Kabla hujaanzisha thread mpya kuhusu Nassari fikiria kuwa MU=change in TU/Change in Q | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kabla hujaanzisha thread mpya kuhusu Nassari fikiria kuwa MU=change in TU/Change in Q

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hofstede, May 11, 2012.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Tokea Nassari alipo-misspoke last week jukwaani kumekuwa na harakati za makusudi za ku-seize the moment na kujenga mlima kutokana na kichuguu. Japo sikuwa nimeafiki jinsi kauli ile ilivyokuwa framed lakini nilimuelewa Mbowe alipotoa ufafanuzi na ku-refute kauli ile on spot. Kwa watu makini kitendo cha Mbowe kiliifanya kauli ile kukosa nguvu umuhimu tena katika siasa za Tanzania. Kwani tukianza kuchambua kauli za wanasiasa majukwaani tutafikia hitimisho kuwa kauli ya Nassari ilikuwa ni sawa na sisimizi kwenye kundi la wanyama wengi tu Tembo na Nyangumi wakiwemo.

  Kumekuzuka mchezo katika vyombo vya habari na hasa hata hapa JF kuanzisha thread kila baada ya saa moja inayozungumzia kauli ile. Ukweli mimi binafsi nimekerwa sana na effort hii ya kujenga mlima kutoka kwenye kichuguu. Tanzania ina matatizo mengi sana, vijana wengi hawana ajira, mahospitali hayana dawa na madaktari hawana vitendea kazi, mfumuko wa bei unazidi kupaa, watanzania kila kukicha inakuwa ni afadhali ya jana, wizi wa mali ya umma bila wahusika kuchukuliwa hatua stahiki. Haya ndiyo mambo ya kuyazungumzia kwa sasa kwani yana madhara ya moja kwa moja katika maisha ya kila siku ya watanzania. Kuzungumzia kauli ya Mbunge mmoja ambaye hajatimiza hata mwezi mmoja tokea ale kiapo ni kupoteza muda wa kushughulikia mambo muhimu yanayowagusa watanzania na nchi moja kwa moja.

  Isitoshe nguvu hizi zinatufanya hata watu ambao tulikuwa wa kwanza kukosoa kauli ya Nassari kwa lengo la kujenga kujikuta sasa tukianza kupata sababu na njia mbadala ya kuanza kujenga hoja za kumtetea Nassari, binafsi hili huenda lisiwe jambo zuri kwa Nassari kwani nina hakika kuwa amejifunza kitu kikubwa sana katika siasa za majukwaani kutokana na instant reaction ya Mbowe.

  Lakini kibaya zaidi nguvu hizi za kum-demonise Nassari zinaondoa dhana nzima ya speech aliyoitoa JK wakati akiapisha tume ya katiba kuwa tusizomeane eti kwa kuwa tu tunatofautiana kuhusu jinsi katiba mpya itakavyokuwa. Mawazo yote yasikilizwe hata ya mtu anayetaka bei ya korosho ipande wakati si mahala pake. Nilitarajia CCM na Nape wangeonesha kwa mfano kumuunga mkono rais anayetoka kwenye chama chao kwa kuacha nguvu hizi za kukandamiza mawazo ya mtu asiyekuwa na dola. Kauli ya Nassari tuipinge kwa kujenga si kuipinga kwa kubomoa na kupotosha na kumfanya Nassari ajisikie dhalili, hayo si malengo ya kukuza demokrasia. Sasa umefika wakati tuangalie kauli na matendo ya mtu.

  Kwa wale wenye uelewa kidogo wa uchumi na hasa microeconomics watakubaliana na mimi kuwa ladha ya kitu huwa bora pale unapokitumia kitu hicho kwa mara ya kwanza, na kila unapoongeza kipimo ndipo ladha hiyo hupungua zaidi na zaidi na zaidi. Tunapoongelea suala la Nassari zaidi na zaidi halitusaidii bali linafanya tuanze kuwachukia na kuwapuuza wale wanaoliendekeza. Tuangalie tusijikute tunajidharaulisha sisi wenyewe.

  MU = change in TU/change in Q (where TU is total utility and Q is the quantity of the good)

  Marginal utility is the additional satisfaction, or amount of utility, gained from each extra unit of consumption. Although total utility usually increases as more of a good is consumed, marginal utility usually decreases with each additional increase in the consumption of a good. This decrease demonstrates the law of diminishing marginal utility. Because there is a certain threshold of satisfaction, the consumer will no longer receive the same pleasure from consumption once that threshold is crossed.

  Take, for example, a chocolate bar. Let's say that after eating one chocolate bar your sweet tooth has been satisfied. Your marginal utility after eating one chocolate bar will be quite high. But if you eat more chocolate bars, the pleasure of each additional chocolate bar will be less than the pleasure you received from eating the one before - probably because you are starting to feel full. The same applies to the Issue of Nassari's statement on the political podium, when people critised him in the first place every body agreed, but when we critise him more and more, people no longer receive the same negative perceiption about Nassari beacuse they feel loaded with unnecessary information.

  Be careful critiques!   
 2. K

  Kiboko Yenu JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 312
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nassari alitumwa na padri slaa
   
 3. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good analysis..I understand.I give u thumb up 4 widening the minds of ignorants.Indeed we are tired of endless nonsense critique on Nassari,lets discuss issues..
   
 4. Mu-Israeli

  Mu-Israeli JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 2,456
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Oohoooo!!
  Tukizungumzia kuhusu kutumwa, huyu hapa alitumwa na nani ???

  View attachment 54071 Kudadadeki !!!!
   
 5. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hofstede,
  Hawa ndugu zetu ambao ni Form II Leaver kina ritz & Co sijui kama watakuwa wamekuelewa! Subiri tuone coment zao!

  TUMBIRI wa JF,
  P.O BOX - PM JF
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hivi Nape na CCM walitoa kauli gani baada ya Lusinde kuporomosha mitusi yake?
   
 7. I

  Iramba Junior Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu thanks! Kama kutakakuwa na mtu yeyote hususani CCM ambaye ataanzisha thread yoyote ya NASARI atakuwa ni mpumbavu wa kutupwa! Msiwe na wasi akina Riz & Co kwa lugha hii ya kigeni tafsiri yake ni hapo juu kwenye kiswahili!
  Well said mkuu, big up
   
 8. S

  STIDE JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Nina uhakika hapo kwenye hiyo mistari ya mwisho mwisho umetoka mweupe!!
   
 9. s

  santesandy JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana! Natoa wito kwa wenye akili timamu, tusiongelee swala hilo tena. Tuwaachie kina rejao, tume ya katiba, ritz &co.
   
 10. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na mwito. Ila tujue hata ku-comment kwenye thread hii bado kuendeleza malumbano yaleyale. Namna nzuri ya kusimamisha mjadala huu ni kuanza na thread hii - mtu unasoma, unapiga like ukipenda kisha unasepa. No more comments!

  Mkuu Hofstede ... Pokea like!
   
 11. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Hofstede Hata Lema alisemwa sana! Usiogope haya yote yatapita tuchape kazi! M4CHANGE :peace:
   
 12. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Walisema alikuwa anajibu mapigo kwa CHADEMA
   
 13. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Lusinde angekuwa chadema kile kipindi angeitwa kuhojiwa na Polisi kwa kutukana hadharani, double standard ndiyo kitu pekee kinachonifanya nisiishie kuwachukia tu polisi bali pia kuwadharau
   
Loading...