume-fall in love na image, au hisia zako (feelings) ambazo zimezikosa upendo wa mwanaume.

  Ndoa si 50/50 wala 100/100 bali ni 150/150 yaani kujitoa kwa ajili ya mwenzako zaidi ya asilimia mia, kwamba umechagua kazi ya kumpenda huyo mwanaume hapa duniani yeye tu bila kujali amefanya nini.

  Pia usikubali kuolewa kwa sababu ndugu zako wanakushauri kwamba uolewe au kwa sababu sasa unahisi mwili unawasha sana unahitaji mume wa kukuridhisha au kwa sababu rafiki zako wanakusema sana kwamba mbona huolewi.
  Au kwa sababu kiongozi wako wa dini anasema uolewe, olewa kwa sababu ni wakati wako na kwamba umekubali mwenyewe baada ya kukaa na kufikiria kwa makini na kumkubali mwanaume huyo.
  Kawaida dunia nzima inaweza kukushauri na kukusema hata hivyo mwamuzi wa mwisho ni wewe maana wewe ndiye utakaye kuwa na huyo mwanaume siku meli yenu ya ndoa itakapokuwa inapita kwenye kina kirefu cha maji wakati wa dharuba kali, usiwategemee wanadamu kwani ndivyo walivyo ni vigeugeu.

  Zaidi omba Mungu akupe amani ya kweli na huyo mwanaume ili uwe na uhakika na uamuzi unaenda kuutoa.

  “Marriage is a school in which the pupil learns too late.”

  Kama haupo makini kuchagua partner mzuri wakati wa kuolewa basi hiyo sentensi inaweza kuwa ni ukweli mtupu.
  Hahahahahaha mnashangaa hii picha! ni pete za ndoa hizo.

  AMEN............
   
 2. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  haya mambo huwa hayana formular bana, ni kujitosa tu mbele kwa mbele.... wengi wanaojifanya mabingwa wa kuzingatia vigezo na masharti ya kuchagua a better life partner huishia kuwa surprised
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ni kweli hayana formula ila yana misingi ya kufuata...
   
 4. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Umeeleweka mkuu
   
 5. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  nakubaliana na wewe mkuu,ni kujivisha mabomu tu LIWALO NA LIWE....lol:redface::redface:
   
 6. EARPHONE

  EARPHONE JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 357
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hahahaaa...'kujivisha mabomu tu LIWALO NA LIWE' Ok!Maisha ni kuchagua....somo lako ni zuri sana.
   
Loading...