Kabla hujaagiza gari, pitia hapa kujua gharama kamili za ushuru na bandarini

Habari Mck,
Kwa mujibu wa tra calculator
Ushuru wa gari yako ni 11,029,645.19
Na bei ya kuifikisha gari hadi bandari ya Da es salaam, kwa sawa sawa na screenshot yako ni
10,742,976

11,029,645.19 (Ushuru)
10,742,976 (CIF)

Inakua : Tshs
21,772,621.19


Handling ni $7 jumlisha VAT (18%) per cbm (cubic meters)
Ile gari ina 14.621 CBM

Kwahiyo unafanya $7*14.621 = $104 plus VAT (18%)
$122.72
Kwahiyo handling inakua $122.72

CORRIDOR LEVY ;
$0.3 plus vat per cbm

$0.3*14.621 = $5 + 18% VAT = $5.9

Kwahiyo Corridor levy inakua $5.9


WHARFAGE :
Hii huwa ni 1.6% ya thamani ya cif
Cif value ya gari yako ni $4,640

$4,640*1.6% = $74.24

Kwahiyo wharfage ni $74.24

TUJUMLISHE

Handling = $122.72
Corridor levy = $ 5.9
Wharfage = $74.24

= $202.86

Uki change kwa TZS inakua Tshs 476,000
Jumlisha agency fee (200,000)


Inakua Tshs 676,000

USHURU NA GHARAMA ZA KULETA HII GARI TULISEMA JUMLA NI

Tshs 21,772,621.19

Kwahiyo Tshs 21,772,621.19 jumlisha 676,000

Inakua TSHS 22,449,000 (Hiyo ndiyo budget kamili ya kumiliki hilo gari .. yaani hadi kuwa nalo mikononi .. bima haijajumuishwa)
Asee kumbe jamaa huwa wanatupiga sana
 
TOYOTA VOLTZ

Cif = Tshs 6,891,000
Ushuru = Tshs 7,048,000= 13,039,000

Handling = $7*12.348 = $86.436+ 18% vat = $102
Corridor levy = $0.3*12.348 = 4 + 18% vat = $4.72
Wharfage = 1.6%*2,976 = $47.616

= $155 = Tshs 364,000

Pllus agency fee 200,000

= Tshs 564,000


13,039,000 + 564,000

= Tshs 13,603,000

(Hapo hadi kuitoa bandarini na kuwa mikononi mwako, bima haijajumuishwa)
Na labda kama budget inakua imebana kwa sababu za wingi wa kimajukumu

Unaweza kuiagiza gari hii kupitia Semsella ENTERPRISES
Badala ya kulipia 13,603,000
Unalipia 10,202,250 tu
Gari ikifika, unakabidhiwa

3,400,750 iliyobakia unaimalizia kwa instalment
Ya muda wa miezi 7
Kila mwezi 486,000

Instalment zinaanza mwezi mmoja baada ya kukabidhiwa gari lako.


Semsella Enterprises/ecarstanzania
P.o.box 63178, Dar es salaam
Shekilango, nhc plot number 242
Block number 1,1F
Call/text/Whatsapp text us 24/7
+255745229947
Hivi hii nchi ina shida gani? Inakuwaje gharama za kutoa Gari zinazidi thamani ya Gari lenyewe? Absurd

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nipe mahesabu kwenye link hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna ya 2010 na 2007.
Screenshot_2019-04-16-11-34-10-060_com.android.chrome.jpeg
Screenshot_2019-04-16-11-18-52-977_com.android.chrome.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Mck,
Kwa mujibu wa tra calculator
Ushuru wa gari yako ni 11,029,645.19
Na bei ya kuifikisha gari hadi bandari ya Da es salaam, kwa sawa sawa na screenshot yako ni
10,742,976

11,029,645.19 (Ushuru)
10,742,976 (CIF)

Inakua : Tshs
21,772,621.19


Handling ni $7 jumlisha VAT (18%) per cbm (cubic meters)
Ile gari ina 14.621 CBM

Kwahiyo unafanya $7*14.621 = $104 plus VAT (18%)
$122.72
Kwahiyo handling inakua $122.72

CORRIDOR LEVY ;
$0.3 plus vat per cbm

$0.3*14.621 = $5 + 18% VAT = $5.9

Kwahiyo Corridor levy inakua $5.9


WHARFAGE :
Hii huwa ni 1.6% ya thamani ya cif
Cif value ya gari yako ni $4,640

$4,640*1.6% = $74.24

Kwahiyo wharfage ni $74.24

TUJUMLISHE

Handling = $122.72
Corridor levy = $ 5.9
Wharfage = $74.24

= $202.86

Uki change kwa TZS inakua Tshs 476,000
Jumlisha agency fee (200,000)


Inakua Tshs 676,000

USHURU NA GHARAMA ZA KULETA HII GARI TULISEMA JUMLA NI

Tshs 21,772,621.19

Kwahiyo Tshs 21,772,621.19 jumlisha 676,000

Inakua TSHS 22,449,000 (Hiyo ndiyo budget kamili ya kumiliki hilo gari .. yaani hadi kuwa nalo mikononi .. bima haijajumuishwa)
TRA noma kodi milioni 11wanatengeza wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipe mahesabu kwenye link hiyo
Sent using Jamii Forums mobile app
Model:VANGUARD
Year of Manufacture:2010
Engine Capacity:2001 - 2500 CC
Customs Value CIF (USD):8,631.00
Excise Duty due to Age (USD):1,618.31
Total Import Taxes (TSHS):17,333,323.66
Vehicle Registration Fee (TSHS):500,000.00
TOTAL TAXES (TSHS):17,833,323.66

CIF$7,614
(Approx. Exchange Price: TSh 17,626,405)
Duh huu mgari kiboko ngoja aje Semsella na mm nashangaa mbona gari haijafiisha iaka 10 bado inachajiwa Excise Duty due to age? wakati nikijua walishasamehe hii kitu
Duh kabla ya kuitoa Bandarini na kina MAGARI7 wanadai jumla 35,459,728.66
 
Nissan Leaf EV Auto 5 dr ya 2013 naomba unipe ushuru ni ngapi mkuu
Hii ni ya umeme

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Kutafuta kodi huwa nachukua CIF ya gari nazidisha mara 2.5 just incase.
Kama gari inauzwa 10M. Basi prohection ya kodi naweka 25M.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hawa TRA bado kikokotoo chao hakieleweki kinaweza kukubadilikia wakati wowote, kumbuka walisema zisiingizwe gari zilizozidi miaka 10 ikiwa hivyo zitachajiwa zaidi
hii kodi yao ni mara 2 ya manunuzi hata kwa gari la zaidi ya miaka 20
HAPA
kwanini kuna tofauti ya ukokotoaji wa magari wakati ni aina moja, mwaka, cc ya injini petrol, na yote yanatoka Japan mfano
Harrier ya mwaka 2000 (ushuru ni 7,664,094/ na alteza ya 2000 ni 4,452,927/)
1073067
 
Hivi hapa bongo hamna yadi inayouza magari mapya kwa gharama zinazoshabihina na hizo za nje..ili kuepusha hayo mambo ya bandarini sijui..
Sent using Jamii Forums mobile app
hata kwenye hizo Yard ushuru wa TRA upo palepale
Labda ununue kwa mtu ambaye tayari keshalipia huo ushuru wa kuingiza Nchini na kapewa namba lakini usithubutu kuingiza hata gari la bure au zawadi, ili lisajiliwe lazima uingie kikokotoo hicho na ulipe
kama Harrier ni ya bure lazima ulipie ushuru milioni 7
 
Habari ndugu,

Calculator inafanya kazi sawia kabisa .. na ndio hiyo tunayoitumia.
Lakini, elewa kwamba, baada ya ushuru, kuna gharama zingine za bandari n.k
Gharama ambazo huzikuti kwenye kikokotoo cha Tra.

Kwa sababu hiyo, watu wengi wamekua wakipewa gharama kubwa ambazo sio sahihi na baadhi ya watu (wakutoa magari/kuagiza) ambao sio waaminifu.

Ndio maana nimejitolea kufafanua hizo gharama hapa.


Natumai umenielewa.


Ikiwa kuna mahali unaona labda napotosha kwa namna iwayo yote ile
Nakuomba, unisahihishe.

Ahsante.
gharama za bandari na shipping line hazizidi hata laki 5!
 
gharama za bandari na shipping line hazizidi hata laki 5!
"Ndakilawe, post: 31119012, member: 47759"]
Nenda kwenye TRA calculator
MUWE WAKWELI wakati watu km MAGARI7 kaweka bayana na evidence na wewe tushushie za Kampuni yako au uwezo wako wa kutoa Vanguard, Harrier au Land Cruiser maana nikisema Coster hizo CBM na VAT nina uhakika ni zaidi ya laki 5 labda km Vits na kina Opa ndio laki 4
 
Back
Top Bottom