Kabla hujamkopesha mtu pesa jiulize maswali haya ili usiingie kwenye majuto baadaye.

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,119
Habari!
Watu wa zama hizi, wa mjini na vijijini wengi hawana aibu kumkopa mtu. Uvumilivu katika matatizo yanayohitaji pesa haupo.
Mtu ukimsimulia mafanikio yako au mipango yako tu umemfungulia mlango wa kukukopa.
Utafiti usio rasmi unaonyesha kuwa wanaokopeshana kienyeji(kindugu na kirafiki) wanaolipana ni chini ya 50%.
Wengi huishia kuvunjiana urafiki na undugu baada ya kutolipana.
Kabla hujamkopesha mtu pesa jiulize haya;
1. Pesa ya kulipa ataitoa wapi?
Kama anakuambia ataipata sehemu fulani, je, kiasi anachokwenda kukipata kitatosha kulipa deni kwako naye akabakiwa na pesa nyingine kwaajili ya matumizi yake?
2. Kwanini amekosa kuwa na hiyo pesa mfukoni mwake mpaka anakuja kukuazima wewe?
3. Je, hana madeni sehemu nyingine ?
Kuna watu wanadaiwa na watu wengi, imefika wakati wanakopa huku wanapunguza deni kule . Mtu mwenye madeni mengi usitegemee akulipe pesa yako kirahisi.
4. Je, mali anazomiliki zina thamani zaidi ya kiasi anachokukopa?.
Usipozingatia haya wewe utaishia kutoa sadaka ya lazima kwa watu mpaka ulie na hutaendelea.
Yote kwa yote.
Ni vizuri mkaandikishiana unapomwazima mtu fedha ambayo hutaweza kumsamehe.
 
Sheria yangu ya kwanza kabla hata sijajiuliza hayo maswali......

Simkopeshi mtu aliyembali na mimi,

Mdeni sugu akiona simu au msg zako za madai anachukulia msg au calls zako kama zile Customer care za Muito kwa mpigaji....

Sijawahi mkopesha mtu niliyekaribu naye akaacha kulipa zaidi ya kuchelewesha..
Hapa namaanisha mtu ambaye mda wowote nikitaka namuona.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom